Rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa nimekuwa nakupa taarifa kuhusu tukio kubwa sana la kimafanikio la mwaka huu 2018.

Tukio hilo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, ambayo itafanyika jijini Dar es salaam, jumamosi ya juma hili, tarehe 03/11/2018. Semina hii huwa inafanyika mara moja tu kila mwaka na ni semina inayokuwa imejaa mafunzo na hamasa unazoweza kutumia kwa mwaka mzima kwa mafanikio yako.

Ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii kubwa na ya kipekee, zimebaki siku mbili pekee. Mwisho wa kulipia ili upate nafasi ya kushiriki semina hii ni jumatano ya tarehe 31/10/2018. Hivyo kama hutaki kukosa tukio hili kubwa sana la kimafanikio kwa mwaka 2018 mpaka mwaka 2019 unapaswa kulipa ada yako mapema na kujihakikishia nafasi yako.

semina 2017 3
Kocha Makirita Amani akifundisha kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017

Nafasi za kushiriki semina hii zipo 100 pekee, na zikishajaa nafasi hizo hakuna za ziada.

Baadhi ya vitu adimu kabisa utakavyovipata kwenye semina hii, ambavyo huvipati kwa kujisomea kazi nyingi ninazokuandalia ni hivi;

  1. Kukutana ana kwa ana na mimi kocha wako, ambapo tutajadiliana mengi kuhusu maisha ya mafanikio. Siyo wengi wanapata nafasi hii hivyo ni fursa kubwa sana kwako.
  2. Kukutana na watu wengine wanaoendana na wewe, watu wenye kiu ya mafanikio, wanaotaka kupiga hatua zaidi ili kufanikiwa. Unakumbuka sheria ya watu watano? Kwamba wewe ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka? Sasa unakwenda kuiboresha sheria hii kwa kupata watu watano bora sana kwako.
  3. Kupata mwongozo sahihi wa kuishi maisha ya mafanikio kwa mwaka 2018/2019. Watu wengi hawana mwongozo wanaoufuata kwenye maisha yao, hivyo wanapokutana na changamoto mbalimbali za kila siku, wanakata tamaa na kushindwa.
  4. Kupata jawabu la changamoto mbalimbali zinazokuzuia kufanikiwa kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla.
  5. Kupata nafasi ya kufanya kazi na mimi kocha wako moja kwa moja kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kukuza zaidi biashara yako. Hapa nimetoa nafasi za watu 12, lakini lazima watu hao wahudhurie semina hii, kwa sababu kuna kitu kikubwa tutakifanya baada ya semina. Wapo ambao wamebanwa na kushindwa kuhudhuria semina, ila wanaomba sana nafasi hii, nasikitika kuwataarifu kwamba haitawezekana, wanaweza kupata huduma ya personal coaching kwa kile wanachofanyia kazi.
  6. Utaambukizwa nguvu na hamasa kubwa waliyonayo wengine. Wanasema nguvu na hamasa huwa zinaambukizwa, kuna watu ukikaa nao unajisikia kukata tamaa na kukosa cha kufanya, lakini wapo ambao ukikaa nao unapata hamasa kubwa na msukumo wa kufanya. Kwa kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 utaondoka ukiwa na nguvu na hamasa ya kufanya zaidi.
  7. Utajifunza kutoka kwa washiriki wengine wa semina, changamoto wanazopitia na jinsi wanavyozitatua. Unapokuwa mwenyewe unaweza kuona kama dunia inakuonea hivi, lakini unapokutana na wengine na ukagundua wana changamoto kama zako, unapata faraja ya kuendelea kuweka juhudi kubwa.

Rafiki, yote haya na mengine mengi utayapata siku ya jumamosi tarehe 03/11/2018 kama utakuwa umelipia kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 mpaka kufikia tarehe 31/10/2018.

Ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ni tsh laki moja (100,000/=) ambayo itajumuisha huduma zote muhimu za siku hiyo ya semina, kwa vyakula vya siku nzima, vifaa vya kuandikia na eneo zuri la kujifunzia.

Kupata nafasi ya kushiriki semina hii nzuri sana kwako, tuma malipo, tsh 100,000/= kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo, tuma ujumbe wenye majina yako na namba za simu ili uweze kupata taarifa zaidi kuhusu semina hii.

Rafiki, nakusubiri kwa hamu kubwa siku hiyo ya semina, tuweze kujifunza na kuhamasika kwa pamoja, na kuondoka na mwongozo na mpango tunaofanyia kazi kwa kipindi cha mwaka mzima.

Nina imani hutakosa nafasi hii bora sana na ya kipekee kwako, nafasi ambayo siyo kila mtu anaweza kuipata. Itumie vizuri nafasi hii katika kujijengea msingi imara kabisa wa mafanikio. Karibu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; http://eepurl.com/dDZHvL