Rafiki yangu mpendwa,

Tayari tumeimaliza miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu 2019. Makampuni makubwa ambayo yanauza hisa zake kwa umma huwa yanapaswa kutoa ripoti fupi ya kila robo mwaka.

Hiki ni kitu ambacho nataka na wewe uwe unafanya kwenye maisha yako, kwa sababu kitakupa manufaa makubwa sana.

Iko hivi rafiki, katika watu 100 walioweka malengo makubwa mwaka huu 2019, ni chini ya watu watatu wanaoendelea na malengo hayo mpaka sasa, saba wanayakumbuka lakini hawayafanyii kazi kila siku, na 90 wameshayasahau kabisa, ni mpaka tena mwaka mpya ujao watajiwekea malengo na kuyasahau.

Sasa hii ni njia ya uhakika ya kushindwa na kubaki na maisha yasiyo bora. Utafanikiwa kama utajiwekea malengo na kuyafanyia kazi kwa kipindi chote ulichojiwekea. Kama umejiambia kwamba mwaka huu utapiga hatua fulani, basi kila siku lazima uchukue hatua hiyo.

Na hii ndiyo maana ni muhimu sana kujipima kadiri unavyokwenda.

Nimekuwa nakushauri ujipime kila siku, kila unapoianza siku yako weka mipango ya siku hiyo, ukimaliza siku hiyo fanya tathmini, yapi umefanya vizuri, yapi umekosea na wapi pa kuboresha.

Pia unapaswa kujipima kila juma, mwanzo wa juma weka mipango ya juma unalokwenda kuanza na mwisho wa juma fanya tathmini jinsi juma zima lilivyokwenda, na ona maeneo ya kuboresha zaidi.

KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO

Kila mwezi pia lazima ujipime, kwa kuweka mipango mwanzo wa mwezi, na kisha mwezi unapoisha unajitathmini kuona hatua ulizopiga na maboresho ya kufanya.

Na sasa tunakwenda kwenye robo mwaka, kila baada ya miezi mitatu, lazima ujipime, kuona hatua ambazo umepiga ukilinganisha na malengo uliyojiwekea.

Kadiri kujipima kwako kunavyokuwa kwa karibu na kwa umakini, ndivyo unaona makosa unayofanya na jinsi ya kuyarekebisha.

Leo tenga muda wa kukaa na kutathmini miezi mitatu ya kwanza ya mwaka wako jinsi ilivyokwenda. Pitia malengo yote uliyojiwekea kwa mwaka huu 2019, kisha angalia utekelezaji ambao umefanya kwenye kila lengo.

Unapaswa kuwa umeshafikia robo kwenye kila lengo, hivyo angalia malengo yapi umezidi robo, yapi upo chini ya robo na yapi hujayagusa kabisa.

Rafiki, najua wengi hawapendi kufanya zoezi hili, kwa sababu hawataki kukutana na ukweli uso kwa uso, ukweli kwamba wamekuwa wazembe na hawafanyii kazi malengo yao. Wanapenda kujidanganya mpaka mwaka unaisha na wanajikuta hawajafanya chochote.

Wewe ukabili ukweli kama ulivyo, kama umekuwa mzembe kubali umekuwa mzembe na jisukume kuchukua hatua, hakuna unayeweza kumdanganya zaidi yako wewe mwenyewe.

Ukishaangalia miezi mitatu iliyopita, weka mikakati ya miezi mitatu ijayo, kisha gawa kwa kila mwezi na kwa mwezi husika gawa kwa wiki. Unapoanza wiki, angalia mpango wa wiki na ugawe kwa siku.

Kwa kufuata utaratibu huu rahisi wa kuweka mipango na kuitathmini, utaona madhaifu mengi uliyonayo na kuweza kuyarekebisha.

Fanyia kazi hili leo na unaweza kuubadili kabisa mwaka huu 2019 hata kama hukuuanza vizuri. Kumaliza robo ya haimaanishi umeshapoteza, bado una robo nyingine tatu ambazo ukiweza kuzifanyia kazi utapiga hatua zaidi.

Hatua za wewe kuchukua ili kuweza kuleta mabadiliko makubwa kwako kwa mwaka huu 2019.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, hili ni jambo ambalo unapaswa kulifanya sasa, maana ndani ya KISIMA siyo tu utajifunza kila siku, bali pia kujitathimini kila mwezi ni sehemu ya wajibu wako kama mwanachama. Tuma sasa ujumbe kwa wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA na utapata maelekezo ya kujiunga.

Kama bado hujajiunga na channel yetu mpya ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA unajichelewesha katika kupata hekima. Kuna maarifa mengi na ya viwango vya juu zaidi kutoka kwenye vitabu yanapatikana kwenye channel hii. Tuma sasa ujumbe kwa kutumia app ya TELEGRAM MESSENGER kwenda namba 0717396253 wenye maneno TANO ZA JUMA na utaunganishwa.

Na kama hujasoma vitabu vyote nilivyoandika, vipo vitabu 8, vipate sasa na kuvisoma. Vitabu vyote kwa jumla ni tsh elfu 60, lakini ukilipia elfu 30 utavipata vyote kama zawadi. Kupata zawadi hii ya vitabu tuma ujumbe kwa wasap namba 0717396253 wenye maneno ZAWADI YA VITABU na utapata maelekezo ya kuvipata.

Ipo huduma ya UKOCHA BINAFSI, ambapo unapata nafasi ya mimi kukusimamia kwa karibu kwenye chochote unachotaka kufanya au unachokwama kufanya. Hapa nakusimamia kwa karibu, kwa kukushauri vyema na kufuatilia hatua unazochukua pamoja na kukusaidia pale unapokutana na changamoto mbalimbali. Natoa zawadi kwa robo ya pili ya mwaka, kwa ambaye atapenda nimsimamie kwa miezi mitatu ijayo basi atalipia nusu ya ada kila mwezi. Huu ni uwekezaji ambao utakusaidia sana, jaribu kwa miezi mitatu tu na utaona jinsi ambavyo umekuwa unajizuia mwenyewe kufanikiwa. Kupata zawadi hii tuma ujumbe kwa wasap namba 0717396253 ujumbe uwe na maneno ZAWADI YA UKOCHA BINAFSI.

Rafiki, nikutakie kila la kheri kwenye robo ya pili ya mwaka huu 2019, ukajipange vyema, uchukue hatua na uweze kuwa bora sana. Kumbuka mimi kocha wako nipo kwa ajili yako, popote unapokwama usisite kunitafuta ili tukaweza kusaidiana na ukapiga hatua zaidi. Hakuna kinachoshindikana, hivyo karibu sana tufanye kazi pamoja kwa njia mbalimbali nilizokushirikisha hapo juu.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge

cropped-mimi-ni-mshindi