Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo kwani kuamka salama ni ushindi mkubwa katika maisha yako hivyo tumia ushindi huo wa uhai kuacha alama siku hii ya leo kumbuka kuwa maisha ni muda. Kumbuka kuiendea siku hii ya leo kwa misingi yetu ya Amka Mtanzania ya nidhamu, uadilifu na kujituma.

Rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena siku hii ya leo katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Kwa namna ya pekee rafiki yangu, nakusihi sana tusafiri pamoja hadi mwisho wa somo letu la leo ambapo leo tutakwenda kujifunza kitu muhimu sana cha kuzingatia katika maandalizi yoyote yale  hivyo basi,  karibu tujifunze.

Ni kawaida sana katika jamii yetu pale tunapokuwa tunahitaji kufanya jambo lolote huwa tunapata muda wa maandalizi. Maandalizi hayo hufanyika kwa vikao mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha mambo siku ya tukio husika. Chochote unachotaka kufanya lazima utahitaji kufanya maandalizi kwa namna moja au nyingine.

Kwahiyo, tunafanya maandaizi mengi sana katika maisha yetu. Ukitaka kulima lazima utaanza na maandalizi ya kuandaa shamba, ukitaka kujenga nyumba lazima utahitaji maandalizi muhimu kama vile kiwanja na vifaa vya ujenzi vinavyohitajika katika gari. Ukitaka kupika chakula lazima utakua na maandalizi ya mahitaji muhimu ili chakula chako kiwe katika uhalisia wa chakula unachokihitaji.

Licha ya kufanya maandalizi hayo muhimu sana lakini bado kuna kitu muhimu sana ambacho kikikosekana katika maandalizi basi maandalizi hayo yanakuwa ni hakuna. Rafiki, kitu muhimu katika maandalizi ni ufanisi. Maandalizi bila ufanisi ni sawa na hakuna kitu. Hata ufanye maandalizi ya mwaka mzima lakini kama hujafikia katika viwango vya ufanisi maandalizi yako yanakuwa hayana maana.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kuondokana Na Hali Ya Kukosa Uthubutu Na Kuingia Kwenye Biashara Itakayokufikisha Kwenye Ubilionea.

Mpendwa msomaji, maandalizi yoyote yanadai ufanisi wa hali ya juu. Kama unawaambia watu uko katika maandalizi na ili maandalizi yako yawe ya uhakika basi unahitaji kuonesha ufanisi wa kile ulichokuwa unakihangaikia muda wote. Changamoto kubwa ya watu wengi siku hizi ni kuwa na maandalizi lakini wanakosa kitu muhimu ambacho ni ufanisi.

Vikao, mikutano inakuwa ni mingi lakini mara chache sana vikao au mikutano hiyo kuja na maazimio ya ufanisi. Tunapokuwa na maandalizi basi tunaalikwa kukumbuka kuwa maandalizi yanaenda na ufanisi bila ya kuwa na ufanisi basi maandalizi yetu yanakuwa hayana maana kubwa katika maisha yetu.

Hatua ya kuchukua leo, kama unafanya maandalizi ya kitu chochote kile hakikisha kinakuwa na ufanisi mkubwa. Maandalizi bila ufanisi ni sawa na hakuna kitu.

Kwahiyo, haijalishi utakaa kwenye maandalizi juu ya kitu fulani kwa muda gani, ila watu wanahitaji kuona ufanisi wa kile ulichokalia maandalizi. Ufanye maandalizi muda mrefu, ufanye muda mfupi lakini kikubwa kinachoitajika katika maandalizi ni ufanisi wa hali juu.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net  au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com kwa kujifunza zaidi kila siku. Asante sana.