There are too many mediocre books which exist just to entertain your mind. Therefore, read only those books which are accepted without doubt as good. —LUCIUS ANNAEUS SENECA
Tuna muda mchache sana hapa duniani, lakini vitu vya kufanya ni vingi.
Ni muhimu sana kila mmoja wetu kujifunza kupitia usomaji wa vitabu, lakini vitabu vya kusoma ni vingi.
Je unachaguaje vitabu vipi usome?
Seneca anatuambia kuna vitabu vingi sana vya kawaida, ambavyo lengo lake ni kuburudisha akili yako.
Lakini unachohitaji wewe siyo burudani kwa akili,
Unachohitaji ni maarifa ambayo yataikuza akili yako na kukuwezesha kuwa bora, kufanya maamuzi bora na kupiga hatua kwenye maisha.
Hivyo unapaswa kuchagua vitabu bora vya kusoma, ambavyo vimekubalika na wale unaowaheshimu bila ya shaka yoyote kwamba ni vitabu bora kabisa.
Na hili ndiyo tunalokwenda kulifanya mwaka huu 2020, kujifunza kutoka vile vitabu bora kabisa, na siyo vitabu vya kuburudisha akili.
Kupitia tafakari za kila siku (ambapo sasa kutakuwa na tafakari ya asubuhi na ya usiku) tutapata nukuu kutoka kwa waandishi bora kabisa.
Pia kupitia channel ya SOMA VITABU TANZANIA, tutasoma na kuchambua vile vitabu ambavyo watu waliopiga hatua kubwa wanakiri vimekuwa msaada kwao na wanashauri wengine kuvisoma.
Tafakari za 2020 zitatoka kwenye kitabu cha A Calender Of Wisdom cha Loe Tolstoy (nitashurikisha makala ya maelezo zaidi kuhusu kitabu hiki)
Vitabu tutakavyosoma na kuchambua kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA ni vile vilivyopendekezwa zaidi kwenye mtandao wa MOST RECOMMENDED BOOKS (https://www.mostrecommendedbooks.com/)
Na kujiunga na channel ya SOMA VITABU TANZANIA, fungua http://www.t.me/somavitabutanzania
2020 siyo mwaka wa kupoteza kwenye vitabu vya kawaida au habari za udaku na nyinginezo.
2020 ni mwaka wa kupata maarifa bora kabisa, kuchukua hatua na kufanikiwa zaidi.
Karibu sana twende pamoja kwenye safari hii.
Heri ya mwaka mpya 2020, ukawe mwaka wa kupata hekima zaidi na kuchukua hatua bora kabisa na kupata mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Rafiki yako katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania