Rafiki yangu mpendwa,

Napenda kuchukua nafasi hii kukuarifu kwamba leo ndiyo siku ya mwisho kabisa kwako kupata nafasi ya kushiriki semina ya kukuwezesha kukuza sana biashara yako.

Hii ni semina ambayo nimeiandaa maalumu kwako kama mfanyabiashara na hata mfanyabiashara mtarajiwa, uweze kupata mbinu zitakazokuwezesha kuongeza faida kwenye biashara yako kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Kama umewahi kuwa na changamoto zozote kwenye biashara, basi chimbuko kubwa huwa linaanzia kwenye mzunguko wa fedha, ambao unategemea mauzo na ambayo yanatengeneza faida. Kama vitu hivyo havijakaa sawa, biashara haitakoma kuwa na changamoto.

Hivyo rafiki yangu, hii ni nafasi ya kipekee kwako kuweza kukuza biashara yako na kupata faida kubwa kupitia ongezeko la wateja na ongezeko la mauzo.

Semina hii ya biashara itakufundisha kwa kina maeneo muhimu matano ya biashara yako na hatua tano za kuchukua kwenye kila eneo ili kuweza kukuza ana biashara yako.

Mpaka unafika mwisho wa semina hii, utakuwa umejifunza mbinu 50 na utaondoka na mkakati ambao utaweza kuufanyia kazi moja kwa moja kwenye biashara yako.

Na muhimu zaidi, unaweza kupata nafasi ya mimi kufanya kazi na wewe moja kwa moja kwenye utekelezaji wa mikakati hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima ili uweze kuona ukuaji mkubwa zaidi wa biashara yako.

Lisha Akili

Kushiriki semina hii nzuri sana kwa ukuaji wa biashara yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, kupitia kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Ili kujiunga na kundi hili, unapaswa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh elfu hamsini (50,000/=) kupitia namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha unatuma ujumbe wenye majina yako kamili, email yako na namba ya simu kwa njia ya wasap namba 0717396253. Ukishatuma ujumbe huo utawekwa kwenye kundi na kuanza kujiandaa kwa semina yetu hii muhimu kwa ukuaji wa biashara.

Rafiki, vipo vitu ambavyo nimekuahidi kuhusu semina hii na kuhusu KISIMA CHA MAARIFA, ambavyo nataka nikukumbushe na uwe na uhakika na maarifa unayokwenda kupata na hata fedha yako pia.

Iwapo umelipia kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, na baada ya semina ukaona hakuna kikubwa ambacho umejifunza, unaweza kuniambia na nikakurejeshea ada uliyolipa, bila ya maswali ya ziada.

Na ukiona kipo cha maana unajifunza, ukakaa mwaka mzima ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, ukijifunza na kuchukua hatua, lakini mwisho wa mwaka maisha yako yakawa yako vile vile, hakuna hatua yoyote umepiga, unaniambia na nakulipa mara mbili ya ada uliyolipa.

Hayo mawili nakuahidi rafiki yangu na sitakuja kuvunja ahadi hiyo, maana hichi ninachofanya, nitakifanya maisha yangu yote na hivyo uaminifu kwangu ni nguzo muhimu sana.

Nakupa uhakika huu kwa sababu najua wengi wanakuwa na wasiwasi iwapo kuna kikubwa watakwenda kujifunza, hasa kama hujawahi kushiriki aina ya mafunzo ninayotoa. Ninachokuambia, lipia, pata mafunzo haya na utashukuru sana baadaye kwa hatua ambayo utakuwa umeichukua leo.

Kwa wale marafiki ambao hawataweza kabisa kushiriki semina hii, kwa sababu moja au nyingine, sitaki kuwaacha bila ya cha kufanya. Unajua mimi ni rafiki yako na ninakupenda na napenda kuona ukifanikiwa zaidi, iwe umelipia chochote ninachotoa au la, na  ndiyo maana kila siku nakuandikia makala za kukuwezesha kupiga hatua.

Kama hutaweza kushiriki kabisa semina hii ya ukuaji wa biashara yako, nataka uondoke na hili muhimu sana, na uanze kulifanyia kazi na ukiona kuna matokeo mazuri, nitafute nikupe zaidi.

Mafanikio yoyote kwenye maisha, na kwenye biashara yanatokana na vitu viwili; UNACHOJUA NA UNACHOFANYA. Ni hivyo tu, UNAJUA NINI na UNAFANYA NINI.

Ikiwa na maana kwamba, unahitaji kuwa na maarifa sahihi kabisa kwenye chochote unachofanya na maisha yako. Jua kwa undani kadiri uwezavyo, kila wakati jifunze na uelewe kwa kina kila unachofanya. Na kwa kuwa mabadiliko yanaenda kwa kasi, lazima uwe mbele sana kwenye kujifunza la sivyo utaachwa nyuma.

Baada ya kuwa umejifunza, unahitaji kuchukua hatua mara moja kwenye kile ulichojifunza. Unaweza kujifunza utakavyo, lakini kama hakuna hatua unayochukua, utakuwa unajifurahisha tu mwenyewe. Utaendelea kubaki pale ulipo, na tena inaweza kuwa hatari, maana utakuwa unajua sana kiasi cha kukata tamaa, ukiona huna cha kujifunza tena. Lakini ukiwa mtu wa kuchukua hatua, utaona una mengi zaidi ya kujifunza.

Sasa kwenye biashara yako, ili uweze kuikuza, nataka ujue vitu vitatu muhimu sana kuhusu biashara yako, yaani jua nje ndani.

Kitu cha kwanza; WATEJA.

Kitu cha kwanza unapaswa kujua kuhusu biashara yako ni wateja wa biashara yako. Unapaswa kujua sana kuhusu wateja wa biashara yako, kujua mahitaji yao, kujua maumivu yao, kujua nini kinawasukuma kununua na kujua wanamudu kulipia kiasi gani kwenye kile unachouza. Kadiri unavyojua kuhusu wateja wako, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwahudumia na kuweza kuikuza biashara yako.

Sasa ili kuongeza wateja zaidi kwenye biashara yako, unapaswa kufanya vitu viwili muhimu;

Moja; ongeza idadi ya wateja tarajiwa, hawa ni watu wanaojua kuhusu biashara yako. Maana kinachokuzuia kukua ni wengi kutojua kama hata upo kwenye biashara.

Mbili; ongeza kiasi cha wateja tarajiwa wanaokuwa wateja halisi. Mtu akijua kuhusu biashara yako, ni mteja tarajiwa, akilipa fedha kununua unachouza huyo ni mteja wa biashara yako. Unahitaji kuongeza idadi ya wateja tarajiwa wanaokuwa wateja halisi wa biashara yako.

Kitu cha pili; MAPATO.

Mapato ni eneo la pili muhimu sana unalopaswa kujua kuhusu biashara yako. Mzunguko wa fedha ndiyo damu ya biashara yako, kama hakuna mapato, hakuna biashara. Hata ukiwajua wateja wako kiasi gani, kama mapato hayapatikani na siyo mengi, biashara yako haiwezi kudumu kwa muda. Kadiri mapato ya biashara yanavyokuwa mengi, ndiyo faida inavyokuja kuwa kubwa mwishoni.

Sasa katika kuongeza mapato kwenye biashara yako, unahitaji kufanya vitu viwili muhimu sana.

Moja; unahitaji kuongeza idadi ya manunuzi kwa kila mteja wako. Wafanyabiashara wengi huwa wanakazana kumpata mteja, halafu cha kushangaza mteja ananunua mara moja na harudi tena. Kama ulikuwa hujui rafiki yangu basi jua leo, mteja akinunua mara moja tu kwenye biashara wewe umekula hasara. Faida unapata pale mteja anaponunua mara nyingi zaidi. Hivyo unahitaji kujua jinsi ya kuongeza idadi ya manunuzi ya wateja wako.

Mbili; kiasi cha manunuzi ambayo mteja anafanya anaponunua. Mteja akija kwenye biashara yako, akanunua kitu kimoja, usikubali aondoke na hicho pekee. Bali unahitaji kumshawishi anunue kitu kingine kinachoendana na kile ambacho amenunua. Wateja wanapenda sana kununua zaidi pale wanaponunua kitu kimoja, lakini wafanyabiashara wamekuwa hawawapi nafasi hiyo nzuri. Unahitaji kuhakikisha kila mteja anayekuja kununua kitu kwako, anaondoka na kingine cha ziada alichonunua.

Kwa njia hizi mbili, utaweza kuongeza mapato ya biashara yako.

Kitu cha tatu; FAIDA.

Faida ndiyo tunda la mwisho la biashara, hapa sasa ndiyo biashara inapona au kufa. Kwa sababu unaweza kuwa na mapato mengi sana, lakini huoni faida, na hapa ndipo wengi watakuambia hawajui fedha inaenda wapi. Ili biashara yako ikue, unahitaji kutengeneza faida, na siyo faida ndogo, bali faida kubwa sana.

Ili kuweza kuongeza faida kwenye biashara yako, baada ya kuwa kwamba umeongeza mapato, unahitaji kufanya kitu kimoja muhimu sana.

Kitu unachopaswa kufanya ni kuangalia kiasi cha faida kwenye kila unachouza, kuangalia gharama zote za uendeshaji wa biashara yako na kisha kuona wapi pa kuongeza kiasi cha faida na wapi pa kupunguza gharama. Ukiweza kufanyia kazi hili vizuri, utabaki na faida kubwa na utafurahia sana kuwa kwenye biashara.

Rafiki yangu, hayo ndiyo maeneo matatu muhimu sana kwa ukuaji wa biashara yako, unapaswa kuyajua nje ndani na unapaswa kuchukua hatua kwenye kila eneo.

Kama ulikuwa unafuatilia kila eneo kwa umakini hapo, utagundua mwisho wa siku kuna vitu vitano vya kufanyia kazi, wateja tarajiwa, kiasi cha wateja tarajiwa wanaokuwa wateja, idadi ya manunuzi, kiasi cha manunuzi na kiwango cha faida. Haya matano ndiyo tunakwenda kujifunza kwa kina kwenye semina hii ya ukuaji wa biashara. Ambapo kila eneo nitakushirikisha mambo 10 ya kufanyia kazi, na utakwenda kuchukua hatua mara moja.

Ili usikose nafasi hii ya kipekee sana, hakikisha leo hii, sasa hivi unajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, kwa kulipa ada ya mwaka kama ilivyokuelekeza hapo juu.

Na kama hutashiriki semina hii, kwanza usiseme huna fedha, kwa sababu kama kweli unataka kupiga hatua, kwa njia yenye uhakika, basi utakuwa tayari kufanya chochote kupata nafasi kama hii.

Hivyo tuseme hutashiriki, kwa sababu nyingine ambazo unazijua wewe, basi nakuomba sana rafiki yangu, fanyia kazi maeneo hayo matatu ya biashara yako na chukua hatua kwenye vipengele hivyo vitano. Anza leo na chukua hatua kila siku.

Nakusisitiza sana rafiki yangu kwenye hili, kwa sababu najua kwa hakika litakusaidia, halitakuacha hapo ulipo sasa. Hivyo nakuomba, jifunze na chukua hatua. Na kama utashiriki semina ninayokwenda kutoa, jiandae kwa hatua muhimu sana za kuchukua ili biashara yako ikue.

Nikutakie kila la kheri rafiki yangu, nikutakie mafanikio makubwa sana kwenye biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Rafiki na kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

MUHIMU; Nafasi pekee ya kushiriki semina ya ukuaji wa biashara yako ni kufanya malipo leo. Kama bado hujafanya hivyo na unajua unataka biashara yako ikue, fanya malipo sasa, ada ya mwaka tsh 50,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye majina yako, email na namba ya simu kwa wasap namba 0717396253 na utajihakikishia nafasi ya kupata mafunzo ya kukuza biashara yako. CHUKUA HATUA SASA rafiki yangu.