Rafiki yangu mpendwa,

Tumefika juma la mwisho kabisa la mwaka huu 2018, juma namba 52.

Ni jambo kubwa na la kushukuru sana kwa sababu kuna wengi walioweka mipango mingi na mizuri kwa mwaka huu 2018, lakini sasa hatupo nao tena.

Hivyo hata kama uliweka malengo makubwa na hujaweza kuyafikia, kwanza shukuru kwa kuendelea kuwa hai, kisha tafakari wapi ulipokwama na njoo na mkakati wa kuhakikisha mwaka 2019 hutakwama tena.

Katika juma hili la mwisho la mwaka huu 2018 nimekuandalia tano za juma ambazo zimebeba mjumuisho mkubwa wa mwaka 2018 na namna bora ya kwenda kuuanza mwaka 2019 ili uwe wa mafanikio makubwa sana kwako.

Rafiki, jipe muda wa kusoma kwa kina TANO HIZI ZA JUMA, jifunze na chukua hatua na kwa hakika maisha yako hayatabaki hapo yalipo.

new-year-2019-

Karibu sana kwenye nondo hizi tano za kuufunga mwaka 2018 na kwenda kuufungua mwaka 2019.

#1 VITABU NILIVYOSOMA; VITABU 45 NILIVYOKUSHIRIKISHA KWENYE TANO ZA JUMA NA KITU KIMOJA CHA KUFANYIA KAZI KWENYE KILA KITABU.

Rafiki yangu mpendwa, mwaka huu 2018 nimefanikiwa kusoma vitabu vingi sana. Na kwenye tano za juma nilikuwa nakushirikisha moja ya vitabu nilivyosoma kila juma.

Hapa nakwenda kukushirikisha kila kitabu nilichokuwekea kwenye tano za juma na kitu kimoja cha kufanyia kazi.

Ieleweke kwamba hivi siyo vitabu nilivyosoma 2018, bali ni vitabu nilivyokushirikisha kwenye tano za juma pekee, vipo vingine vingi nilivyokushirikisha kwenye chambuzi za vitabu na vingine ambavyo sikukushirikisha kabisa.

Karibu kwa vitabu hivi na yale ya kujifunza;

Juma #3; 33 STRATEGIES OF WAR; maisha ni vita na wale wenye mbinu sahihi ndiyo wanaishinda vita hii.

Juma #4; THE CHINA STRATEGY; nchi ya China imeweza kuondoka kwenye nchi masikini na kwenda nchi tajiri ndani ya muda mfupi kwa kufungua mipaka yake na kuruhusu soko huria.

Juma #5; THE SECRET OF SUCCESS; hakuna siri ya mafanikio, msingi mkuu wa mafanikio upo kwenye utu wako.

Juma #6; The craving mind; usipoweza kuidhibiti akili yako, itakufanya wewe uwe mtumwa wa tabia zisizo na manufaa kwako.

Juma #7; THE PATH OF PROSPERITY; njia ya kuelekea utajiri na mafanikio makubwa inaanzia ndani yako, huhitaji cha ziada kwa hapo ulipo sasa, unahitaji kuanza kutumia kila kilicho ndani yako.

Juma #8; EVOLUTIONARY ENLIGHTMENT; dini ni kikwazo kwenye ukuaji wa kiroho, wengi wanashikilia dini kuliko kukazana kukua kiroho na kiimani.

Juma #9; PREDICTABLY IRRATIONAL; hisia zetu huwa zinaathiri maamuzi yetu, ukitaka kufanya maamuzi sahihi, fanya wakati ukiwa huna hisia kali.

Juma #10; WHEN BREATH BECOMES AIR; maisha ni kuishi sasa na kifo ni uhakika.

Juma #11; TWO AWESOME HOURS; masaa mawili ya kwanza kwenye kila siku yako yafanye kuwa muda wako, usiruhusu yeyote ayaingilie, huu ndiyo muda unaoweza kuutumia kuwa bora zaidi na kusonga mbele zaidi.

Juma #12; HOW YOUR CHILD LEARN BEST; watoto hawafanani na hata kujifunza kwao kunatofautiana, mtoto ambaye hafanyi vizuri darasani, haimaanishi hatafanya vizuri kwenye maisha, njia yake ya kujifunza ni tofauti na ya darasani.

Juma #13; AN HOUR TO LIVE, AN HOUR TO LOVE; upendo ndiyo nguvu inayoweza kujenga mahusiano bora, hakikisha unapata muda wa kuwa na wale ambao ni muhimu kwako.

Juma #14; MAN; KING OF MIND, BODY AND CIRCUMSTANCE; wewe ni mfalme wa akili yako, mwili wako na mazingira yako, kila kinachotokea kwenye maisha yako kinaanzia kwenye akili yako. ukiweza kudhibiti akili yako utaweza kuyadhibiti maisha yako.

Juma #15; THE HEALING POWER OF MIND; tahajudi (meditation) ni zoezi rahisi ambalo linakuwezesha kuwa na afya imara ya akili na hata ya mwili.

Juma #16; FACTFULLNESS; mambo mengi tunayoyajua kuhusu dunia siyo sahihi, vyombo vya habari vimekuwa vinakuza mabaya machache kuhusu dunia, lakini ukweli ni kwamba dunia inapiga hatua na kuwa bora zaidi kila siku.

Juma #17; SKIN IN THE GAME; Chochote unachofanya kwenye maisha yako, kazi, biashara, mahusiano, imani na mengineyo, unahitaji kuwekeza kila ulichonacho kiasi kwamba ukifanya makosa unapoteza kila kitu. Na kama upo kwenye mahusiano au ushirikiano ambapo mwingine ananufaika na faida ila hasara haimgusi, ondoka haraka.

Juma #18; PERENNIAL SELLER; chochote unachofanya, usifikirie leo, kesho au mwaka ujao, bali fikiria miaka 100 ijayo. Kwa kufikiria miaka mingi utaifanya kazi ambayo ni bora zaidi.

Juma #19; 12 RULES FOR LIFE; ukizijua kanuni za maisha na kuzifuata utaepuka machafuko kwenye maisha yako na kuwa na maisha yenye mpangilio mzuri. Tunaingia kwenye matatizo mbalimbali kwa sababu hatuzijui au hatuzifuati kanuni za maisha.

Juma #20; OWN THE DAY, OWN YOUR LIFE; jinsi unavyoiishi siku yako moja ndivyo unavyoyaishi maisha yako yote. Kama unataka kuyadhibiti maisha yako na kuwa na maisha ya mafanikio, anza kwa kudhibiti kila siku yako, tangu unapoamka mpaka unapolala.

Juma #21; SELLING YOU; maisha ni kuuza na wale wanaoweza kuuza vizuri, kwa kuanzia na kujiuza wao wenyewe, kuuza bidhaa au huduma zao, ndiyo wanaofanikiwa sana. jifunze kuuza na hutakuwa na maisha magumu.

Juma #22; THE GREATEST EMPIRE; ufalme ulio mkuu ni kuwa mfalme wako mwenyewe (the greatest empire is to be emperor of oneself). Ukiweza kujitawala mwenyewe, ukajiongoza mwenyewe, basi dunia nzima itakuwa chini yako, na siyo kwa ubaya, bali kwa wema.

Juma #23; THE MILLIONAIRE’S SECRETS; LIFE LESSONS IN WISDOM AND WEALTH; Mara zote ishi kwa kanuni kuu; wafanyie wengine kile ambacho ungependa wakufanyie. Na ili ufanikiwe zaidi, piga hatua kwenye kanuni hiyo; usifanye chochote kwa ajili yako, fanya kila kitu kwa ajili ya wengine.

Juma #24; THE 22 IMMUTABLE LAWS OF MARKETING; Sheria ya 18; sheria ya mafanikio.

Mafanikio huwa yanaleta kiburi na kiburi huwa kinaleta kushindwa. Watu wanapofanikiwa huwa wanajiona wameshajua kila kitu, wanaacha kuweka juhudi walizoweka mwanzo na wanaanza kushindwa.

Haijalishi umefanikiwa kiasi gani, epuka sana kuwa na kiburi, epuka kujiona umeshajua kila siku, na kila wakati endelea kujifunza na kuchukua hatua kama vile ndiyo unaanza.

Juma #25; HOW TO SELL ANYTHING TO ANYBODY; Kuna vitu viwili muhimu sana unapaswa kuvipata kwenye mauzo, cha kwanza unapaswa kupata fedha, na cha pili unapaswa kupata urafiki. Sasa watu wengi huangalia cha kwanza, kupata fedha pekee na hivyo huwa tayari kufanya chochote wauze. Ila kama utamuuzia mtu kitu ambacho hakimfai, jua siyo tu umempoteza mteja huyo, bali umepoteza wateja wengine wengi. Unahitaji kutengeneza urafiki na kila mteja wako, kwa kujali hasa hitaji lake na kuhakikisha anarudi kununua kwako na anawaambia wengine kuhusu unachofanya. kama utapata fedha na ukakosa urafiki, hutadumu kwenye biashara kwa muda mrefu.

Juma #26; MARKETING THAT MATTERS; Usiogope kuitangaza biashara yako. Masoko ndiyo msingi muhimu wa biashara yoyote ile. Kikwazo namba moja kwenye biashara yako ni wateja kutokujua kuhusu uwepo wako. Hivyo unahitaji kuitangaza biashara yako na kuhakikisha kila mteja inayemfaa anajua uwepo wa biashara hiyo. Na unapotangaza, eleza kile ambacho biashara yako inafanya, yaani wateja wananufaikaje na biashara hiyo. Ili ufanikiwe kwenye biashara, lazima uwe na mkakati mzuri wa kutangaza na kufikia soko la biashara yako.

Juma #27; SELL OR BE SOLD; Mauzo ndiyo njia ya maisha, mauzo ni hitaji muhimu la maisha, ili ule lazima uuze, na lazima pia watu wakuuzie kitu. Kama kuna kitu kimoja unapaswa kujifunza sana kwenye maisha yako, ni jinsi gani unaweza kuuza vizuri chochote unachouza. Kama umeajiriwa unauza muda wako na ujuzi wako pia. Kama upo kwenye biashara unauza bidhaa na huduma ulizonazo. Maisha yanaendeshwa kwa kamisheni ambazo tunazipata kwenye mauzo yetu, inategemea tu jina gani unaita, kwenye biashara utasema ni faida, kwenye kazi mshahara, kwenye mauzo ni kamisheni. Tambua, hakuna kitakachotokea kwenye maisha yako mpaka umuuzie mtu kitu. Amka sasa na anza kuuza kile unachouza kwa kuwa maisha yako yanategemea wewe kuuza.

Juma #28; THE WISDOM OF LIFE; Msaada wa nje hauwezi kumsaidia mtu yeyote ambaye ameshajiwekea ukomo ndani yake. Huwezi kujikimbia wewe mwenyewe, kama ambavyo mtu hawezi kuondoka ndani ya ngozi yake. Mabadiliko ya kweli kwenye maisha ya mtu, lazima yaanzie kwenye utu wake, lazima awe tayari kubadilika yeye mwenyewe. Ukomo wa mtu kwenye maisha, ni ule ambao amejiwekea wewe mwenyewe. Hebu jiangalie ni vitu hani umewahi kukosa kwenye maisha yako na ona kama hakuna ukomo umekuwa unajiwekea wewe mwenyewe.

Juma #29; THE POWER OF RELENTLESS; bila ya kuwa mbishi hutaweza kufanikiwa kwenye haya maisha, unapaswa kuwa mbishi na mgumu ili kufanikiwa. Kwenye safari ya mafanikio utakutana na kikwazo cha kila aina, ubishi wako ndiyo utakaokuwezesha kuvuka vikwazo hivi na kupata kile unachotaka.

Juma #30; SPIRITUAL SOLUTIONS; ANSWERS TO LIFE’S GREATEST CHALLENGES; kila changamoto tunayokutana nayo kwenye maisha, suluhisho lake linaanzia ndani yetu, na linaanzia kwenye imani yetu. Unapoangalia kila kitu kwenye maisha yako, kama ukiwa muwazi kabisa, kama utaondoa kutafuta sababu, utaona jinsi ambavyo wewe mwenyewe umechangia kwenye tatizo uliloingia na suluhisho lake linaanzia ndani yako.

Juma #31; BLUR; HOW TO KNOW WHAT’S TRUE IN THE AGE OF INFORMATION OVERLOAD; tunaishi kwenye zama za mapinduzi ya taarifa, hakuna tena mwenye uwezo wa kumiliki taarifa au kuzuia watu wasipate taarifa fulani. Kwa sababu kila mtu anayo nguvu ya kusambaza na kupokea taarifa yoyote. Japo hili linakuwa faida kwa walaji wa taarifa, lakini pia linakuja na hatari moja, ni vigumu sana kujua usahihi wa taarifa unazopata hasa kwenye mtandao. Watu wengi wamefanya maamuzi kwa taarifa zisizo sahihi kitu ambacho kimewagharimu sana.

Juma #32; MINDFULNESS IN PLAIN ENGLISH; Tahajudi inatusaidia kuweza kudhibiti akili na mawazo yetu, kuweza kuweka umakini kwenye chochote tunachofanya na kuacha kuendeshwa kwa hisia na matukio na badala yake kuwa na utulivu kwenye chochote ambacho mtu umechagua kufanya.

Juma #33; YOUR FIRST 100 MILLION; Mafanikio makubwa siyo kwa watu laini laini. Dunia ya sasa watu wamekuwa laini sana. Wanataka mafanikio makubwa na wakati huo huo wanataka wamfurahishe kila mtu kwenye maisha. Hicho ni kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa namna yoyote ile. Kwenye mafanikio makubwa hakuna urafiki, na kama unatafuta rafiki nunua mbwa, maana hao ndiyo rafiki wazuri, wengine mtasumbuana sana inapokuja kwenye mafanikio makubwa.

Juma #34; MASTERY: KEYS TO SUCCESS AND LONG-TERM FULFILLMENT; ili uweze kufikia mafanikio makubwa na ya kudumu kwenye maisha yako, unapaswa kuwa na ubobezi kwenye eneo fulani. Na ili kufikia ubobezi unahitaji vitu viwili, muda na kuweka kazi.

Juma #35; REWORK; Usijifunze kutokana na makosa yako, badala yake jifunze kutokana na mafanikio yako. tumezoea kuambiwa jifunze kutokana na makosa, lakini hilo halisaidii sana. jifunze kutokana na mafanikio yako, hata kama ni madogo sana, utajua njia sahihi ya kufanya ili ufanikiwe tena.

Juma #36; THE PERFECT DAY FORMULA; Kanuni ya siku ya mafanikio imejengwa kwenye misingi mikuu mitatu; moja, KUDHIBITI yale yaliyo ndani ya uwezo wako na kupokea yale ambayo huwezi kuyadhibiti. Ili kuwa na siku ya mafanikio, unahitaji kuwa na udhibiti mkubwa kwenye ASUBUHI YAKO.

Msingi wa pili ni KUSHINDA kelele na usumbufu wa kila siku ili kuweza kufanya yale muhimu. Ili kuwa na siku ya mafanikio, unahitaji kushinda kelele na usumbufu kwenye MCHANA WAKO.

Msingi wa tatu ni UMAKINI. Hapa unahitaji kuweka umakini kwenye yale ya muhimu zaidi kwako na kupuuza mengine ambayo siyo muhimu. Ili kuwa na siku ya mafanikio, unahitaji kuweka umakini kwenye yale yaliyo muhimu sana kwenye JIONI YAKO.

Juma #37; BUYING CUSTOMERS; ili biashara yako iweze kukua lazima uwekeze fedha kwenye kupata wateja wa biashara hiyo. bila ya kuwekeza fedha kupata wateja, biashara yako haitajulikana na hili litapelekea biashara hiyo kufa.

Juma #38; HOW TO RUN A COUNTRY; ili kuwa kiongozi mzuri, unapaswa kufuata sheria za asili. Sehemu ya sheria hizo za asili ni kwamba watu wote ni sawa, kila mtu anastahili kupata haki, kila mtu ana uhuru wa kuishi na kufanya maamuzi yake, na pia kila mtu anayo haki ya kuwa na furaha kwenye maisha yake. Kama kiongozi, lazima uhakikishe watu wako wana uhuru huo wa maisha, tofauti na hapo uongozi utakuwa mgumu.

Juma #39; THIS IS GOING TO HURT; SECRET DIARIES OF A JUNIOUR DOCTOR; Kuchagua kazi yoyote ila kwa kigezo cha kipato ni kujiandaa kuumia, kwa sababu kazi nyingi hazitakupa kipato kinachoendana na juhudi unazopaswa kuweka kwenye kazi hiyo. Hivyo kitu cha kwanza unachopaswa kutumia kufanya maamuzi ya kazi ni mapenzi na kujali. Ikiwa unafanya kile unachopenda, na unakijali kwa sababu kina maana kwako, hata kama hutapata fedha nyingi kwa haraka, utakuwa na maisha bora na baadaye kipato chako kitakuwa kizuri.

Juma #40; JUMA LA USTOA; Ustoa ni falsafa ya matendo, ni falsafa ambayo imelenga kumwezesha mtu kuwa na maisha bora, kwa kufikiri sahihi na kuchukua hatua sahihi kwenye maisha yake. Falsafa ya ustoa siyo kama falsafa nyingine za kubishana na kutaka kuonekana unajua zaidi, badala yake ni falsafa ya kufikiri sahihi na kuchukua hatua sahihi. Falsafa ya ustoa inalenga kudhibiti hisia zetu na kuishi kulingana na asili. Kwa njia hiyo, tunakuwa na maisha bora wakati wote.

Juma #41; GO-GIVER; Zipo kanuni kuu tano za kukuwezesha kupata mafanikio makubwa sana, kutoa thamani kubwa, kuwahudumia wengi zaidi, kuweka mbele maslahi ya wengine, kuishi maisha ya uhalisia wako na kuwa tayari kupokea.

Juma #42; THE ART OF GOOD LIFE; Inapokuja upande wa fedha, kuwa na kiasi cha fedha kitakachokuwezesha kuendesha maisha yako bila ya kutegemea kipato cha moja kwa moja, usijilinganishe na yeyote kifedha na hata kama una fedha nyingi kiasi gani, ishi maisha ya kawaida, utajiri hujenga wivu.

Juma #43; CHARLIE MUNGER; THE COMPLETE INVESTOR; Charlie Munger ni mmoja wa watu ambao wamejenga msingi wao wameujenga kwenye maarifa na hekima. Munger anaamini sana katika kujifunza, siyo tu kwenye lile eneo ambalo mtu unafanyia kazi, bali kwenye maeneo mengine pia.

Munger ana mfumo wake anaouita MENTAL MODELS, ambapo anasema ili kuweza kufanya maamuzi sahihi, lazima uweze kufikiri kwa mifumo mbalimbali. Lazima uweze kutumia mifumo tofauti na kile unachofanyia kazi. Kwa mfano kwenye uwekezaji, lazima uweze kufikiria kama mwanahisabati, mwanafizikia, mwanasaikolojia, mwanahistoria, mwanabaiolojia na mwanafalsafa.

Juma #44; SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018; Kwenye juma la 44 tulifanikiwa kufanya semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 ambayo ilifanyika kwa mafanikio makubwa sana. Kama ulikosa semina hii basi ulikosa mengi, anza kujiandaa sasa usikose semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019. Taarifa za semina ya 2019 zitatolewa mapema zaidi ili uweze kujiandaa mapema.

Juma #45; THE BORON LETTERS; ili kuwa na afya bora, fanya mazoezi kila siku, hasa kukimbia, funga siku moja kwa wiki na kula chakula bora.

Juma #46; THE GREAT GAME OF BUSINESS; Njia bora ya kuendesha biashara ni kuwa na uwazi, kwa kila aliye kwenye biashara, hasa waajiriwa kujua kila kitu kinachoendelea kwenye biashara. Kujua kiasi cha mtaji, mauzo, gharama za uendeshaji na hata faida. Makampuni mengi yamekuwa yanafanya taarifa hizi kuwa siri, lakini usiri huu ndiyo unapelekea makampuni mengi kufa.

Juma #47; 151 QUICK IDEAS TO INCREASE SALES; Zipo njia nyingi za kuwafikia wateja wa biashara yako, tumia nyingi uwezavyo na usitegemee moja au chache pekee. Njia unazoweza kutumia; matangazo, maonesho ya kibiashara, taarifa kwa uma, tovuti, mauzo ya moja kwa moja, uandishi na mafunzo mbalimbali.

Juma #48; THE ART OF MONEY GETTING; Njia ya kuelekea kwenye utajiri iko wazi kama njia ya kuelekea kisimani. Fursa zipo nyingi na kwenye kila sekta kwa yeyote anayetaka kupata fedha. Kwa kuijua na kuifuata misingi ya kupata mafanikio na utajiri, kila mtu anaweza kutengeneza utajiri mkubwa kwenye maisha yake.

Juma #49; THE ATTRACTOR FACTOR; Sheria ya mvutano inasema kwamba chochote kinachotokea kwenye maisha hakiji kama ajali, badala yake kimevutwa. Hii ina maana kwamba, chochote ambacho kimewahi kutokea kwenye maisha yako na kila kitakachoendelea kutokea, hakiji kama ajali au bahati mbaya, bali ni wewe mwenyewe umevutia hicho kilichotokea. Wewe ndiye umekikaribisha na kukiruhusu kitokee.

Juma #50; THE DAILY ENTREPRENEUR; Kanuni kuu ya mafanikio kwenye ujasiriamali ni kuanzia sokoni, wengi huanza kufanya kitu kwa mapenzi yao wenyewe na siyo mapenzi ya soko. Kama unataka kufanikiwa, anza kujua watu wanataka nini kisha wape hicho wanachotaka.

Rafiki yangu mpendwa, hivyo ndivyo vitabu 45 ambavyo nilikushirikisha kwenye tano za juma za mwaka 2018. Pata muda wa kupitia kila cha kujifunza kwenye kila kitabu na kitumie kuyaboresha maisha yako.

#2 MAKALA YA JUMA; MAKALA 5 ZILIZOSOMWA SANA 2018.

Rafiki, kwa mwaka 2018 makala zifuatazo ndiyo zimesoma sana kwenye blog ya AMKA MTANZANIA.

Kama kwa sababu yoyote ile hukupata nafasi ya kuzisoma basi unaweza kuzisoma hapa;

USHAURI; Biashara Nzuri, Inayolipa Na Unayoweza Kuifanya.

USHAURI; Biashara Unazoweza Kuanza Kwa Mtaji Wa Tsh Laki Mbili Na Kuweza Kufanikiwa.

Biashara Kumi (10) Unazoweza Kuanzisha Mwaka Huu 2018 Na Ukapata Mafanikio Makubwa.

Hizi Ndizo Njia Sita Za Kukutoa Kwenye Umaskini.

Mbinu Saba(7) Za Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Ya Kundi Kubwa La Watu.

#3 TUONGEE PESA; MPANGO WA FEDHA WA KUANZA NAO 2019.

Rafiki, kama ambavyo umekuwa unajifunza kila siku, nimekuwa nasisitiza sana kuhusu umuhimu wa fedha, na kufikia utajiri na uhuru wa kifedha.

Nina neno moja muhimu sana kwako unapokwenda kuuanza mwaka 2019, neno hilo ni hili; kwa kila fedha utakayoingiza, iwe ni mshahara, faida, zawadi au hata kama umeokota, basi sehemu ya kumi ya fedha hiyo usiitumie, badala yake iweke pembeni kabisa na hii utaitumia kwa uwekezaji ili kuongeza kipato chako zaidi.

Kwa mwaka 2019 nashauri uwe na akaunti maalumu ambayo utakuwa unaweka fedha hizi, na akaunti hiyo usiwe na uwezo wa kutoa fedha, bali kuweka tu. Kisha jipime kwa mwaka mzima wa 2019, na mwaka utakapoisha basi angalia ni kiasi gani cha fedha umeweza kujilipa na tumia yote kwenye uwekezaji.

Kama akaunti ni ngumu kwako kufungua, nashauri usajili line maalumu ya simu ambayo utaitumia kuweka fedha hizo, ila weka namba ya siri kimakosa ili usiikumbuke kwa mwaka mzima na kila sehemu ya kumi ya kipato chako weka kwenye line hiyo, utaona kwa mwaka mzima umepiga hatua kiasi gani.

Rafiki, ishi kwa msingi huo muhimu sana wa kifedha kwa mwaka 2019 kisha mwisho wa mwaka nishirikishe matokeo uliyopata. Na kama utahitaji msaada zaidi wa jinsi ya kufanikisha hili usiache kuwasiliana na mimi.

#4 HUDUMA NINAZOTOA; HUDUMA MUHIMU KWAKO YA KUANZA NAYO MWAKA 2019.

Rafiki, katika kuuanza mwaka 2019 nimekuandalia zawadi bora sana ya kuuanza mwaka huo kwa mafanikio makubwa. Zawadi hiyo ni SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI.

Kwenye semina hii tutajifunza tabia kumi za kuishi kila siku ili kufikia utajiri mkubwa kwenye maisha yetu.

Semina itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki ukiwa popote pale bila ya kuacha shughuli zako.

Semina itaanza tarehe 03/01/2019 mpaka tarehe 13/01/2019.

Kupata nafasi ya kushiriki semina unalipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA (tsh 100,000/=) au kama huwezi hiyo unalipia ada ya kushiriki semina tu (tsh 20,000/=)

Namba za kufanya malipo ni 0755 953 887 au 0717 396 253 majina Amani Makirita.

Mwisho wa kulipia ni tarehe 02/01/2019 ila nafasi zikijaa kabla hutapata tena nafasi.

Unaweza kumlipia mtu wa karibu kwako akajifunza tabia hizi za kitajiri.

Kujiunga na kundi la semina hii tumia kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/JvJBnoKixGrJZpZdw3shRv  (kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hili).

Karibu sana tupate maarifa sahihi ya kutujenge tabia zitakazotufikisha kwenye utajiri mkubwa. Fanya malipo yako ya ada leo ili uweze kupata nafasi ya kujifunza TABIA HIZO 10 ZITAKAZOKUPELEKA KWENYE UTAJIRI MKUBWA.

Pia fanya malipo yako leo ili usikose nafasi ya kujifunza tabia hizo kumi za kitajiri na kuondoka na mpako mkakati wa kufanyia kazi kwenye maisha yako ya kila siku.

Rafiki, nimalize kwa kukuambia kauli hii moja muhimu sana, kinachokukwamisha siyo unachojua, bali kile usichojua. Na kwa upande wa tabia, zile tabia nzuri ambazo huzijui, ndiyo zinakukwamisha. Zijue tabia nzuri na muhimu kwa mafanikio, zifanye kuwa sehemu ya maisha yako, na kitakachobaki ni wewe kuvuna matunda ya tabia hizo nzuri.

Semina ya TABIA ZA KITAJIRI, ni semina ambayo hupaswi kuikosa kama umeamua kuwa makini na maisha yako. Jiunge sasa hivi na kundi hili la semina na ulipe ada ya tsh elfu 20 kwa namba 0717396253 au 0755953887 ili ujipatie nafasi hii adimu sana na ya muhimu kwa mafanikio yako.

Kujiunga na kundi la semina hii tumia kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/JvJBnoKixGrJZpZdw3shRv  (kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hili).

#5 TAFAKARI YA KUFIKIRISHA; KAULI KUU YA KUIISHI MWAKA 2019.

Rafiki yangu mpendwa, kila mwaka nimekuwa nakuandalia maneno matatu ambayo yanakuwa mwongozo kwetu kwa mwaka mzima.

Lakini mwaka 2019 tutafanya tofauti kidogo, tutakuwa na kauli ambayo tutaiishi kila siku ya maisha yetu kwa mwaka mzima. Na kauli hiyo itakuwa na maneno matatu ndani yake.

Kauli ambayo tutaiishi mwaka 2019 inatoka kwa Benjamin Franklin na kauli hiyo inasema;  “Early to bed and early to rise, makes a man healthy, wealthy, and wise”

Ikimaanisha kuwahi kulala na kuwahi kuamka kunamfanya mtu kuwa na afya bora, utajiri na hekima.

Je nani asiyetaka kuwa na afya bora? Nani ambaye asingependa kuwa tajiri? Na nani asiyetaka kuwa na hekima?

Hivi ni vitu vitatu ambavyo kila mmoja wetu anapenda kuwa navyo.

Na Ben Franklin ameshatupa kanuni ya kuvipata, ambayo ni kulala mapema na kuamka mapema.

Mwaka 2019 unakwenda kuwa mwaka wetu wa kulala mapema na kuamka mapema kila siku. Unapoamka mapema unapata muda mzuri wa kuianza siku yako kwa mafanikio makubwa.

Tutaiishi kauli hii kila siku ya maisha yetu kwa mwaka 2019.

Na pia maneno matatu ya mwaka 2019 yatakuwa AFYA, UTAJIRI na HEKIMA.

Karibu sana tuendelee kuwa pamoja mwaka 2019, kwani nimekuandalia mambo mazuri sana yatakayokuwezesha kupiga hatua kubwa zaidi kwenye maisha yako.

Nikutakie heri ya mwaka mpya 2019, ukawe mwaka wa mafanikio makubwa kwako.

Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)

Kupata huduma nyingine za ukocha tembelea www.amkamtanzania.com/kocha

Kupata vitabu vizuri vya kusoma tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu