Rafiki yangu mpendwa sana,
Ni imani yangu uko vizuri, ukiendelea kupata maarifa sahihi na kuchukua hatua za tofauti ili kuyafanya maisha yako kuwa bora sana. Kama ndivyo basi hiyo ndiyo furaha yangu kubwa sana.
Naweka nguvu kubwa kukuandalia maarifa sahihi kwako ambayo yatakuwezesha wewe kuchukua hatua sahihi na utoke popote ambapo umekwama na kupiga hatua zaidi.
Msingi mkuu ninaouishi ni huu, ili nifanikiwe inabidi wewe ufanikiwe kwanza. Yaani sitaweza kuwa na mafanikio makubwa kama wewe hutakuwa na mafanikio makubwa. Ndiyo maana naweka nguvu kubwa sana kwenye hili.
Kesho tarehe 04/07/2019 tunakwenda kuanza semina yetu ya KUTENGENEZA MFUMO WA BIASHARA YENYE MAFANIKIO. Ni moja ya semina ambazo zitawawezesha wale wote wanaomiliki biashara au wanaopanga kuingia kwenye biashara kufanya biashara zao kwa uhuru mkubwa na kuweza kupata mafanikio makubwa.
Katika kipindi hiki cha semina, ambayo itakwenda mpaka tarehe 14/07/2019 nitaweka nguvu zangu zote kwenye kuendesha semina hii. Hivyo baadhi ya mafunzo ninayotoa yatasimama.
Moja ya mafunzo yatakayosimama ni email ambazo nimekuwa nakutumia kila siku, za DAKIKA MOJA na mafunzo mengine.
Hivyo nachukua nafasi hii kukutaarifu kwamba hutapokea mafunzo kwa email mpaka tarehe 15/07/2019. Na siku hiyo ya tarehe 15 julai nitakuja kwako na taarifa nzuri sana, ambazo namalizia kuzifanyia kazi sasa. Nitakupa tarehe ya uzinduzi wa vitabu viwili ambavyo vimeshaanza kuchapwa, ambavyo ni TANO ZA MAJUKA 50 YA MWAKA na ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Rafiki, kaa mkao wa kula, kwani vitabu hivyo viwili vimesheheni maarifa bora sana ya kukutoa hapo ulipo sasa na kupiga hatua zaidi. Nisimalize uhondo kwenye hilo, nitakupa taarifa zaidi vitakapokuwa tayari.
Katika kipindi hiki ambacho hutapokea mafunzo kwenye email, nakusihi utembelee www.amkamtanzania.com kila siku na usome makala nyingi sana zilizopo huko ambazo ni bure kabisa. Lakini pia makala ya TANO ZA JUMA itaendelea kwenda hewani kila jumapili, pamoja na makala ya juma kutoka kwenye kitabu cha juma. Na kwa wale ambao tayari ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, makala za KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO zitaendelea kwenda hewani kila siku.
ZAWADI KWA AMBAO HAWAJAWEZA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA BIASHARA.
Rafiki, najua wapo wengi ambao hawajaweza kushiriki semina ya MFUMO WA BIASHARA kutokana na sababu mbalimbali, na kwa wengi kushindwa kumudu ada ya kulipa.
Lakini mimi rafiki yako sitakuacha mikono mitupu, badala yake nakupa zawadi ya vitabu kumi (10) ambavyo nimevisoma kwa kina wakati naandaa masomo haya. Hivyo vipate vitabu hivi, tenga muda na visome na fanyia kazi yale unayojifunza, utapiga hatua kubwa sana.
Rafiki, nimekuwa nakuambia kuna vitu vitatu ambavyo LAZIMA uviwekeze ili kupiga hatua. Vitu hivyo ni MUDA (time), FEDHA (money) na UMAKINI (attention). Kama huwekezi vitu hivyo vitatu, huwezi kupiga hatua yoyote. Hivyo kwenye vitabu hivi 10 ninavyokutumia, wekeza MUDA na UMAKINI wako na utaondoka na maarifa bora kabisa.
Na siku utakayoweza kumudu kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA masomo ya semina hii ya MFUMO WA BIASHARA utayapata na yatakuwezesha kupiga hatua zaidi.
Kupata zawadi hiyo ya vitabu 10 vitakavyokuwezesha kutengeneza mfumo bora wa kuendesha biashara yako bonyeza maandishi haya.
Ukifungua hayo maandishi chagua kupakua kitabu kimoja kimoja na anza kuweka muda kusoma na kuchambua yale utakayofanyia kazi mara moja.
Vitabu kumi na moja nilivyokupa zawadi ni kama ifuatavyo;
- The Personal MBA: Master the Art of Business by Josh Kaufman
- MBA in a Day: What You Would Learn at Top-Tier Business Schools by Steven Stralser
- Work the System: The Simple Mechanics of Making More and Working Less by Sam Carpenter
- The 4-Hour Work Week by Timothy Ferriss
- Just Run It!: Running an Exceptional Business is Easier Than You Think by Dick Cross
- Traction_ Get a Grip on Your Business by Gino Wickman
- The E-Myth Revisited (2009) by Michael E. Gerber
- The Checklist Manifesto- How to Get Things Right (retail) by Atul Gawande
- Built to Sell by John Warrillow
- 101 Crucial Lessons They Don’t Teach You in Business School
Nikutakie wakati mwema rafiki yangu, endelea kujifunza, endelea kuchukua hatua mpya na mafanikio yatakuwa ni yako.
Tutaendelea kuwa pamoja kuanzia tarehe 15 julai ambapo nitakuja kwako na habari njema sana kuhusu uzinduzi wa vitabu viwili vinavyochapwa sasa.
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha
Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge