Mpendwa rafiki yangu,

Kama tunavyojua fedha ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Hakuna ambaye anaweza akamaliza siku yake bila kutumia fedha kwa namna yoyote ile. Na matumizi yote tunayofanya ndani siku siyo kila mtu anayenunua hilo hitaji ni muhimu sana kiasi kwamba akikosa maisha yake hayawezi kwenda kama kawaida.

Kimsingi, tuna aina mbili za matumizi ambayo ni matumizi ya lazima na matumizi ambayo siyo ya lazima. Kuna matumizi ambayo hata usiponunua kitu hiko maisha yako hayatoathirika na kitu chochote badala yake kitaenda vizuri hata ukikosa. Kwa mfano, maisha yako hayawezi kusimama kama ukikosa kuangalia tv hivyo usiponunua king’amuzi bado maisha yako yataendelea kama kawaida.  Lakini huwezi kusimama mbele za watu na kusema kununua king’amuzi ni kitu muhimu, ukikosa kuangalia labda utakufa.

Kabla ya kununua unatakiwa kuchuja kwanza matumizi yako muhimu. Je kile unachokwenda kununua ni muhimu kiasi kwamba ukikosa utakufa? Je kinaweza kusubiri? Kama kinaweza kusubiri basi hilo siyo hitaji lazima. Manunuzi mengi tunayofanya katika maisha yetu mengi yanaweza kusubiri kwa asilimi kubwa tu lakini watu wengi wanashindwa kujinyima na kujitesa. Watu wamekuwa kama watoto wadogo wanataka kile wanachokitaka papo kwa papo.

Nini kinasababisha wewe kuwa na matumizi makubwa? Asilimia kubwa ya watu wanaonunua wananunua kwa hisia. Wengi wanaongozwa na hisia katika kununua vitu. Unakuta hata mtu hajapanga kununua hitaji fulani akikutana nalo njiani utashangaa anashawishika na kununua huku akishawishika atakuja kukikosa tena siku nyingine.

FEDHA KWA BLOG

Kama kitu hakipo katika bajeti yako maana yake hiko siyo muhimu ndiyo maana hukukipangilia katika bajeti yako. watu wanaongozwa na hisia katika kufanya manunuzi na mwisho wa siku wanajikuta matumizi yamekuwa makubwa kuliko hata kipato chao.

Kuna kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato kinapoongezeka, hivyo usipokuwa makini ni sawa sawa na kujaza maji katika ndoo iliyotoboka huku ukisubiria ijaye. Kipato kinapoongezeka endelea kutawala matumizi yako kila wakati bila kufanya utashindwa kupiga hatua mbele. Ulivyokuwa una kipato kidogo ulikuwa na matumizi madogo lakini pale tu kipato kitakapoongezeka utashangaa na matumizi nayo yanaongezeka mara dufu.

Tawala sana hisia zako, usikubali kununua kwa hisia hata kama kuna kitu unakipenda basi jipe angalau muda ukifikirie na muda mzuri ni siku ni 28 utashangaa mwenyewe hata hizo siku 28 hazijafika utakuja kuona hilo jambo siyo muhimu kama ulivyokuwa unafikiria hapo awali.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kuzuia Upotevu Wa Fedha Kwenye Biashara Yako Na Kuweza Kuiona Faida.

Usinunue kwa sifa, kuwaonesha watu kuwa wewe unajua kununua hapana, nunua kama kweli ni muhimu na ongozwa na akili. Iko hivi rafiki, watu wananunua kwa hisia na wanakuja kufikiria baadaye kwa kutumia akili kile walichonunua ni sahihi au siyo sahihi.

Hatua ya kuchukua leo; usiongozwe na hisia katika kufanya manunuzi bali ongozwa na akili. Kitu kama siyo muhimu kwako usinunue kisubirishe kwanza. Tawala matumizi yako vizuri ili uweze kufanya mambo muhimu ya kungeza kipato chako.

Kwahiyo, hata uwe mtafutaji au mkusanyaji mzuri wa fedha, kama utashindwa kutawala eneo la matumizi bado utakuwa hujajikomboa katika safari ya mafanikio. Kumbuka kununua matumizi muhimu ambayo ukiyakosa basi utakufa lakini kama hufi kinaweza kusubiri na tumia akili na siyo kuongozwa na hisia.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana!