Habari rafiki yangu mpendwa,

Napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee sana kukufikishia salamu za likizo yangu niliyokuwa nayo tangu tarehe 21/12/2018 mpaka tarehe 27/12/2018.

Imekuwa ni likizo bora sana kwangu na mengi niliyopanga kufanya nimefanikiwa kuyakamilisha, isipokuwa kwa machache ambayo muda haukuweza kutosha kuyatekeleza.

Likizo hii imekuwa ni siku saba za kupata nafasi ya kuwa na mimi binafsi na pia kupata nafasi ya kuwa na wale wa karibu zaidi kwangu.

Pia imekuwa ni nafasi ya mimi kuweza kutafakari zaidi huduma zote ninazozitoa na njia bora zaidi za kuboresha huduma hizi.

Nikukumbushe ya kwamba kila ninachofanya, nakazana kutoa thamani kubwa sana ya matumizi kuliko ninavyopokea kwenye thamani ya fedha. Hii ni siri kubwa sana niliyojifunza kwenye kitabu cha THE SCIENCE OF GETTING RICH, kwamba kwa chochote unachofanya, basi toa thamani kubwa sana ya matumizi kwa wale unaowafanyia kuliko thamani ya fedha unayochukua. Kwa kufanya hivi, kunawavutia watu wengi zaidi kuja kwako, kwa sababu hakuna asiyependa kupata thamani zaidi.

FEDHA KWA BLOG

Nachukua nafasi hii kukukaribisha tena tuendelee kuwa pamoja, kwenye mwaka wetu huu wa mafanikio 2018/2019, na kama ambavyo nimewahi kukuahidi, tutaendelea kuwa pamoja kila siku kwenye huduma hii ya uandishi na ukocha ninayoitoa kwa ajili yako.

Katika likizo hii nimekuja na mengi zaidi ya kuboresha huduma zote ninazotoa na nitaendelea kukushirikisha kadiri tunavyoendelea kwenda pamoja.

Mambo matatu muhimu sana ambayo napenda kukukumbusha uyafanyie kazi;

  1. JIUNGE NA KISIMA CHA MAARIFA.

Rafiki, kama umekuwa pamoja na mimi kupitia mafunzo haya kwa muda sasa lakini bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, basi nakusihi sana kitu muhimu kwako unachopaswa kukifanya sasa ni kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kuwa ndani ya KISIMA, tutakuwa pamoja, tutajifunza mengi zaidi na pia utapata nafasi ya karibu ya kuwasiliana na Kocha Makirita na hata ushauri wa moja kwa moja.

Ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ni tsh 100,000/= (laki moja) ambayo inakuwa ni ada ya mwaka mzima. Ukilipa leo ada inakwenda kwa kipindi cha mwaka mzima. Kwa mwaka mzima utapata nafasi ya kushiriki mafunzo ya kila siku, madarasa ya kila wiki na hata semina mbili kubwa ninazoendesha kwa njia ya mtandao kwa mwaka mzima. Yote hayo utapata nafasi ya kushiriki bila ya kulipa ada ya ziada.

Namba za kufanya malipo ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ni mpesa 0755 953 887 au tigo pesa/ airtel money 0717 396 253. Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kwa njia ya wasap namba 0717396253.

  1. LIPA ADA YAKO YA KISIMA CHA MAARIFA KWA WAKATI.

Rafiki, kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi nakukumbusha kulipa ada yako kwa wakati. Pale unapopewa taarifa ya ada yako kumaliza wakati wake, basi fanya malipo mapema ili tuweze kuendelea kuwa pamoja kwa mwaka mwingine.

Kama mafunzo ambayo umekuwa unayapata kwa mwaka mzima yamekuwa na msaada kwako, basi kamilisha ada yako tuendelee kuwa pamoja. Lakini kama mafunzo hayakuwa na msaada kwako, yaani kama hakuna chochote kilichobadilika kwenye fikra zako, tabia zako na hata maisha yako kwa mwaka mzima ambao umekuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, basi usilipe tena ada. Kusudi kuu la KISIMA CHA MAARIFA ni kuwe na mabadiliko kwenye maisha ya kila anayekuwa ndani yake. Na kama kweli utafanyia kazi yale unayojifunza kila siku, lazima maisha yako yatabadilika sana.

  1. KARIBU KWENYE SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI.

Rafiki, nimekuandalia semina kubwa na ya kipekee sana kwa kuanzia mwaka 2019. Ni semina inayokwenda kwa jina la TABIA ZA KITAJIRI. Kwenye semina hii, tunakwenda kujifunza tabia kumi ambazo mtu ukiziishi kila siku, hakuna chochote kinachoweza kukuzuia usiwe tajiri kwenye maisha yako.

Kwenye semina hii, unakwenda kujifunza kwa vitendo na mifano, vitu gani ufanye na vipi uache kufanya ili uweze kufikia utajiri na mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Hii ni semina ambayo unakwenda kuondoka na kanuni ya kuyaishi maisha ambayo yatakuwa na mafanikio makubwa sana kwako. Huwa wanasema maisha hayana kanuni, lakini huo ni uongo mtupu, maisha yana kanuni  na wote wanaofanikiwa wanajua na kufuata kanuni ya maisha ya mafanikio.

Semina ya TABIA ZA KITAJIRI itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki semina hii ukiwa popote duniani. Huhitaji kusafiri au kuacha shughuli zako za kila siku ili kushiriki semina hii. Unachohitaji kufanya ni kutenga nusu saa kwa siku ya kufuatilia masomo ya semina hii.

Semina itaanza tarehe 03/01/2019 na kumalizika tarehe 13/01/2019. Kila siku utajifunza tabia moja na jinsi ya kuijenga na kuiishi kwenye maisha yako. Kwa siku hizi kumi za semina utaondoka na mpango mkakati wa kuyaishi maisha ya mafanikio makubwa kwako.

Ili kushiriki semina hii unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, hivyo kama bado hujawa mwanachama fuata maelekezo niliyotoa kwenye namba moja hapo juu.

Lakini pia ipo nafasi ya upendeleo ya kuweza kushiriki semina hii hata kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na kwa sababu yoyote ile huwezi kujiunga sasa, basi nimekuandalia kundi maalumu la semina. Ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki semina kwa kundi hili, unapaswa kulipa ada ya kushiriki semina ambayo ni tsh 20,000/= (elfu ishirini).

Namba za kufanya malipo ya tsh 20,000/= ili kupata nafasi ya kushiriki SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI ni mpesa 0755 953 887 au tigo pesa/ airtel money 0717 396 253. Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kwa njia ya wasap namba 0717396253.

Mwisho wa kulipa ada ya kushiriki semina ni tarehe 02/01/2019. Lakini kama nilivyokuambia, nafasi hii ni ya upendeleo, hivyo anayewahi ndiye anayepata nafasi. Kama nafasi zitajaa kamba ya tarehe hiyo basi utakuwa umekosa nafasi ya kushiriki semina hii muhimu sana, kitu ambacho hupaswi kukiruhusu kitokee kabisa.

Rafiki, nikukaribishe tena sana na sana tuendelee kuwa pamoja kupitia huduma hii ya uandishi na ukocha, nina mengi sana ninayoendelea kujifunza ambayo najua nikikushirikisha maisha yako hayataendelea kubaki pale ulipo sasa.

Kwa siku hizi saba za likizo nimekukosa sana na hii imenifanya nione umuhimu wa mimi kuwasiliana na wewe kila siku kupitia huduma mbalimbali ninazotoa.

Karibu pia unishirikishe siku hizi saba za kutokusikia kutoka kwangu moja kwa moja kila siku kama ulivyozoea zimekwendaje kwa upande wako.

Karibu tena rafiki yangu tuendelee kuwa pamoja.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha