Rafiki yangu mpendwa,
Napenda kukushukuru kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja, kipindi ambacho umekuwa unajifunza kupitia kazi mbalimbali ninazoshirikisha na kuweza kupiga hatua zaidi.
Huduma ninazotoa zimegawanyika kwenye makundi mbalimbali, kuna mtandao AMKA MTANZANIA na email ambapo kila mtu anapata mafunzo ninayotoa bure kabisa.
Halafu kuna KISIMA CHA MAARIFA na huduma za ukocha, hapa yule anayetaka kujifunza zaidi basi analipia kiasi fulani na tunakuwa karibu zaidi.
Moja ya huduma zilizopo kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni semina ya kukutana ana kwa ana ambayo huwa inafanyika mara moja kila mwaka. Kwenye semina hii, tunapata nafasi ya kuuanza mwaka mpya mapema kabla ya wengine, na hivyo tunakuwa mbele zaidi ya kundi kubwa la watu.
Lakini pia kwenye semina hizi, tunajifunza mikakati mbalimbali tunayokwenda kuitumia ili kupiga hatua zaidi. Tunajifunza pia kupitia shuhuda za wenzetu, ambao wanapambana na kupiga hatua kwenye maisha yao.
Hizi ni semina ambazo zinakuwa na watu chanya na wanaopambana kufanikiwa.
Kwa mwaka huu 2019, semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA itafanyika jumapili ya tarehe 03/11/2019 jijini Dar es salaam.
Ombi langu kwako wewe rafiki yangu ni moja, tafadhali thibitisha kama utashiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 leo hii, ili tuweze kufanya maandalizi bora kwa ajili ya semina.
Naomba leo hii uniambie kama utashiriki semina ha mwaka huu, nitumie ujumbe wenye majina yako kamili, email na namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki semina. Ujumbe utume kwa njia ya wasap namba 0717396253.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, karibu tujifunze, tuhamasike na kwenda kuchukua hatua kubwa zaidi ili kufanikiwa kwenye maisha yako.
Nijulishe leo hii kama utashiriki semina hii ili maandalizi yaweze kuwa bora.
Nikutakie kila la kheri.
Kocha Dr Makirita Amani.