Mpendwa rafiki,
Mambo yanayofanywa na wengi katika jamii yetu ndiyo huwa yanaonekana sahihi hata kama siyo sahihi. Watu wakishaona kila mtu anafanya wanaamini ni sawa kumbe ni mazoea tu, mazoea au ukawaida wa watu kufanya mambo unaweza kuleta athari kubwa sana katika jamii yetu.
Waswahili wanasema wajinga ndiyo waliwao na wanapokusanyika tai wengi ndipo kwenye mizoga. Watu wanaopenda vitu virahisi na kutokupenda kufanya kazi ndiyo maisha yanawapiga sana. Watu ambao maisha kwako ni magumu lakini bado wanajionea huruma wanataka kulala,kuongelea mafanikio bila kazi na kulalamika hovyo.
Njia inayoongoza katika maangamizi ni pana. Mafanikio yanapatikana katika njia nyembamba na siyo kila mtu yuko tayari kupita katika njia nyembamba wakati kuna njia pana. Njia pana inapendwa na wengi lakini ndiyo njia inayoangamiza watu wengi sana kila siku. Wengi wanaangamizwa katika dunia ya sasa, watu wengi wanatapeliwa kwa sababu wengi wanapenda kupitia njia pana ukichagua njia pana tayari umechagua kuangamizwa.
Njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembaba sana,na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba na ni watu wachache tu wanaweza kuigundua njia hiyo.
SOMA;USHAURI; Hatua Za Kuchukua Pale Unaposhindwa Kwenye Kila Unachofanya Kwenye Maisha Yako.
Umechagua kupita njia gani? pana au nyembamba? Kila mtu anachagua kupita njia yake ila njia pana ni njia inayoongoza katika maangamizi, angalia watu wanaopotea ni wale wanaofanya mambo kwa mazoea ambao wengi wanapatikana katika njia hii ya pana. Angalia tu hata katika hali ya kawaida mambo hasi ndiyo yanateka hisia za watu kuliko hata mambo chanya mambo chanya ni njia nyembamba na hasi ni njia pana.
Maisha ni yako na uchaguzi ni wako, ni uhuru wako kuchagua kupita njia gani, ila mimi kama rafiki yako nakusihi usipite njia ya wengi bali pita njia nyembamba ndiyo utafika vizuri kwa sababu haina foleni na watu wengi hawaipendi kuliko njia pana.
Hatua ya kuchukua leo; chagua kupita njia nyembamba kwani ndiyo ina uzima.
Hivyo basi, njia ya kuepuka maangamizi ni kukataa kupita njia pana inayopendwa na wengi.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net
Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti hii hapa www.mtaalamu.net/kessydeo .
Asante sana na karibu sana !