Habari za leo rafiki yangu?

Hongera kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo, hii ni fursa ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Leo napenda nikupe taarifa muhimu sana za likizo yangu kwa mwaka 2017 na hatua muhimu kwako kuchukua ili mwaka 2018 uwe bora kwako.

Likizo yangu kwa mwaka 2017.

Mwishoni mwa mwaka 2014 nilianza utaratibu wa kujipa likizo ya wiki moja, ambapo kwa wiki hiyo nimekuwa nakaa mbali na mitandao ya kijamii, shughuli zangu za aina yoyote na hata mawasiliano yanakuwa yale ya lazima pekee. Katika likizo hizi nimekuwa nafanya mambo matatu makubwa; kusoma kwa kina zaidi, kutafakari na kutahajudi na kuweka mikakati ya kuboresha zaidi shughuli ambazo ninazifanya.

Tangu nilipoanza zoezi hili mwaka 2014, limekuwa na manufaa makubwa sana kwangu na kwa shughuli zangu pia. Huduma zote ambazo nimeweza kuanzisha na kuendeleza yamekuwa ni mawazo ambayo nayapata katika kipindi hichi.

Mwaka huu 2017, kwa mara ya nne nachukua likizo yangu hii ya wiki moja kwa ajili ya mambo yale makuu matatu, kusoma kwa kina, kutafakari na kutahajudi na kuweka mikakati ya kuboresha zaidi.

Likizo hii ya siku saba kwa mwaka huu itaanza Alhamisi tarehe 21/12/2017 mpaka Jumatano tarehe 27/12/2017.

Katika kipindi hichi cha likizo sitakuwa napatikana kwenye njia nyingi ambazo huwa napatikana, kama mitandao ya kijamii, na hata mijadala mbalimbali ya KISIMA CHA MAARIFA na AMKA MTANZANIA. Mawasiliano kwa njia ya simu yatakuwa yale ya ulazima na haraka pekee.

Likizo hii siyo ya mapumziko kama zinavyokuwa likizo za wengi, bali hii ni likizo maalumu ambayo lengo lake ni kupata utulivu wa kuweza kufanya maamuzi muhimu ya kupiga hatua zaidi kwenye kila eneo la maisha yangu, na hatua hizi zitakuwezesha wewe rafiki yangu kupiga hatua zaidi.

Katika kipindi hichi cha likizo, sitakuwa natoa makala wala mafundisho kwenye AMKA MTANZANIA na hata KISIMA CHA MAARIFA, makala pekee zitakazoendelea kwenda hewani ni makala za KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Baada ya siku saba za likizo mambo yote yatarudi na nina imani yatarudi kwa ubora zaidi.

Nikutakie wakati mwema rafiki yangu katika kipindi hichi cha likizo, uendelee kujifunza kupitia makala mbalimbali na vitabu pia. Na pia nikutakie heri ya sikukuu za mwisho huu wa mwaka.

095a5b996f7db11bfe3b1d93a17b444b.0

Hatua muhimu sana kwako kuchukua ili mwaka 2018 uwe bora kwako.

Rafiki yangu, katika kipindi hichi cha mwisho wa mwaka, napenda kukukumbusha hatua hizi muhimu za kuchukua ili mwaka 2018 uwe bora na wa kipekee sana kwako.

  1. Endelea kujifunza sana.

Jifunze kupitia makala mbalimbali zilizopo kwenye AMKA MTANZANIA, www.amkamtanzania.com na KISIMA CHA MAARIFA, www.kisimachamaarifa.co.tz

Pia jifunze kwa kujisomea vitabu mbalimbali ambavyo vitakuwezesha kupiga hatua zaidi. Kuna vitabu vizuri sana kwako kujisomea kwenye www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu Pata na usome vitabu hivi ili uweze kuweka mikakati mizuri sana kwa mafanikio yako.

  1. Jiunge na huduma hizi mbili kama bado hujafanya hivyo.

Nina huduma nyingi ambazo ninatoa kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Zipo huduma za bure kabisa na zipo za kulipia. Kama bado hujajiunga na huduma za kulipia basi jiunge na huduma hizi mbili za kuanzia, ambazo kwa maoni yangu ni muhimu sana kama upo makini na mafanikio yako.

Huduma ya kwanza ni ya KISIMA CHA MAARIFA, hii itakupa nafasi ya kujifunza kila siku na kuweza kuzitengeneza fikra zako kwa njia ambayo utaweza kuziona na kuzitumia fursa ambazo zipo ndani yako. Maana hapo ndipo wengi wanapokosea na kukazana na fursa za nje huku za ndani wakiwa hawazioni. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA unapaswa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/=. Njia za malipo ni kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA 0717 396 253. TUMA ADA SASA (50,000/=), kisha tuma majina yako na email kwenye moja ya namba hizo na utaunganishwa.

Huduma ya pili ni KURASA KUMI ZA KITABU LEO, hii ni huduma maalumu ambayo nimeianzisha kwa wale ambao wanapenda kusoma vitabu ila hawapati muda wa kufanya hivyo. Ninaamini sana kwenye usomaji wa vitabu kwa sababu maarifa yote muhimu na siri zote za mafanikio zimefichwa ndani ya vitabu. Hivyo nimekuwa nawasihi sana watu wasome vitabu. Lakini wengi wamekuwa na vipingamizi kwamba hawana muda wa kusoma vitabu au fedha za kununua vitabu. Nimeanzisha program hii maalumu ya mtu kusoma angalau kurasa kumi pekee za kitabu kwa siku, kitu ambacho kitamwezesha kusoma angalau kitabu kimoja kila mwezi. Kwa kusoma kitabu kimoja kila mwezi, mtu anaweza kupiga hatua kubwa sana. Kujiunga na program hii mtu anapaswa kulipa ada tsh 10,000/= ada ambayo inalipwa mara moja pekee. Ada inalipwa kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha unatuma ujumbe wenye majina yako na maneno KURASA ZA KUMI ZA KITABU kwa njia ya wasap kwenda 0717 396 253.

  1. Tenga muda mchache kwako kutafakari na kutahajudi kwa kina kuhusu maisha yako.

Changamoto kubwa ambayo watu wanayo, hasa kwenye zama hizi ni kwamba watu hawafikiri tena. Watu hawataki kufikiri kabisa, wanataka vitu rahisi ambavyo wanaweza kuvifanya kwa urahisi. Wanavikosa halafu mambo yanakuwa magumu kwao.

Usikubali na wewe kuingia kwenye mkumbo huu wa watu ambao wanakwenda kama kuku waliokatwa vichwa. Badala yake tenga muda wa wewe kutafakari na kutahajudi kwa kina kuhusu maisha yako, kile unachofanya na kule unakokwenda. Ndani ya kichwa chako kuna mashine yenye uwezo mkubwa sana iwapo itatumika vizuri. Tumia mashine hiyo vizuri na itakuwezesha wewe kupata kile unachotaka.

Njia bora ya wewe kuweza kufikiri na kutahajudi, ni kutenga muda wa kufanya hivyo kisha kufanya. Usisubiri mpaka upate muda, bali tenga muda wa kufanya hivyo. Kwa kuweka muda na kuutumia kwa zoezi hilo, utanufaika sana na majibu utakayoyapata.

vitabu softcopy

Shukrani za kipekee kwako rafiki yangu.

Asante sana rafiki yangu kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja. Wewe umekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu na kazi zangu. Nikutakie kila la kheri unapoumaliza mwaka 2017 na uwe na mwaka wenye mafanikio makubwa 2018. Karibu sana tuendelee kuwa pamoja, mimi nipo kwa ajili yako na mwaka 2018 utazidi kuwa bora sana kwetu.

Karibu sana rafiki tuendelee kuwa pamoja kwenye huduma mbalimbali ninazotoa, tushirikiane pamoja kwa mafanikio yetu.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog