“Leave the past behind, let the grand design take care of the future, and instead only rightly guide the present to reverence and justice. Reverence so that you’ll love what you’ve been allotted, for nature brought you both to each other. Justice so that you’ll speak the truth freely and without evasion, and so that you’ll act only as the law and value of things require.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 12.1
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Tumeipata nafasi nyingine ya kipekee kwetu, kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari HESHIMA NA HAKI…
Maeneo mawili tunayopaswa kuyasimamia kwa umakini ili kuwa na maisha bora ni HESHIMA NA HAKI.
Heshima ili kupokea na kupenda kile ulichopewa na asili, na kukitumia vizuri kwa ajili yako na wengine.
Haki ili kusimamia ukweli kwa uhuru na kutukuyumbishwa na chochote.
Kwa kusimamia maeneo hayo mawili, hutakuwa na nafasi ya kulalamika, kwa sababu kila unachopata utakitumia vizuri, kiwe kizuri au kibaya.
Lakini pia hutaweza kuwatendea wengine isivyo haki kwa sababu unajua ukiwaumiza wengine umejiumiza wewe mwenyewe pia.
Ukawe na sikubora sana ya leo, siku ya kuwa na HESHIMA na kutenda HAKI ili kuwa na maisha tulivu wakati wote.
#JengaHeshima #SimamiaHaki #FanyaKilichoSahihi
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1