Rafiki yangu mpendwa,

Kadiri siku zinavyokwenda, ndivyo watu wengi wanavyojiona hawana udhibiti wa maisha yao. Wanajiona wanapelekwa tu na maisha bila ya kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi wanayoyataka wao.

Lakini hilo siyo sahihi, haijalishi upo kwenye hali gani, bado wewe una udhibiti mkubwa wa maisha yako. Unaweza kuwa umefungwa gerezani, unanyanyaswa na wengine, au unapitia ugumu mkubwa, lakini unapaswa kukumbuka hili, udhibiti wa maisha yako uko ndani yako.

Coach George Raveling, aliyekuwa kocha wa mpira wa kikapu, na sasa kocha wa mafanikio, ni mmoja wa watu ambao wamewekeza muda na maisha yao kwenye kujifunza na kushirikisha uzoefu wanaokutana nao kwenye maisha yake.

coach rav

Katika moja ya makala zake, Coach Rav anatushirikisha machaguo 23 kuhusu maisha yako ambayo yako ndani ya uwezo wako. Coach anatuambia kwa kufanya machaguo haya, tutaweza kuwa na udhibiti mkubwa wa maisha yetu na hakuna kitakachotuyumbisha.

Bila ya maelezo mengi, Coach Rav ametuorodheshea machaguo haya 23 ambayo tunapaswa kuyazingatia ili kuwa na uhuru mkubwa kwenye maisha yetu.

 1. Kuwa wewe, usiwe wao.

 

 1. Fanya zaidi, tarajia kidogo.

 

 1. Kuwa chanya, usiwe hasi.

 

 1. Kuwa suluhisho, usiwe tatizo.

 

 1. Kuwa mwanzilishi, usiwe mkwamishaji.

 

 1. Hoji zaidi, amini kidogo.

 

 1. Kuwa mtu fulani, usiwe mtu yeyote.

 

 1. Penda zaidi, chukia kidogo.

 

 1. Toa zaidi, pokea kidogo.

 

 1. Ona zaidi, angalia kidogo.

 

 1. Weka akiba zaidi, kuwa na matumizi kidogo.

 

 1. Sikiliza zaidi, ongea kidogo.

 

 1. Tembea zaidi, kaa kidogo.

 

 1. Soma zaidi, angalia kidogo.

 

 1. Jenga zaidi, bomoa kidogo.

 

 1. Sifia zaidi, kosoa kidogo.

 

 1. Safisha zaidi, chafua kidogo.

 

 1. Ishi zaidi, usiwe upo upo tu.

 

 1. Kuwa majibu, usiwe maswali.

 

 1. Kuwa mpenzi, usiwe adui.

 

 1. Kuwa mtuliza maumivu, usiwe mtoa maumivu.

 

 1. Fikiri zaidi, itikia kidogo.

 

 1. Kuwa wa tofauti, usiwe wa kawaida.

 

Rafiki, machaguo haya 23 yapo ndani ya uwezo wako, hapo ulipo sasa bila ya kujali unapitia nini au uko wapi. Fanya maamuzi hayo kila siku na maisha yako yatakuwa bora zaidi.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge

vitabu softcopy