Habari rafiki yangu mpendwa,
Kila mwisho wa mwaka nimekuwa na utaratibu wa kujipa likizo ya siku saba. Likizo hii imekuwa inaniweka mbali kabisa na mitandao na mawasiliano mengine ya kawaida na kunipa muda zaidi wa kusoma kwa kina, kuweka mikakati mbalimbali ya kukuza na kuboresha zaidi huduma ninazotoa.
Kwa zaidi ya miaka mitano sasa nimekuwa nafanya zoezi hili na limekuwa na manufaa makubwa sana kwangu na kwa huduma ninazotoa. Huduma zote mpya ambazo nimewahi kuja nazo na zikawasaidia sana, nilizipata kwenye likizo hizi ambazo ninapata muda wa kufikiri na kutafakari kwa kina.
Kwa mwaka huu 2018 likizo yangu fupi itaanza ijumaa ya tarehe 21/12/2018 na kumalizika alhamisi ya tarehe 27/12/2018. Hizi zitakuwa siku saba ambazo sitapatikana kabisa kwenye mtandao wa intaneti na pia mawasiliano ya kawaida ya simu yatakuwa kwa kiwango cha chini sana.
Pia makala zote ambazo zimekuwa zinaenda hewani kila siku kwenye AMKA MTANZANIA, KISIMA CHA MAARIFA na kwenye email, hazitakuwepo ila tu makala za KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO kwenye KISIMA CHA MAARIFA ndiyo zitaendelea kuwa hewani. Makala hizi za kurasa nimejiahidi kuziandika kila siku mpaka siku nitakayoondoka hapa duniani, na ninaandika kwa siku husika.
Hivyo kitu pekee nitakachofanya wakati wa likizo hii fupi kwenye uandishi ni kuandika makala ya siku na kisha msaidizi wangu atahakikisha inakwenda hewani siku husika.
Kwenye likizo hii fupi huwa napata muda wa kusoma kwa undani zaidi, kutafakari na kuweka mipango mikubwa ambayo nakwenda kuifanyia kazi kuboresha zaidi huduma ninazotoa.
Kwenye likizo ya mwaka huu, nitazama zaidi kwenye kazi za mwandishi mmoja. Na huu ndiyo utaratibu ambao nitaenda nao kila mwaka. Kila mwaka nitachangua mwandishi mmoja ambaye nitazama ndani zaidi kwenye kazi zake zote. Unaposoma kazi zote za mwandishi mmoja, unapata uelewa mpana sana wa kile anachotoa na pia unaelewa namna anavyofikiri kwenye mafunzo anayotoa.
Mwandishi ambaye nitazama ndani zaidi kwenye kazi zake kwenye likizo hii ya mwaka 2018 atakuwa ni James Allen. Huyu ni mwandishi ambaye ameandika sana kuhusu nguvu ya akili na kufikiri. Kitabu chake maarufu sana ni AS A MAN THINKETH. Kitabu ambacho kimeeleza nguvu kubwa ambayo ipo kwenye akili na fikra zetu. Kwama kama tutadhibiti fikra zetu, zinaweza kutupatia chochote tunachotaka.
Kipo kitabu ambacho kina mkusanyiko wa vitabu vyote 19 ambavyo James Allen aliandika. Kitabu hicho kinaitwa MIND IS THE MASTER. Hivyo naweza kusema kusudi kuu la likizo yangu fupi ya mwaka huu ni KUTAWALA FIKRA ZANGU, kwa sababu nikiweza kuzitawala vizuri nitaweza kufanya makubwa zaidi.
MAMBO YA WEWE KUFANYA WAKATI MIMI NIPO LIKIZO.
Rafiki, kwa siku saba ambazo nitakuwa likizo, nashauri ufanye mambo yafuatayo;
- Kwa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA ambao ada zao zimefikia ukomo kamilisha malipo ya ada yako mapema ili tuendelee kuwa pamoja kwa mwaka 2019.
- Kwa wale ambao bado hawajawa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, hakikisha kabla mwaka 2019 haujaanza unakuwa umejiunga kwa sababu mambo bora zaidi yataendelea kupatikana kupitia KISIMA CHA MAARIFA.
- SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI itaanza januari 03 lakini mwisho wa kulipia ili kuweza kushiriki ni januari 02. Nashauri mtu ulipie mapema ili usikose semina hii ya kipekee kabisa kwako. Kushiriki semina hii unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na kama siyo mwanachama basi unalipa ada ya tsh 20,000/= kwa namba 0717396253 au 0755953887.
- Kwa wale ambao siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, nimeandaa kundi maalumu la wasap kwa ajili ya semina ya TABIA ZA KITAJIRI, kama bado hujajiunga fungua hapa kujiunga; https://chat.whatsapp.com/JvJBnoKixGrJZpZdw3shRv (kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hili).
- Endelea kutembelea amkamtanzania.com na www.kisimachamaarifa.co.tz kila siku kusoma makala za nyuma. Zipo makala nyingi sana za nyuma ambazo unaweza kujifunza mengi.
- Pia endelea kusoma vitabu mbalimbali, na soma kujifunza siyo kusoma kujifurahisha au kusoma kumaliza.
- Tenga siku moja kabla mwaka huu haujaisha na ifanye kuwa siku yako, siku ambayo hutakuwa na usumbufu wowote na pitia maisha yako yote, unakotoka, ulipo na unapokwenda. Pitia kila unachofanya na ona kina mchango gani kufika kule unakotaka kufika. Zoezi hili litakupa mwanga mkubwa sana kuhusu maisha yako. Kwa sababu kuna mengi unaweza kuwa unafanya ambayo hayana mchango wowote kwako.
Nikutakie kila la kheri na wakati mwema sana kwako rafiki yangu kwa kipindi ambacho nitakuwa likizo. Nikutakie sikukuu njema, usherekee kwa amani na utulivu na usiyasahau malengo yako makubwa. Kama ambavyo nimekuwa nakuahidi, tutaendelea kuwa pamoja kwenye huduma hii ya uandishi na ukocha kwa kipindi chote cha maisha yangu. Kila ninachofanya ni kwa ajili yako wewe rafiki yangu.
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha
Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge