Unaendeleaje rafiki yangu mpendwa?

Ni imani yangu kwamba unaendelea kuweka juhudi kubwa kwenye maisha yako ili kuweza kupata matokeo bora na kupiga hatua zaidi kimafanikio. Kama ambavyo nimekuwa nakuambia, mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa, hakuna anayeweza kukuzuia kufanikiwa, wala hakuna anayeweza kukulazimisha kufanikiwa. Ni hatua unazochukua au kutochukua ndiyo zinapima mafanikio yako.

Kila siku endelea kuweka juhudi kubwa kwenye kila unachofanya ili kuendelea kupiga hatua zaidi, kwa sababu haijalishi umefika wapi sasa, bado unaweza kwenda juu zaidi ya hapo ulipofika sasa.

Napenda kuchukua nafasi ya leo kukukumbusha kuhusu semina yetu ya mafanikio, inayofanyika mara moja kila mwaka ambayo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii inawakusanya wanamafanikio wote kutoka kila kona ya Tanzania na hata walio nchi jirani, kukaa pamoja kwa siku nzima wakijifunza na kuhamasika ili kwenda kuchukua hatua kubwa zaidi kwenye maisha yao.

9D1A5674

Semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 inakwenda kufanyika jumapili ya tarehe 03/11/2019 kwenye moja ya hoteli zilizopo jijini Dar es salaam. Inakuwa semina ya siku nzima, kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja usiku. Ukitoka kwenye semina hii, unakuwa na maarifa na hamasa ya kutosha kukusukuma kwa mwaka mzima.

Ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 ni tsh laki moja (100,000/=) ambayo itachangia kupata ukumbi mzuri wa kufanya semina hii, chakula na huduma zote muhimu kwa sababu semina hii itakuwa ya siku nzima. Mwisho wa kulipa ada hii ni tarehe 31/10/2019 lakini una nafasi ya kulipa kidogo kidogo ili usikose nafasi hii.

Kuhakikisha hukosi nafasi ya kushiriki semina hii, tuma ujumbe wenye majina yako na namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki semina ya 2019 kwenda namba 0717396253, kwa kufanya hivyo utaihifadhi nafasi yako ya kushiriki semina hii. Tuma ujumbe sasa kama bado hujafanya hivyo na anza kufanya malipo yako sasa ili usikose nafasi hii ya kipekee sana inayokuja kwako mara moja tu kwa mwaka.

Sababu Kumi Kwa Nini Hupaswi Kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.

Hapa ninakushirikisha sababu kumi kwa nini hupaswi kabisa kukosa semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA ya mwaka 2019. Zisome na chukua hatua mara moja.

  1. Ni semina pekee ninayofanya kwa mwaka. Kama umekuwa unauliza mbona huna semina za kawaida, kwa nini unafanya semina za mtandaoni pekee? Majibu ni kwamba nina semina moja kila mwaka, na kwa mwaka huu 2019 inafanyika tarehe 03/11/2019. Ukikosa hii ni mpaka tena mwaka 2020 kipindi kama hicho. Hivyo usikubali kukosa nafasi hii ya kipekee sana kwako kujifunza.
  2. Ni njia rahisi ya mimi na wewe kuonana. Baadhi ya watu ambao wamekuwa wanaomba tuonane wamekuwa wanaona ni jinsi gani zoezi hilo lilivyo gumu. Hii ni kutokana na ufinyu wa muda na mambo mengi ya kufanya. Kwenye semina hii utakuwa na mimi siku nzima, kuanzia asubuhi mpaka jioni. Na utakuwa na ruhusa ya kuniuliza swali lolote unalotaka kuniuliza, ambalo labda umekuwa unajiuliza siku nyingi bila kupata majibu. Utaweza kupata ushauri wangu wa moja kwa moja kwa changamoto yoyote unayopitia.
  3. Utakutana na walimu wengine kwa wakati mmoja. Kwenye semina hii kutakuwa na walimu wengine mbalimbali, baadhi ya walimu hao ni Paul Masatu ambaye atatufundisha UMUHIMU WA KUJIJENGA KIHISIA KATIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA na Hamisi Msumi ambaye atatufundisha JINSI YA KUJENGA MAHUSIANO BORA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO. Hii ina maana ndani ya semina moja, utajifunza mambo mengi ambayo yanakuhusu moja kwa moja kwenye safari yako ya mafanikio.
  4. Unazungukwa na watu chanya, watu ambao siyo rahisi kuwakuta sehemu moja. Uzuri wa KISIMA CHA MAARIFA ni kwamba unakutana na watu ambao wameamua wao wenyewe, kwa hiari yao kukazana kuwa bora zaidi. Watu wa aina hii siyo rahisi kupatikana kwenye mazingira yetu ya kawaida. Hivyo utajifunza na kuhamasika kupitia wengine pia.
  5. Unapata nafasi ya kujifunza bila ya usumbufu. Tunaishi kwenye dunia yenye usumbufu. Katika zama hizi ni vigumu kupata nusu saa au saa moja yako peke yako ya kujifunza. Kwa sababu dunia inakupigia kelele, watu wanataka kuwasiliana na wewe na mengine mengi. Siku ya semina, unapata fursa ya kujifunza kwa siku nzima, bila ya kuwa na kitu cha kuondoa akili yako kwenye mafunzo unayopata.
  6. Ni wakati sahihi wa kuweka mipango yako ya mwaka 2020. Watu wengi huwa wanasubiri tarehe moja Januari ili kuweka malengo na mipango ya mwaka husika, lakini ndani ya mwezi mmoja, wanakuwa wameshasahau kabisa mipango hiyo. Kwenye semina hii unakwenda kuweka mipango yako ukiwa umetulia na siyo ukiwa na hamasa za mwaka mpya ambapo kila mtu anafanya hivyo. Kwenye Kisima cha maarifa, mwaka wetu wa mafanikio huwa unaanza mapema kabla ya mwaka mpya wa watu wengine. Hivyo mwezi novemba tunakuwa tayari na mipango yetu ya mwaka mzima na tunaanza kuchukua hatua kubwa. Semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA ndiyo mwanzo wa mwaka wetu wa mafanikio 2019/2020 hivyo unakwenda kujiwekea malengo unayokwenda kufanyia kazi.
  7. Kuwa ndani ya ukumbi wa semina kunakuongezea hamasa ya kujifunza na kuchukua hatua. Unaposoma makala au vitabu, mara nyingi unakuwa mwenyewe, hivyo kuna kitu unakikosa cha kukusukuma kuchukua hatua. Unapokuwa kwenye ukumbi wa semina, kuna nguvu kubwa unaipata pale unapoona wengine ambao wanajifunza na kupanga kuchukua hatua. Usikose nguvu hii.
  8. Kupata nafasi ya kuuliza na kupata ufafanuzi kwenye vitu ambavyo vimekuwa vinakupa utata. Huenda umekuwa unajifunza lakini unakutana na vitu ambavyo huvielewi au vinakupa utata. Unapokuwa unasoma mwenyewe, huwezi kupata majibu ya vitu hivyo. Ila unaposhiriki semina, unapata nafasi ya kuwauliza wengine na ukapata ufafanuzi wa kutosha.
  9. Ni sehemu ya kukuza mtandao wako wa watu unaofahamiana nao. Kumbuka tunaishi kwenye dunia ambayo siyo unajua nini ndiyo kunakusaidia, bali unamjua nani, na zaidi nani anakujua wewe. Semina kama hizi zinakupa fursa ya kujuana na watu wengi, na kuweza kupata fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuwa bora kwako.
  10. Utakwenda kujifunza kupitia shuhuda nyingi za wengine ambao wamepiga hatua kubwa. Semina ya mwaka huu 2019 itakwenda kuwa na shuhuda nyingi sana. Baada ya semina ya mwaka 2018 kuna programu mbili kubwa ambazo tumezijaribu kwenye KISIMA CHA MAARIFA ambazo ni GAME CHANGERS na LEVEL UP, programu hizi zimeleta matokeo makubwa sana ambayo hakuna aliyeyategemea. Kwenye semina hii tutakwenda kupata shuhuda za wale walioshiriki programu hizi na matokeo bora waliyopata, wapo wengi na matokeo ni mzuri sana. Unapoona wengine wanapiga hatua kubwa wakitokea chini au kwenye changamoto kubwa, unapata hamasa kubwa kumbe na wewe unaweza pia.
DSC_0096
WANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA KWENYE SEMINA YA MWAKA 2018

Rafiki yangu mpendwa, hizo ndizo sababu 10 kwa nini hupaswi kabisa kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, ni imani yangu umeona manufaa makubwa unayokwenda kupata kwenye semina hii. Hivyo usikubali kabisa kuikosa semina hii ya kipekee sana kwako.

Ukikosa hii ni mpaka tena 2020. Kama utakosa semina ya mwaka huu 2019, itakubidi usubiri mpaka mwaka 2020, hivyo kama kuna vitu ungeweza kuvifanyia kazi baada ya semina hii ili uwe bora zaidi, utavikosa, na hivyo kwa mwaka mmoja unaokuja, utaendelea kufanya unavyofanya sasa, kitu ambacho kitakuwa siyo kizuri kwako. Kazana sana ushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA ili usijicheleweshe kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa.

Tuma ujumbe leo hii wa kuweka nafasi ya kushiriki semina hii kwa namba 0717 396 253 na anza kufanya malipo kidogo kidogo ili mpaka kufikia tarehe 31/10/2019 uwe umeshakamilisha malipo yako ya tsh 100,000/= na uweze kuuanza mwaka wako mpya wa mafanikio ukiwa na hamasa na mikakati bora ya mafanikio.

Nakukaribisha sana kwenye semina hii, tujifunze na kuweka mikakati ya kufanyia kazi. Naamini hutakubali kuikosa semina hii, hivyo chukua hatua sahihi sasa.

Rafiki na kocha wako,

Dr. Makirita Amani.

www.amkamtanzania.com/kocha