Rafiki yangu mpendwa,
Nimekuwa nafanya kazi hii ya kushirikisha maarifa ya maisha na mafanikio kwa zaidi ya miaka mitano sasa. Lakini kadiri siku zinavyokwenda, ndivyo ninaona watu hawana muda, hata ule muda wa kujifunza.
Kwa sasa watu wamezongwa na usumbufu wa kila aina, kuanzia kazi zao, mitandao ya kijamii, habari, na mambo mengine yanayoendelea kwenye jamii.
Kadiri usumbufu unavyozidi kuwa mkubwa, ndivyo watu wengi wanavyokosa nafasi ya kujifunza vitu ambavyo vingeweza kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi.
Usumbufu umekuwa mkubwa sana sasa kiasi kwamba mtu akikutana na makala ndefu, anajiambia nitaisoma baadaye, na hapo inakuwa ndiyo imetoka, baadaye wala hakumbuki tena kama kuna makala alisema ataisoma.
Watu wengi wananunua vitabu lakini hawavisomi mpaka mwisho, wengi huwa wanaanza sura chache za mwanzo na kuishia hapo.
Kwa kifupi hali ya wengi inaelekea kwenye hatari kwa sababu hawajifunzi, na wanazidi kuwa kwenye usumbufu.
Sasa ili kuhakikisha kila rafiki yangu anajifunza, kila mtu anakuwa na hatua bora kabisa ya kupiga kwenye maisha yake, nimekuja na kipengele kipya cha makala ambazo zitatumwa kwa email tu.
Kipengele hiki kipya cha makala kitaitwa DAKIKA MOJA ambapo nitakushirikisha maarifa mafupi ndani ya dakika moja na kukupa hatua ya kuchukua kutokana na maarifa hayo.
Makala hizi zitakuja moja kwa moja kwenye email yako kila siku asubuhi saa 12 kamili.
Hivyo ninachokiomba kwako rafiki yangu ni hiki, kila unapoamka, kabla ya kuianza siku yako, ingia kwenye email yako na tafuta makala ya DAKIKA MOJA nitakayokuwa nimekutumia.
Nakuahidi itakuwa makala fupi, ambayo haitazidi dakika moja kusoma na utaondoka na kitu cha kufanyia kazi kwenye maisha yako kwa siku hiyo, ambacho kitakuwezesha kupiga hatua zaidi.
Ninaweka juhudi kubwa sana kuhakikisha kila ninachokushirikisha kinakuwa bora zaidi, na nina imani makala za DAKIKA MOJA zitaongeza thamani zaidi kwako.
Makala ndefu zitaendelea kuwepo, zipo zitakazotumwa kwa email na nyingine zitaendelea kuwepo kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA. Pia kwenye makala za DAKIKA MOJA nitakuwa nakushirikisha makala mpya ambazo huenda hujazisoma.
Rafiki, niahidi kitu kimoja, kwamba kila siku asubuhi kabla hujaianza siku yako, utaingia kwenye email yako na kusoma makala ya DAKIKA MOJA, ninachoomba kwako ni hicho tu, ujifunze na kuchukua hatua.
Ninachoamini ni kwamba maisha yako yakiwa bora, basi na maisha yangu yatakuwa bora zaidi, ni sheria ya asili ambayo huwa inafanya kazi mara zote na kwa kila mtu.
Karibu sana kwenye makala za DAKIKA MOJA, tujifunze, tuhamasike na tuchukue hatua kila siku ili maisha yetu yaweze kuwa bora zaidi.
MUHIMU; mfumo tunaotumia kutuma email hizi umebadilika, hivyo naomba ubonyeze hapa ili kuboresha taarifa zako.
TAARIFA YA KUBADILIKA KWA MFUMO WA KUPOKEA EMAIL.
Nina taarifa fupi na muhimu sana kwako,
Umekuwa unapokea mafunzo haya ninayotuma kwa njia ya email kwa muda sasa.
Napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha ya kwamba, mfumo wetu wa kutuma email hii umehama na kubadilika.
Mfumo ambao tumekuwa tunautumia haufikishi email kwa wengi na kwa wakati, hivyo wengi wamekuwa wanauliza mara kwa mara mbona hawapati tena email au utaratibu umebadilika.
Email zinatumwa lakini hazifiki kwa wengi.
Hivyo kwa sasa tumebadili mfumo wa kutuma email. Taarifa za wapokeaji wote wa email zimehamishiwa kwenye mfumo mpya, lakini zinaweza zisiwe sawa hasa hapa mwanzoni.
Hivyo ninakuomba ufanye mambo yafuatayo, kama hujapokea email iliyotumwa asubuhi basi bonyeza maandishi haya na ujiunge upya.
Kama umepokea email iliyotumwa asubuhi, bonyeza maandishi haya kuboresha taarifa zako.
Kama email zilizotumwa huzioni, nenda kwenye spam emails na utazikuta huko, mara nyingi email zinapokuja kwa mfumo mpya, huwa zinaonekana kama spam, kitu ambacho siyo sahihi mara nyingi.
Karibu sana tuendelee kuwa pamoja, na tafadhali hakikisha upo kwenye mfumo wa kupokea email kwa sababu tunaanza kipengele kipya na muhimu sana cha DAKIKA MOJA, hizi ni makala za kila siku, za kujifunza, kuhamasika na kuchukua hatua.
Ili usikose kipengele hiki, fuata maelekezo niliyotoa hapo juu, muhimu zaidi ni uweze kupata na kufungua email zako kila siku.
Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.
Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.
Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.
Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)
Kupata huduma nyingine za ukocha tembelea www.amkamtanzania.com/kocha
Kupata vitabu vizuri vya kusoma tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu