Rafiki yangu mpendwa,

Aliyekuwa mwandishi na mhamasishaji maarufu Jim Rhon amewahi kunukuliwa akisema, mafanikio huwa yanaacha alama, kama utafanya kile ambacho waliofanikiwa wanafanya, na wewe lazima ufanikiwe.

Huu ni ukweli usiopingika kwamba mafanikio huwa yanaacha alama, mafanikio siyo siri, mafanikio yapo wazi kabisa kama tutakuwa tayari kujifunza kupitia wale waliofanikiwa na kupiga hatua zaidi.

Lakini kwa kuwa kwenye jamii zetu waliofanikiwa ni wachache kuliko ambao hawajafanikiwa, na kwa kuwa waliofanikiwa huwa siyo wafundishaji wazuri wa mafanikio yao, mafanikio yamekuwa yanaonekana kama ni siri fulani.

Pamoja na urahisi wa upatikanaji wa maarifa mengi kuhusu mafanikio, bado watu wengi wamekuwa hawapati maarifa sahihi ya kuwawezesha kupiga hatua. Mara nyingi watu wamekuwa wanapata hamasa pekee lakini hawana mkakati wa kufanyia kazi ili kupiga hatua.

Lakini pia mtandao wa intaneti umejaa kila aina ya maarifa ambayo kwa wengi yamekuwa usumbufu badala ya msaada. Wengi wanajikuta wakisoma kitu kimoja kinachoeleza siri fulani ya mafanikio, wakitoka hapo wanaenda kusoma kitu kingine kinachopinga kile cha kwanza.

Mfano unasoma kwenye mtandao mmoja kwamba ili ufanikiwe unahitaji kufanya kazi sana, unahitaji kujinyima starehe na usingizi kwa kipindi fulani. Ukienda kwenye mtandao mwingine unaambiwa hupaswi kujitesa, unapaswa kuwa na maisha yenye mlinganyo, upate muda wa kutosha wa kupumzika na kulala. Hapo unabaki njia panda, usijue kipi cha kubeba na kufanyia kazi.

Kutokana na changamoto hii ya kukosekana kwa mwongozo sahihi wa mafanikio, nimekuandalia kitabu ambacho kitakuwa mwongozo wako wa maisha ya mafanikio kwa mwaka mzima.

Kitabu hiki kina mkusanyiko wa mambo matano ya kujifunza na kufanyia kazi kila juma majuma 50 ya mwaka. Ni kitabu kikubwa kiasi na ambacho hupaswi kukisoma kwa haraka. Badala yake kila juma unasoma sura moja ambayo inakuwa na vitu vitano.

Kitabu hiki kinaitwa TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA.

KITABU; TANO ZA MAJUMA YA MWAKA

Kitabu kimeanza na mwongozo wa maisha ya mafanikio ambao ni msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA. Huu ni msingi unaopaswa kujijengea kabla hata hujafanikiwa, kwa sababu ukifanikiwa bila msingi huo, kitakachofuata ni majanga.

Pia kitabu kitakuonesha kipimo sahihi cha muda kwako, ambacho ni juma, na ndani ya juma kuna masaa 168, hivyo utaweza kuyapangilia vizuri ili usipoteze muda wowote ule. Kwenye kitabu kuna chati nzuri ya matumizi ya muda wako wa juma, ambayo ukiifuata utaweza kufanya makubwa sana.

MAMBO MATANO YA KUJIFUNZA NA KUFANYA KILA JUMA.

Kitabu ni TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA, hivyo kila juma kuna mambo matano ya kujifunza na kufanya ili kupiga hatua zaidi.

SIRI 50 ZA MAFANIKIO.

Jambo la kwanza utakalojifunza na kufanyia kazi kila juma ni siri za mafanikio. Utajifunza siri 50 za mafanikio. Na zinaitwa siri siyo kwa sababu ni siri, bali kwa sababu wengi hawaoni na kutumia.

Kila juma kuna siri moja ya mafanikio utakayojifunza na kuiishi kwa juma zima na ikaleta matokeo bora sana kwenye maisha yako.

VITABU 50 VYA MAFANIKIO.

Kila juma utasoma uchambuzi wa kitabu kimoja cha mafanikio. Mpaka sasa unajua umuhimu wa vitabu kwenye mafanikio yako. Pamoja na kujua umuhimu huo, huenda hupati muda wa kutosha wa kusoma vitabu vingi.

Kwa kusoma kitabu hiki cha TANO ZA JUMA, utaweza kusoma uchambuzi wa kina wa vitabu 50 bora kabisa vya mafanikio.

Hivyo kila juma utasoma uchambuzi wa kitabu kimoja, utaondoka na mambo unayokwenda kufanyia kazi kwenye juma hilo. Kwa mpango huu ndani ya mwaka unakuwa umejifunza kutoka kwenye vitabu zaidi ya 50.

MAKALA 50 ZA MAFANIKIO.

Kila siku kuna makala nzuri sana ninazokuandikia na kukushirikisha kupitia mtandao wa AMKA MTANZANIA (www.amkamtanzania.com).

Katika makala hizo nzuri za kila siku, kuna ambazo huwa zinasoma sana kuliko nyingine. Hivyo kama watu wanasoma zaidi makala fulani, ina maana ndani yake kuna kitu kikubwa na kizuri.

Kwenye kitabu cha TANO ZA JUMA nimekukusanyia makala 50 za mafanikio ambazo zimesomwa sana kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA. Makala hizi zinakupa maarifa na hamasa ya kufanikiwa zaidi.

TUONGEE PESA.

Kipengele cha nne kwenye mambo matano ya kufanya kila juma kwa mwaka mzima nimekiita TUONGEE PESA. Iko hivi rafiki, kuongelea fedha kwenye jamii zetu huwa inaonekana kama ni kitu kibaya, kama uchuro hivi. Hivyo watu wengi wamekuwa hawaongelei mambo ya fedha kwenye jamii zetu. Na hali hiyo inakuza zaidi tatizo la kifedha.

Hivyo kwenye kipengele hiki cha TUONGEE PESA, tunajadili kwa uwazi mambo yote muhimu kuhusu fedha, mambo ambayo wengi hawapendi kuyazungumzia.

Mambo kama umasikini ni mbaya, utajiri ni mzuri, matajiri ni watu wazuri na kadhalika. Kila juma utapata maongezi muhimu kuhusu fedha ambayo yatakutoa kwenye fikra za uhaba wa kifedha na kukupeleka kwenye utele wa kifedha.

TAFAKARI 50 ZA KUFIKIRISHA.

Kipengele cha tano kwenye mambo yako matano ya kujifunza kwenye kila juma lako ni TAFAKARI ZA KUFIKIRISHA. Hizi ni kauli tata kutoka kwa wale waliofanikiwa zaidi, ambazo zinatufanya tufikiri upya namna ambavyo tumekuwa tunachukulia mambo yetu.

Kila juma utapata tafakari ambayo itakuamsha usingizini na kukufanya uuone uhalisia kama ulivyo na hivyo kuchukua hatua sahihi ili kupiga hatua zaidi.

JINSI YA KUPATA KITABU HIKI.

Kitabu cha TANO ZA JUMA kimechapwa (Hardcopy) na kinapatikana kwa uwekezaji wa shilingi elfu 50 (50,000/=). Ni kitabu kikubwa kiasi na ambacho utakisoma kwa mwaka mzima, hivyo ni uwekezaji ambao utakulipa sana.

Kitabu hiki unaletewa pale ulipo kama upo jijini Dar es salaam. Na kama upo mkoani basi unatumiwa kwa njia ya basi.

Kupata kitabu tuma ujumbe kwenye namba 0717396253 au 0755953887 na kisha utaweza kulipia na kupata kitabu chako ambacho utakisoma kwa mwaka mzima na kupata maarifa sahihi kwako kupiga hatua zaidi.

ZAWADI YA KUPATA KITABU HIKI.

Rafiki yangu mpendwa, kwa kuwa nilishakuambia kazi yangu ni wewe, nimekuandalia zawadi nzuri ya kupata kitabu hiki cha TANO ZA JUMA.

Kama utakinunua kitabu hiki mapema kabla ya tarehe 01/08/2019 basi utakipata kwa bei ya zawadi ambayo itakuwa tsh elfu 40 (40,000/=) badala ya elfu 50.  Hivyo chukua hatua ya kupata kitabu hiki leo hii ili uweze kunufaika na zawadi hiyo ya kipekee sana kwako.

Pia kwa kununua kitabu hiki cha TANO ZA JUMA, unapata bure vitabu vyote 50 vilivyochambuliwa kwenye kitabu hicho kwa mfumo wa nakala tete. Utaunganishwa kwenye CHANNEL YA TANO ZA JUMA kwenye mtandao wa telegram ambapo utaweza kupakua vitabu vyote 50 bure kabisa. Na kama utapendelea kubaki kwenye channel hiyo kwa mwaka mzima ili uendelee kupata maarifa zaidi kutoka vitabuni basi utapewa utaratibu wa kunufaika na hilo.

Karibu sana rafiki yangu uwekeze kwenye maarifa sahihi kwa mafanikio yako. Kwa kupata, kusoma na kufanyia kazi yale utakayojifunza kwenye kitabu cha TANO ZA JUMA, utaweza kuwa mtu wa tofauti kabisa na kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.

Tuwasiliane sasa kwa namba 0717396253 au 0755953887 ili ujipatie kitabu chako.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge