Rafiki yangu mpendwa,
Hongera sana kwa nafasi hii nyingine nzuri ya leo.
Leo ni siku moya, siku ya kipekee na nafasi nzuri sana kwa kila mmoja wetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UNACHOJIFUNZA NA UNACHOFUNDISHA.
Kuna maswali mawili muhimu sana ya kujiuliza kila siku unapoianza siku yako.
1. Kama ungekuwa huogopi mabadiliko, ungejifunza nini? Maana kila mtu kuna vitu vingi wana anavyoweza kujifunza. Ila wengi wanaogopa kubadilika. Watu wanapenda kufanya kile walichozoea kufanya.

  1. Kama ungekuwa huogopi kukataliwa, unhefundisha nini? Maana kila mtu ana kitu anaweza kuwafundisha wengine, lakini wengi wanaogopa kukataliwa, kupingwa na hata kukosolewa. Hivyo wengi huchagua kukaa kimya ili wasisumbuane na wengine.

Maisha yako ni matokeo ya kile unachojifunza na kile unachofundisha.
Kama hujifunzi vitu vipya na kama huwafundishi wengine, unajizuia kupiga hatua kubwa zaidi kwenye maisha yako.

Kila mtu ana kitu anaweza kujifunza akawa bora zaidi.
Na pia kila mtu ana kitu anaweza kuwafundisha wengine, na akazidi kuwa bora zaidi.
Maana wanasema humaelewa kile ulichojifunza kama bado hujaweza kuwafundisha wengine na wakaelewa.

Jitoe kujifunza kila siku na pia jitoe kufundisha kila siku, kupitia chochote unachofanya.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujifunza na kufundisha.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha