Rafiki yangu mpendwa,
Leo ninayo furaha kubwa sana ya kutambulisha kwako bidhaa mpya kabisa kati ya bidhaa nyingi za mafunzo ninazozitoa. Bidhaa hii ina nguvu kubwa ya kutusukuma ili tuweze kufanikiwa zaidi kwenye maisha yetu.
Bidhaa ninayokwenda kukutambulisha na kukukaribisha leo ni KLABU YA KISIMA CHA MAARIFA. Lakini kabla hatujaingia zaidi kwenye bidhaa hiyo, nikukumbushe kidogo chimbuko la KISIMA CHA MAARIFA.
Nilianzisha KISIMA CHA MAARIFA miaka mitano iliyopita (2014) kama sehemu ya wale wanaojifunza kwenye AMKA MTANZANIA kuweza kujifunza kwa kina zaidi na kuwa karibu na mimi kocha wao. Tulianza na wanachama wachache sana, chini ya kumi, baadaye tukakua mpaka wanachama 50, baadaye 100 na sasa zaidi ya 200.
Mafunzo ya KISIMA CHA MAARIFA kwa kipindi chote yamekuwa kwa njia ya mtandao isipokuwa semina moja ya mwaka ambayo inafanyika mara moja kila mwaka.
Jamii ya KISIMA CHA MAARIFA imekuwa jamii ya kipekee na ya tofauti sana ukilinganisha na jamii inayotuunguka. Hivyo tunahitaji kuiboresha zaidi jamii hii, kwa kuitoa mtandaoni na kuileta kwenye maisha yetu ya uhalisia.
KISIMA CHA MAARIFA kina wanachama waliosambaa nchi nzima ya Tanzania pamoja na wengine waliopo nje ya nchi. Hivyo tunakwenda kuanzisha klabu ya KISIMA CHA MAARIFA ambayo itawaleta pamoja wale waliopo eneo la karibu na kutengeneza jumuia bora kabisa ya mafanikio.



Kwa nini Klabu?
Upo usemi kwamba ulivyo wewe ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka. Yaani mafanikio yako hayawezi kuwazidi watu ambao unatumia nao muda wako mwingi.
Sasa kwa kuwa tupo watu ambao tuna kiu kubwa ya kufanikiwa, na ambao tunachukua hatua kubwa kufanikiwa, kama tutakaa pamoja, tutaweza kusukumana zaidi kufanikiwa.
Pia kwenye kitabu bora kabisa cha maendeleo binafsi na mafanikio kinachoitwa THINK AND GROW RICH, mwandishi Napoleon Hill anasema moja ya vitu unavyohitaji ili kufanikiwa ni kuwa na kikundi cha watu wanaokusukuma zaidi. Anakiita kikundi hiki MASTER MIND GROUP. Hivyo klabu ya KISIMA CHA MAARIFA itafanya kazi kama MASTER MIND GROUP, ambapo wanachama wa klabu hiyo watasukumana kufanikiwa zaidi.
Utaratibu wa klabu ya KISIMA CHA MAARIFA.
- Klabu ya KISIMA CHA MAARIFA itaanzishwa na wanachama hai wa KISIMA CHA MAARIFA ambao wapo ndani ya mkoa mmoja au wilaya moja. Idadi ya chini ya watu wanaohitajika ili kuanzisha klabu ni watu watano, idadi ya juu ni watu 10. Kama ndani ya wilaya moja kuna wanachama zaidi ya watano, wanaweza kuanzisha klabu yao. Kama hakuna basi kutakuwa na klabu ya mafanikio ya mkoa. Na kama ndani ya mkoa hakuna watu wanaofika watano basi waliopo watajiunga kwenye klabu iliyopo mkoa jirani.
- Klabu itakuwa na uongozi wake ambao utaratibu shughuli mbalimbali za klabu. Kutakuwa na mwenyekiti, katibu na mweka hazina.
- Hakutakuwa na ada ya ziada ya kujiunga na klabu, ukishalipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA tayari unakuwa na sifa ya kuwa mwanachama wa klabu. Ila kutakuwa na michango mbalimbali kulingana na shughuli nyingine za klabu.
- Kutakuwa na mkutano wa kila mwezi ambapo kila mwanachama wa klabu anapaswa kuhudhuria, mikutano itakuwa inafanyika kila jumapili ya kwanza ya mwezi, kuanzia saa nane mchana mpaka saa 12 jioni.
- Katika mikutano ya klabu, kila mwanachama atashirikisha kitabu alichosoma kwa mwezi mzima kwa aliyojifunza na anayokwenda kufanyia kazi, kueleza mipango aliyofanyia kazi na matokeo aliyopata, changamoto alizokutana nazo na pia atashirikisha mipango anayokwenda kufanyia kazi juma linaloanza. Wanachama wengine watatoa michango yao na kumshauri zaidi. Kitabu cha TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA kitatumika katika kujifunza kwenye mikutano ya mwezi.
- Kutakuwa na utaratibu wa wanachama wa klabu kutembeleana kwenye maeneo yao ya kazi au biashara ili kujifunza zaidi na kushauriana njia bora za kupiga hatua zaidi. Mwanachama anayetembelewa atawashirikisha wengine zile hatua anazopiga na changamoto anazokutana nazo pamoja na mipango mikubwa ya baadaye. Pia atatoa elimu ya kile anachofanya kwa wengine ili nao wajifunze na kuhamasika.
- Klabu zitajihuisha na shughuli mbalimbali za kijamii kama kutoa misaada kwa wenye uhitaji, kujihusisha kwenye shughuli za mazingira na pia kujihusisha na kuchangia kwenye utoaji wa huduma za kijamii kama afya na elimu.
- Kocha atatembelea kila klabu kuona shughuli mbalimbali za klabu na kuwatembelea wanachama na kuangalia maendeleo yao pamoja na kuwashauri zaidi.
- Kila klabu itakuwa na wajibu wa kukuza zaidi wanachama wake na kuwashirikisha watu wa karibu kujiunga na KISIMA CHA MAAARIFA na kujiunga na klabu. Kwenye kila mkutano wa mwezi, kila mwanachama atapaswa kuja na mgeni mmoja ambaye atashiriki sehemu ya mkutano, hasa ya kushirikishana yale ambayo watu wamejifunza na hatua walizopiga. Baada ya mkutano mtu atapewa ukaribisho wa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili apate sifa ya kujiunga na klabu.
- Kila klabu itajiwekea taratibu zake ndogo ndogo za uendeshaji kulingana na mazingira ya ilipo klabu, shughuli za klabu, michango mbalimbali ya wanachama na mengine muhimu kama kuboresha mahudhurio ya mikutano na kuongeza idadi ya wanachama. Taratibu hizi zitawasilishwa kwa Kocha kabla hazijaanza kutumika na kama kukiwa na mabadiliko pia yatawasilishwa kwa Kocha kwanza.
Hizo ndiyo taratibu kuu kumi za uanzishaji na uendeshaji wa KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA.
UZINDUZI WA KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA AGOSTI 2019.
Rafiki, tunakwenda kuzindua rasmi klabu hizi za KISIMA CHA MAARIFA jumapili ya kwanza ya mwezi Agosti 2019 ambayo itakuwa ni tarehe 04/08/2019 kuanzia saa nane kamili mchana mpaka saa kumi na mbili kamili jioni.
Kwenye siku hii ya uzinduzi wanachama wa klabu hizi nchi nzima watapata nafasi ya kujuana na kuweka mipango na taratibu mbalimbali za klabu.
Pia siku hiyo ya uzinduzi wa klabu za KISIMA CHA MAARIFA kutakuwa na uzinduzi wa vitabu viwili vilivyochapwa ambavyo ni TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA pamoja na kitabu ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.
Hii siyo nafasi ya mtu yeyote anayetaka kufanikiwa zaidi kuikosa.
Hakikisha unapata nafasi hii kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA LEO. Na kama tayari ni mwanachama ila ada yako inamalizika, lipa mapema ili unufaike na klabu hizi za KISIMA CHA MAARIFA.
Kama tayari umeshakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA au unapanga kuwa mwanachama siku za karibuni, fungua kiungo hiki na ujaze fomu ya kujiunga na KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA. Kiungo ni; https://forms.gle/ELbfvox7MWaaMQkX9
Nikukaribishe sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA rafiki, lakini pia nikukaribishe kwenye KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambapo tutapata nguvu ya kufanikiwa zaidi kupitia wale waliotuzunguka.
Kumbuka pia kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kushiriki semina muhimu kama ya KUTENGENEZA MFUMO WA BIASHARA YENYE MAFANIKIO ambayo itaanza tarehe 04/07/2019.
Semina hiyo itaendeshwa kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.
Ili ushiriki semina hii unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=) kabla ya tarehe 01/07/2019.
Rafiki, hiyo ni faida nyingine kubwa ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA leo kama bado hujawa mwanachama. Kazana uwezavyo uingie kwenye familia hii kuu ya wanamafanikio.
Kufanya malipo ili kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada tsh laki moja (100,000/=) kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 (majina ya namba hizo ni Amani Makirita) kisha tuma ujumbe wasap wenye majina yako na ujumbe kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na hapo utaunganishwa na uweze kunufaika na hayo mazuri.
KISIMA CHA MAARIFA ni sehemu pekee ambayo wale wenye kiu kubwa ya mafanikio wanapatikana, karibia sasa ujiunge nao na kwa pamoja tuweze kupiga hatua zaidi kwenye maisha yetu.
Kama bado hujajaza fomu ya kujiunga na KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA, fungua hapa; https://forms.gle/ELbfvox7MWaaMQkX9
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha
Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge