“Walk the long gallery of the past, of empires and kingdoms succeeding each other without number. And you can also see the future, for surely it will be exactly the same, unable to deviate from the present rhythm. It’s all one whether we’ve experienced forty years or an aeon. What more is there to see?”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.49
Kuiona siku hii mpya ya leo, ni jambo bora na la kipekee sana kwetu.
Siyo kwa nguvu zetu, wala kwa akili zetu, bali ni kwa bahati tu.
Na njia bora ya kutumia bahati hii vyema ni kufanya kilicho sahihi, kuweka vipaumbele vyetu vizuri na kutokupoteza muda.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA.
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA.
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari; HAKUNA KIPYA…
Tukiangalia jana, na kisha kuangalia leo, tunajionea wazi kwamba kesho haiwezi kuwa tofauti sana na leo au jana.
Kila kinachotokea sasa kimewahi kutokea huko nyuma, na kitakuja kutokea tena siku za mbeleni.
Watu wamekuwa wanazaliwa na kufanya, imekuwa hivyo miaka mingi iloyopita na itaendelea kuwa hivyo kwa miaka mingi ijayo.
Tawala zimekuwa inaamzishwa, zinakua na kisha zinaangushwa, imekuwa hivyo tangu enzi za Roma, Hispania, Ufaransa, Uingereza na itaendelea.
Watu wamekuwa wanatapeliwa kwa njia mbalimbali zinazoahidi utajiri wa haraka bila ya kufanya kazi, imekuwa hivyo kwa miaka mingi, iko hivyo sasa na itaendelea kuwa hivyo.
Jambo la kusikitisha ni kwamba, sisi binadamu huwa hatujifunzi kutokana na historia, huwa tunajidanganya kwamba hali ya sasa hi tofauti au sisi wenyewe ni tofauti. Ni mpaka pale tunapoumia wenyewe, ndiyo tunajifunza kwamba hakuna utofauti.
Hatuna tofauti na watoto wadogo, ambao unaweza kuwakanya sana wasishike nyembe, ukawaeleza madhara yake, lakini wataenda kushika, na wakishajikata ndiyo wanalielewa somo.
Rafiki, wewe usisubiri mpaka uumie ndiyo ujifunze, jifunze kutoka kwa wale waliopita kwa sababu hakuna kipya. Jifunze kupitia historia na usirudie makosa ambayo wengine walishayafanya.
Wanasema mpumbavu huwa hajifunzi kabisa, mjinga hujifunza kwa makosa yake mwenyewe na mwerevu hujifunza kwa makosa ya wengine.
Kuwa mwerevu, usitake kurudia makosa ya wengine.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujifunza kutoka kwenye makosa ambayo wengine walifanya huko nyuma ili usiyarudie.
#HakunaKipya #HistoriaNiMwalimuMzuri #UsirudieMakosaYaWengine
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania