Rafiki yangu mpendwa,

Watu wengi wamechagua kuishi kwenye utumwa wa kujitakia wao wenyewe, lakini wasijue kama wao ndiyo wametengeneza utumwa huo.

Hii ni kwa sababu jamii zetu zina tabia ya kulalamika na kulaumu, pale jambo linapotokea, basi watu huangalia nani wa kutupiwa lawama. Na cha kushangaza, huwa hakosekani wa kutupiwa lawama.

Inapokuja kwenye swala la fedha, watu wengi kipato chao hakitoshelezi, wapo kwenye madeni na hawana maandalizi yoyote ya maisha ya baadaye.

WhatsApp Image 2019-07-13 at 18.40.50

Badala ya watu hawa kukaa chini na kuona wapi wanakosea ili waweze kurekebisha, wao wanatafuta nani wa kulaumiwa. Na hapo serikali inapata lawama mno, waajiri ndiyo usiseme, uchumi nao unalaumiwa. Watu wakikosa kabisa cha kulaumu wapo tayari hata kuwalaumu wazazi wao kwa mambo waliyofanya miaka 20 iliyopita. Wengine wamekuwa wanajitoa ufahamu na kuwalaumu watoto waliowazaa wao wenyewe kama ndiyo sababu ya wao kuwa na changamoto ya kifedha.

Rafiki, leo nataka nikupe ukweli kama ulivyo, na sitakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kama ambavyo umekuwa unadanganywa na kujidanganya wewe mwenyewe.

Upo kwenye matatizo ya kifedha kwa sababu huna elimu sahihi inayohusu fedha. Chochote unachojua kuhusu fedha umeiga kwa watu wako wa karibu, ambao nao hawajawahi kupata elimu sahihi ya kifedha.

Na kudhibitisha hili, hebu fikiria ni lini umewahi kukalishwa chini, iwe ni nyumbani, shuleni au popote na kufundishwa misingi sahihi ya kifedha? Hakuna. Tena kwenye jamii zetu ukionekana unaongelea fedha sana unaonekana ni mtu mwenye tamaa, mtu mwenye roho mbaya na asiyejali.

Kwa mazingira haya, kila mtu amekuwa anakufa kimyakimya na kivyake, kila mtu ana mzigo mkubwa wa matatizo kifedha, lakini hakuna hatua anazochukua ili kuondoka kwenye matatizo hayo.

Na hapa ndipo mimi rafiki yako, ninayekupenda na kukujali sana, nakuja kwa ajili ya ukombozi wako. Nimeandika kitabu kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, hiki ni kitabu ambacho kinakupa mafunzo yote muhimu ambayo unapaswa kuwa nayo kuhusu fedha, na kuyafanyia kazi.

Ukijifunza mafunzo haya na kuyafanyia kazi, kuna vitu VINNE (04) vitakavyotokea kwenye maisha yako, kwa uhakika kabisa. Na vitu hivyo sitakuambia mimi, bali atakuambia mtu ambaye alikuwa amekwama kifedha kama wewe, akapata elimu hii ya MSINGI YA FEDHA, na maisha yake yakabadilika sana.

Vitu vinne vitakavyotokea kwenye maisha yako baada ya kusoma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kama alivyotushuhudia rafiki yetu Huvira Hezron.

Asante Kocha,

Cha ajabu ni kwamba hata ukitoka hiyo tarehe 25  tarehe 30 yote imeshatumika tena kwa kulipa madeni na ni baadhi tu wala sio yote.

Binafsi tangu niipate hii elimu ya msingi ya fedha nimeokoka.

Kwanza sina pressure ya kulipa madeni maana sina.

Pili nina mwongozo wa matumizi hata kabla sijapokea mshahara. Ninajua kupanga mafungu kwa asilimia.

Tatu hata mshahara ukichelewa  sina pressure tayari nina vyanzo vingine vya mapato.

Nne nina account ya fedha ya dharura hivyo nina utulivu moyoni. – Huvira H.

Rafiki, umejisomea mwenyewe hapo, jinsi ambavyo ELIMU YA MSINGI YA FEDHA inaweza kuwa na manufaa makubwa sana kwako, na kukuondoa hapo ulipokwama sasa.

Basi sasa usijicheleweshe, kama bado hujapata na kusoma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, chukua hatua leo kukipata na kuanza kukisoma.

Kitabu ni nakala ngumu (HARDCOPY) na kinapatikana kwa gharama ya elfu 20. Kukipata piga simu namba 0678 977 007, kama upo dar utaletewa ulipo, kama upo mkoani utatumiwa kwa basi.

Usiendelee kuteseka na changamoto za kifedha huku ukilaumu watu ambao hawana msaada kwako. Shika sasa hatamu ya maisha yako kifedha kwa kupata maarifa sahihi na kuyafanyia kazi.

OMBI MUHIMU; Kama umepata mafunzo haya ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na yakawa na manufaa kwako naomba utushirikishe ushuhuda wako ni jinsi gani mafunzo haya yamekusaidia. Ushuhuda wako utakuwa kichocheo cha wengine nao kuchukua hatua ili waondoke kwenye changamoto. Tuma ushuhuda wako kwa kujibu email hii au kutuma kwenda kwenye email maarifa@kisimachamaarifa.co.tz

Asante sana.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha