Kila mtu ana kitu anachokifanya katika maisha yake kila siku. Kila mtu kitu hicho hutaka kukimalisha kwa ukamilifu wote bila kupoteza muda. Lakini jambo la kushangaza kuna wakati kile unachokifanya huwa hakikamiliki.

Utakuta umepanga vizuri tu kwamba, leo nitafanya jambo hili kuanzia hapa na kuishia pale, lakini inapofika mwisho wa siku pale ulipokuwa umepanga kwamba utafika haufiki na wakati mwingine hata nusu yake unakuwa hujafika kabisa.

Hali hii imewakuta watu wengi sana, miongoni mwao ni wewe. Na changamoto kubwa inayotokea unapokutana na hali hii, inakuwa ni hali inayokurudisha nyuma kwa kiasi fulani, hasa ukiangalia mbona unaweka juhudi lakini kwanini hazifikiki.

Najua kwenye maisha yako kuna wakati lazima umeshakutana na kitu kama hiki na mara nyingi hujui chanzo chake ni nini. Hata hivyo pia si wewe tu peke yako, ukiangalia karibu kila mtu amekutana na hali hii ya kushindwa kukamilisha majukumu yake.

brain fit press release elements

Naomba nikuulize, umeshawahi kujiuliza chanzo chake hasa ni kitu gani. Ni nini kinachosababisha hasa wewe ushindwe kukamilisha ile kazi uliyojiwekea? Ni jambo la kawaida kutokukamilisha au ni uzembe au ni kitu gani hasa?

Sitaki uumize kichwa sana kujiuliza majibu ya swali hilo, makala haya inayo majibu tosha ya kukuonyesha wewe mambo ambayo ukiyafanya yatakuzia moja kwa moja ushindwe kukamilisha kazi yoyote kwa ufanisi unaotaka.

  1. Mwingiliano wa vitu vidogo vidogo.

Kabla sijasema kitu chochote hapa jibu rahisi hapa la kwanza ni mitandao ya kijamii. Kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana wa mitandao ya kijamii na kazi tunazozifanya. Watu wamekua hawataki kufanya kazi moja kwa moja bila kuingia kwenye mitandao.

Kwa mfano kwa sasa, utakuta ni ngumu sana kwa mtu kuweza kufanya kazi yake angalau hata kwa saa moja tu bila kuangalia simu yake ya mkononi. Utakuta anachoangalia huko si kingine bali ni nini katumiwa kwenye mitandao yake.

Kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii ikiwemo ‘facebook, whats app’ na mingineyo imekuwa ni chanzo kimojawapo cha watu kushindwa kutimiza shughuli zao muhimu za kila siku kwenye maisha.

Soma; Sumu Hatari Inayokumaliza Taratibu Kisaikolojia.

  1. Kusahau majukumu yako ya siku.

Kitu kingine kinachokufanya wewe ushindwe kukamilisha majumu yako muhimu ya siku ni kwa sababu ya kusahau majukumu yako ya siku ni yapi. Unaamka asubuhi badala ya ufanye moja kwa moja kazi zako unaanza kujiuliza hivi leo naanzia wapi?

Kwa kijiuliza swali kama hili ni matokeo mabovu ya kutokuipangilia siku yako mapema, kwa hiyo kwa vyovyote vile ni lazima kukamilisha majukumu yako itakuwa ni ngumu kidogo kuweza kutokea kwa sababu huelewi hasa wapi unaanzia na utapoteza muda sana.

Inatakiwa kila kitu kiwe kwenye karatasi kwamba utafanya nini na baada ya kitu hicho kwisha nini kitafatia tena. Kinyume cha hapo utaendelea kuteseka na kutokukamilisha majumu yako karibu kila siku. Dawa ya hili panga mambo ya kufanya siku moja kabla.

  1. Kulala sana.

Ndio, sijakosea nimesema kulala sana. Kitaalamu inashauriwa kulala saa 8 lakini wapo watu wanaozidisha au kulala masaa hayo hayo ambacho si kitu kizuri sana kama una majukumu ya msingi ya kila siku na yanayokutaka wewe moja kwa moja.

Lazima ifike mahali ufanye kitu cha ziada ikiwa pamoja na kuamka angalau saa moja kabla kama ulivyozoea kila siku. Ifike mahali uwe ‘extra ordiary na sio ordinary.’ Unapokuwa ‘extra ordinary’ unakuwa mtu wa kufanya kwa ziada yaani kwenda mbele kidogo.

Lakini kuendelea kuchapa usingizi kwa muda mrefu halafu ukitegeme kuna majukumu utayakamilisha yote naomba usahau. Swala la usingizi mzito na wa nguvu waachie watoto. Kama kulala ni kweli lala ila usipite viwango, unatakiwa kuchapa kazi.

Soma; Jinsi Ya Kuishinda Hofu Ya Wengine Wananichukuliaje.

  1. Kutumia muda mwingi kuifikiria ndoto yako.

Hata siku moja ndoto yako haiwezi ikawa ya kweli eti kwa kuifikiria sana. Naomba usijadanganye katika hili, ndoto yako itakuwa ya kweli kama tu umeamua kujikita na kuifanyia kazi kila siku.

Sasa inawezekana unashindwa kukamilisha majukumu na kazi zako kwa sababu tu ya kufanya kazi kwa kufikiria ndoto yako zaidi. Hapa yaani nikiwa na maana unaishi kwa hisia zaidi badala ya kuishi kwenye uhalisia wenyewe.

Kama unafikiria sana ndoto yako na huchukui hatua, utajikuta kweli hakuna ambacho umekifanya hata kimoja. Kama unataka kukamilisha majukumu yako kwa uhakika chukua hatua kila siku, hatua hizo zitakusogeza kwenye ndoto yako.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; http//www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

 

 

 

 

 

.