Heri ya mwaka mpya 2020 rafiki yangu mpendwa.

Ni nafasi ya kipekee sana kwetu tumeipata kuiona siku hii nyingine mpya, ya mwaka mwingine mpya. Siyo kwa nguvu zetu, wala kwa akili zetu, bali ni kwa neema tu. Hivyo tunapaswa kutumia nafasi hii vizuri, ili iwe na maana kwetu na wengine pia.

soma 2020.png

Najua huu ndiyo wakati ambao unaweka malengo yako ya mwaka huu mpya 2020.

Umeshajiambia mwaka mpya mambo mapya na umeazimia mambo mengi na makubwa.

Huenda umejiambia kwamba huu ndiyo mwaka wa kwenda kuanzisha biashara ambayo umekusa unajiambia utaanzisha muda mrefu.

Huenda huu ndiyo mwaka ambao umepanga kuanza ujenzi wa nyumba yako.

Huenda huu ndiyo mwaka ambao umepanga kuingia kwenye ndoa au kama upo kwenye ndoa umepanga kuboresha mahusiano yako na mwenza wako.

Na najua huu ni mwaka ambao umejiahidi kubadilika, kuna mambo mengi ambayo umejiahidi kuyaacha mwaka 2019 na sasa umekuja 2020 ukiwa mtu mpya.

Kwanza nikupongeze sana kwa kufikiri na kupanga mambo hayo mazuri sana kwa mwaka huu mpya 2020.

Lakini nikupe tahadhari na kukukumbusha tu kwamba kila mwaka umekuwa unapanga mambo mengi na mazuri, umekuwa unaweka malengo mazuri sana, lakini mwezi Januari unapoisha, unakuwa umeshasahau kabisa malengo hayo na kurudi kwenye maisha ya kawaida.

Sasa nataka nikusaidie mwaka huu 2020 uwe wa tofauti kwako, malengo yote uliyojiwekea uyafanyie kazi na kuyafikia.

Na hilo litawezekana kama tu utajiwekea lengo moja muhimu sana ambalo wengi huwa wanasahau kuliweka. Kwenye makala hii nitakushirikisha lengo hili, jinsi ya kuliweka na utekelezaji wake.

Lakini kabla ya kuingia kwenye lengo moja muhimu ninalokushauri ujiwekee kwa mwaka huu mpya 2020, nikushirikishe kauli moja kutoka kwa aliyewahi kuwa raisi wa Marekani, Abraham Lincolin. Aliwahi kunukuliwa akisema; ‘ukinipa masaa 6 ya kukata mti, nitatumia masaa 4 kunoa shoka langu.’

Hiyo ni kauli fupi, lakini iliyobeba ujumbe mkubwa mno, ambao ukiuelewa, mwaka huu 2020 utakuwa bora na wa kipekee sana kwako. Anachosema Lincolin ni kwamba, kabla hajakimbilia kufanya kile anachotaka, anahakikisha kwamba ana zana bora ya kufanya kitu hicho, kwenye kukata mti zana ni shoka, lakini kama shoka ni butu, utatumia muda mwingi na nguvu kukailisha kazi, lakini kwa shoka lililonolewa, nguvu kidogo muda mchache. Hivyo kama ataweka muda mwingi kwenye kunoa shoka, atakuwa na ufanisi zaidi kwenye kukata mti.

Na hicho ndiyo ninachotaka wewe rafiki yangu ufanye kwa mwaka huu 2020, ili uweze kufikia malengo yote uliyojiwekea 2020, tumia muda wako kunoa shoka lako, ambalo ni akili yako. Unapokuwa na fikra sahihi, zinafanya uwe na mtazamo sahihi kitu ambacho kitapelekea uchukue hatua sahihi na kisha kupata matokeo bora.

Lengo moja muhimu ninalokushauri ujiwekee kwa mwaka huu 2020 ni lengo la KUJIFUNZA KUPITIA USOMAJI WA VITABU. Kwenye vitabu (hasa vile ambavyo ni bora) kuna maarifa mengi sana ambayo yatakufanya uwe bora zaidi.

Kwa kila lengo ambalo umejiwekea, kuna vitabu vizuri na vyenye maarifa bora kabisa kwenye lengo hilo ambapo ukiwa nayo, hutakwamishwa na chochote.

Hivyo jiwekee lengo hili, na kila siku tenga muda wa kunoa akili yako, kupitia usomaji wa vitabu.

Kila siku jiwekee lengo la kusoma angalau kurasa 10 za kitabu, ukifanya hivyo kwa mwezi utasoma kurasa zisizopungua 300 ambacho ni kitabu kimoja. Kwa mwaka utasoma vitabu visivyopungua kumi. Nikuambie tu rafiki yangu, ukiweza kusoma vitabu 10 kwa mwaka na ukafanyia kazi yale uliyojifunza, huwezi kubaki hapo ulipo sasa.

Hapo chini nimekushirikisha vitabu 30 kwenye maeneo mbalimbali unayoweza kuwa umejiwekea malengo na nitashauri uchague vitabu 10 ambavyo utavisoma mwaka huu 2020 ili uweze kuyafikia malengo yote uliyojiwekea.

Pia nikukaribishe kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA, ambapo kwa mwaka mzima utapata vitabu pamoja na chambuzi zake, kujiunga na channel hii fungua; https://www.t.me/somavitabutanzania

CHAGUA VITABU 10 VYA KUSOMA 2020.

Rafiki, kupitia vitabu vingi ambavyo nimesoma, nimekuwa navigawa kwenye makundi mbalimbali.

Sasa kulingana na malengo yako ya mwaka 2020, nashauri uchague vitabu 10 kati ya hivi 30 nilivyoshirikisha hapa na usome kimoja kila mwezi pamoja na kufanyia kazi.

Yafuatayo ni makundi ya vitabu muhimu kwako kusoma, kulingana na malengo yako.

Kama ndiyo unaanza kabisa usomaji wa vitabu, basi anza na hivi;

 1. Think And Grow Rich.
 2. Rich Dad, Poor Dad.
 3. The Richest Man In Babylon.
 4. Elimu Ya Msingi Ya Fedha.

Kama umepanga kuanza au kukuza biashara yako 2020 basi hakikisha unasoma vitabu hivi;

 1. Biashara Ndani Ya Ajira.
 2. The Small Business Bible.
 3. The E-Myth Revisited
 4. The Great Game Of Business.
 5. The Psychology Of Selling
 6. Sell Or Be Sold

Kama unataka kujitofautisha kwenye kazi yako ili uwe bora na ulipwe zaidi basi soma vitabu hivi;

 1. So Good They Cant Ignore You
 2. Linchpin
 3. Lean In
 4. Rework

Kama unataka kutumia vizuri muda wako na kufanya makubwa soma vitabu hivi;

 1. 168 Hours
 2. 7 Habits Of Highly Effective People
 3. Getting Things Done
 4. Eat That Frog

Kama unataka kuwa na ushawishi zaidi na kuweka mikakati mbalimbali, basi soma vitabu hivi;

 1. Influence; The Psychology Of Persuation.
 2. The Art Of War
 3. 48 Laws Of Power
 4. How To Win Friends And Influence People

Kuboresha uneni na uandishi soma vitabu hivi;

 1. The Art Of Public Speaking
 2. How To Write A Copy That Sells

Kuboresha mahusiano yako soma vitabu hivi;

 1. 5 Languages Of Love
 2. Men From Mars And Women From Venus

Kuwa na afya bora pamoja na mtindo bora wa maisha soma vitabu hivi;

 1. Bulletproof Diet
 2. Own The Day, Own Your Life
 3. Bluezone
 4. The Longervity Project

Rafiki, vitabu vyote hivi nilivyokuorodheshea hapa vinapatikana kwa nakala tete (softcopy) kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA, ingia kwa kubonyeza hapa; https://www.t.me/somavitabutanzania

Vitabu ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na BIASHARA NDANI YA AJIRA vinapatikana kwa nakala ngumu. Kuvipata wasiliana na 0678 977 007 au 0752 977 170.

Rafiki yangu mpendwa, 2020 uliyokuwa unaisubiri kwa hamu ndiyo hii, 2020 uliyokuwa unajiambia kuna mambo mapya utafanya na ya zamani utaacha ndiyo tumeshaifikia. Sasa kazi ni kwako kuchukua hatua, usiwe mtu wa kupanga na kuacha.

Anza na lengo moja, lengo la kupata maarifa zaidi, lengo la kunoa bongo yako na hilo litakuwezesha kuyafikia malengo mengine uliyojiwekea. Karibu twende pamoja kwenye safari hii ya kujifunza kupitia usomaji wa vitabu, jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo ninachoweka hapa kisha bonyeza JOIN. Kiungo ni hiki; https://www.t.me/somavitabutanzania

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.t.me/somavitabutanzania