Watu hawapendi upweke, hawapendi kuwa upande wao peke yao, wanapenda kuwa kwenye kundi kubwa, kwa namna wanavyofikiri na kufanya maamuzi.
Hii ndiyo sababu dini, jumuia mbalimbali, vyama vya siasa na hata timu za michezo huwa zinapata wafuasi, hata kama zinaonekana ni za hovyo kiasi gani.
Watu wanapenda sana kuamini kwenye kitu, na pale wanapoona kuna watu wengine wanaoamini kwenye kitu hicho, basi imani yao inakuwa kubwa zaidi na wanakuwa waaminifu kwenye kitu hicho.
Watu hawapendi kufanya maamuzi wenyewe, hata kama yapo ndani ya uwezo wao. Wanapenda kupata mwongozo wa wengine na kufanya kile ambacho wengine wanafanya, hata kama siyo sahihi. Watu wanaamini sana kwenye nguvu ya kundi, kwamba kama kitu kinafanywa na watu wengi, basi ni sahihi, japo siyo kweli.
Watu ni wa-kabila, wanapenda kujitambulisha kwa kikundi wanachotokea au kuhusika nacho.
Sasa unawezaje kutumia yote haya kwa manufaa yako? Badala ya kukaa na kulalamikia hali hizo za watu?
Kwa kazi au biashara yoyote ile unayofanya, tengeneza hali ya jumuia, ambapo wateja wako wanapata nafasi ya kujumuika pamoja. Kwa kufanya biashara na wewe, wanapata nafasi ya kuwa ndani ya kundi fulani la kipekee, ambalo linamvutia mtu huyo na kumfanya ajisikie vizuri. Kwa njia hii, wateja hao wataendelea kuwa waaminifu kwako.
Njia nyingine ni pale unapotangaza biashara yako, onesha jinsi ambavyo watu wengine wanaitumia na wamenufaika nayo, tumia shuhuda za wale ambao wameshanufaika na biashara hiyo, mtu kwa kuona wengine tayari wananufaika, hatotaka kuachwa nyuma.
Mwisho, unafikiri kwa nini baadhi ya makampuni yanakuwa na matangazo kama; ‘wajanja wote tayari wanatumia hii… wewe unasubiri nini?’
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante kocha kweli weng wanapenda kufanya kile kinachokubalika natwengi
Hata kama siyo sahihi nguvu ya kundi ni tatizo
LikeLike
Kabisa,
Sasa kwa kuwa hatuwezi kuwabadili watu, tunapaswa kutumia hilo kwa manufaa.
Kutengeneza kundi ambalo litawavuta wengine kwenye kile tunachofanya.
LikeLike