Normal
0
21
false
false
false
SW
X-NONE
X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,sans-serif;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-language:EN-US;}
Kama umeshangazwa na chochote kilichotokea kwenye maisha yako, kwa kujiambia kwamba hukutegemea kitokee, basi jua tatizo ni lako, hujafanya kazi yako sawasawa, hujawa na maandalizi ya kutosha.
Kila kitu kinaweza kutokea wakati wowote ule, hivyo kutegemea kisitokee haikizuii kitu kutokea.
Unapaswa kuifanya kazi yako sawasawa, kwa kujiandaa kwa matokeo yoyote yatakayopatikana.
Lazima ujue kwamba nguvu yako iko kwenye kile unachojua na hatua unazochukua, matokeo unayopata hayapo ndani ya uwezo wako. Hivyo haijalishi unataka kiasi gani matokeo unayotaka wewe ndiyo yatokee, dunia haifanyi kazi hivyo.
Kufanya kazi yako kwa usahihi ni kujua kila aina ya matokeo yanayoweza kutokea na kisha kujua ni hatua zipi utakazochukua kwa kila matokeo yanayoweza kupatikana.
Hivyo matokeo yoyote yanapokuja, hushangazwi nayo na kujiambia hukuyategemea, badala yake unarudi kwenye mpango wako, na kuona ni hatua zipi sahihi kwa matokeo uliyopata.
Kama umejitoa kweli kufanikiwa, usiache jambo lolote kwenye mikono ya bahati, badala yake fanya kazi yako, kuwa na maandalizi sahihi na chukua hatua sahihi kwa kila matokeo unayopata.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kila siku jiandae na matokeo yatakayo kuja kwako ,kila matokeo yana maana kwenye maisha yako
Asante sana kochq
LikeLike