Habari za leo rafiki yangu mpendwa,

Mwanzoni mwa mwezi huu wa mei nilikupa taarifa juu ya kuwepo kwa programu ya GAME CHANGERS mwezi juni 2019. Hii ni programu ya kipekee sana ambayo inalenga kukutoa pale ambapo mtu umekwama.

Programu hii inajumuisha nguvu mbili kwa wakati mmoja, nguvu ya kocha kama mtu anayekusimamia na kukuongoza kwa karibu na nguvu ya mastermind, yaani watu ambao mnaelekea sehemu moja na hivyo kusukumana wenyewe kwa wenyewe.

Three-Game-Changers

Baada ya muda mrefu wa kufanya kazi na watu hasa kwenye eneo la mafanikio, nimekuwa naona kitu kimoja kinachojirudia kwa wengi. Wengi wanaanza safari ya mafanikio wakiwa wanatokea chini kabisa, kipato kidogo, wapo kwenye madeni na maisha ni magumu. Hali hiyo inawapa hasira ya kujituma mno, wanajisukuma sana.

Kwa jinsi wanavyojisukuma, wanapata matokeo mazuri na hayo yanawasukuma kujituma zaidi. Lakini wanavyozidi kufanikiwa na kupiga hatua, ile hamasa inaanza kupungua. Wanakosa ule msukumo waliokuwa nao mwanzo na hapo hawapigi tena hatua. Hapa ndipo safari ya mafanikio ya wengi inapoishia.

Kinachowafikisha watu kwenye hali hii ni hali ya kifikra ambayo kama mtu hataweza kuivunja, hawezi kabisa kupiga hatua, hata akazane kiasi gani. Na kuvunja hali hiyo siyo kazi rahisi, inahitaji mtu ujitoe kweli, ujikane na kuanza upya kifikra, kufanya mapinduzi kabisa kwenye fikra zako.

Programu hii ni ya siku 30 ambapo mtu utaweza kufanyia kazi lile eneo muhimu ulilokwama kwenye maisha yako na uweze kupiga hatua kubwa. Na pia programu hii inakwenda kukujenga msingi ambao unaweza kuutumia kuendesha maisha mapya ya mafanikio kwako.

Gharama za kushiriki programu hii ni tsh laki tatu (300,000/=) na nafasi za kushiriki programu hii ni tano pekee. Nafasi ni chache sana ili kuweza kuwahudumia vizuri wale wanaochagua kuwekeza kwenye programu hii muhimu sana kwao kupiga hatua. Maana moja ya vitu vinavyofanyika kwenye programu hii ni mazungumzo ya simu kwa pamoja kwa watu wote walipo kwenye programu hii inayofanyika mara moja kila wiki, hivyo watu watano pekee ndiyo wanaweza kushiriki kwenye mazungumzo ya simu kwa pamoja.

TAARIFA MUHIMU. NAFASI ZA GAME CHANGERS ZIMESHAJAA.

Napenda kuchukua nafasi hii rafiki kukujulisha kwamba nafasi tano za kushiriki programu ya GAME CHANGERS kwa msimu huu wa JUNE 2019 zimeshajaa, zimejaa haraka sana kuliko nilivyotegemea, hii ni kuonesha jinsi ambavyo watu wana kiu kubwa ya kupiga hatua.

Licha ya nafasi hizi kujaa, bado watu wameendelea kuomba kushiriki kwenye programu hii, na kama nilivyoeleza awali, anayewahi ndiye anayepatiwa nafasi na zikishajaa tano hatuwezi kuongeza tena.

Lakini kwa kuwa mimi Kocha wako niko kwa ajili yako na kwa kuwa kazi yangu kuu ni wewe, kwa kuwa naamini kufanikiwa kwako ndiyo kufanikiwa kwangu, basi nimetafakari sana na kuona si vyema kuwanyima watu nafasi ya kupiga hatua kwenye maisha yao.

Sitaki mtu yeyote ajipe sababu kwamba kama angeipata nafasi basi angeweza kupiga hatua. Nataka kila mtu atumie kila fursa inayopatikana kujiwezesha kupiga hatua zaidi.

Hivyo basi nimeona nifungue msimu mwingine wa GAME CHANGERS kwa mwaka huu 2019, ambao utafanyika mwezi Agosti 2019. Lakini msimu huu mwingine hautatangazwa tena kama wa mwanzo, badala yake wale waliopenda kushiriki kwenye msimu huu na wakakosa nafasi basi ndiyo watakaopata nafasi ya kushiriki msimu wa GAME CHANGERS AGOSTI 2019.

Hivyo basi rafiki, kama ulipanga kushiriki GAME CHANGERS lakini umeikosa nafasi sasa, jiwekee nafasi yako mapema kwa mwezi AGOSTI.

Nafasi ni zile zile tano na anayewahi ndiye anayepewa nafasi, na nafasi zikishajaa hakuna tena nafasi nyingine. Hivyo nikusihi sana rafiki yangu, chukua hatua mapema, chukua hatua sasa hivi ya kutunza nafasi yako kwa ajili ya msimu wa mwezi AGOSTI 2019.

Kujiwekea nafasi yako, fungua hapa na ujaze fomu hii, utapewa maelekezo zaidi msimu utakapokaribia. Fungua hapa; https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSc3TYXVHGR03GQ7ZsSGir1slhEwN3Er3b1Y5rtYxoXsNEaWpw/viewform?usp=sf_link

Rafiki, nikukumbushe tu kwamba nafasi hizi tano ni chache sana kulinganisha na wenye uhitaji, hivyo kama moyo wako unakuambia hiki ni kitu unachohitaji, jaza fomu sasa hivi na endelea kufanya maandalizi ikiwepo ada ili uweze kushiriki kwenye msimu wa GAME CHANGERS AGOSTI 2019.

Nikutakie kila la kheri kwenye mapambano ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

Wako rafiki,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha