Rafiki yangu mpendwa,

Kila kitu kwenye maisha yetu kinabadilika isipokuwa kitu kimoja pekee.

Kitu hicho ni mabadiliko, yaani mabadiliko yataendelea kutokea kwenye maisha, hakuna namna mabadiliko yatakoma.

Lakini sisi binadamu ni viumbe tusiopenda kabisa mafanikio, kwa asili huwa tunapenda vitu vibaki kama vilivyo.

Akili zetu huwa zinapenda sana hali ya uhakika, sasa kwa kuwa mabadiliko hayana uhakika, huwa hatuyapendi.

Lakini asili huwa haiangalii tunapenda au hatupendi nini, ingekuwa asili inatusikiliza, dunia ingeshapotea kabisa.

Hivyo asili inaendelea na mipango yake, mabadiliko yanaendelea kutokea, kama jua linavyochomoza na kuzama kila siku, iwe unataka jua siku hiyo au la.

Hivyo basi, njia pekee ya kukabiliana na mabadiliko haya ambayo lazima yatokee ni kuwa na maandalizi sahihi na kuyapokea mabadiliko hayo.

Hili ni gumu kusema, lakini utekelezaji wake ni mgumu, kwa sababu hakuna eneo ambalo tunafundishwa kuhusu mabadiliko.

Kwenye mfumo wa elimu tunafundishwa vitu vya nyuma, jinsi ambavyo vitu vimekuwa, kama vile havitakuja kubadilika.

Kwenye kazi na biashara tunafanya leo kile ambacho tulifanya jana kwa sababu tunajua matokeo yake. Hatupo tayari kufanya kitu kipya leo ili kuangalia matokeo gani tunapata.

Tunaendelea na mazoea mpaka pale yanapokuwa gharama kwetu.

NUFAIKA NA MABADILIKO

Mwaka 2015 niliandika kitabu kinachoitwa JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADIKIKO YANAYOTOKEA.

Hapa chini ni utangulizi wa kitabu hicho kama nilivyouandika mwaka 2015, bila ya kubadili neno lolote.

Utangulizi

Moja ya vitu ambavyo tunaweza kuwa na uhakika navyo kwenye maisha yetu ni mabadiliko. Mabadiliko ni kitu ambacho lazima kitokee. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema kwamba kila kitu kinabadilika isipokuwa mabadiliko yenyewe. Yaani ni lazima mabadiliko yatokee.

Kwa kujua hivi, je unajiandaaje na mabadiliko ambayo ni lazima yatatokea?

Je utanufaika na mabadiliko au utaachwa nyuma?

Hili ni swali la msingi sana ambalo unatakiwa kujiuliza ili kujua kama upo kwenye njia sahihi ya kukufikisha kule unakotaka kwenda.

Katika mabadiliko yoyote yanayotokea, yanazalisha makundi ya watu tofauti tofauti. Katika makundi hayo, kuna kundi ambalo linafaidika sana na kusonga mbele na kuna kundi ambalo linaachwa nyuma, linapoteza na kubaki katika wakati mgumu.

Lengo la kitabu hiki ni kukuandaa wewe na mabadiliko yanayoendelea kutokea kila siku. Kukufanya wewe usiachwe nyuma na ufaidike na mabadiliko haya.

Kisome kitabu hiki na yafanyie kazi yale unayojifunza na utakuwa katika nafasi nzuri ya kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com

22/03/2015

Rafiki, huo ndiyo utangulizi mfupi wa kitabu hiki cha mabadiliko.

Kama dunia, kwa sasa tunapitia hali ambayo italeta mabadiliko makubwa mno kwenye maisha ya kila mtu hapa duniani.

Mlipuko wa vizuri vya Korona unaoendelea sasa, utafika mwisho, lakini baada ya hapo, dunia itakuwa imezaliwa upya, hakuna chochote kitakachobaki kama kilivyokuwa awali.

Na hapa ndipo yatakapotengenezwa makundi matatu tunayojifunza kwenye kitabu hicho.

Kundi la kwanza ni wale wanaonufaika na mabadiliko, kwa kuyaona haraka na kuchukua hatua kabla wengine hawajayaona mabadiliko. Hapa ndipo unapopaswa kuwa wewe.

Kundi la pili ni wale ambao wanaolazimishwa kubadilika na mabadiliko. Hawa hawaoni mabadiliko haraka, ila yanapotokea wanakuwa hawana namna, wanalazimika kubadilika. Usikubali kuwa kwenye kundi hili, lakini unapojikita umechelewa, ni bora kuwa kwenye kundi hili kuliko kundi la tatu.

Kundi la tatu ni wale ambao wanaachwa nyuma na mabadiliko. Hawa ni wale ambao wanafikiri mambo yatarudi kama zamani, kwamba baada ya hili kila kitu kitarudi kama walivyozoea. Watu hawa wanasubiri lakini mambo hayarudi kama walivyozoea. Watu hawa ni wabishi au wavivu, hawataki kujifunza vitu vipya au kuchukua hatua za tofauti. Hivyo wanaachwa nyuma, kama ni kazi inaisha, kama ni biashara inakufa. Hakikisha kwa namna yoyote ile, huwi kwenye kundi hili, likatae haraka sana.

Hatua ya kuchukua leo kujiandaa na mabadiliko.

Rafiki yangu, ninachokusihi ufanye leo ni kusoma kitabu cha JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Kitabu kipo kwenye mfumo wa nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email. Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu 5, lakini kutokana na mabadiliko yanayoendelea na umuhimu wa wewe kukipata na ukisome, ninakupa kwa bei ya zawadi, utakipata kwa tsh elfu 3.

Kupata kitabu hiki, tuma tsh elfu 3 (3,000/=) kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na maelezo umelipia kitabu cha mabadiliko na utatumiwa kitabu hicho.

Usikubali kuachwa nyuma na mabadiliko, maarifa sahihi kwako yapo, jifunze na chukua hatua na baada ya hili, utajishukuru sana.

Zawadi ya vitabu nane vya mafanikio.

Rafiki, nikukumbushe pia kwamba zawadi ya vitabu nane nilivyotoa inaendelea na karibu itafika ukingoni.

Kwenye zawadi hii, unapata vitabu nane nilivyoandika, katika mfumo wa nakala tete kwa kulipa nusu ya bei pale unapochukua vitabu vyote.

Vitabu hivyo na bei zake za zawadi ni kama ifuatavyo;

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, bei ya zawadi elfu 3.
  2. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG, bei ya zawadi elfu 7.
  3. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA, bei ya zawadi elfu 3.
  4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, bei ya zawadi elfu 7.
  5. BIASHARA NDANI YA AJIRA, TOLEO LA KWANZA, bei ya zawadi elfu 7.
  6. MIMI NI MSHINDI, AHADI YANGU NA NAFSI YANGU, bei ya zawadi elfu 7.
  7. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING), bei ya zawadi elfu 3.
  8. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, bei ya zawadi elfu 3.

Ukichukua vitabu vyote nane kwa pamoja, unalipa tsh elfu 30 badala ya elfu 40 kama utachukua kimoja kimoja kwa bei ya zawadi.

Karibu sana upate zawadi hii, tuma fedha kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu au vitabu ulivyolipia kisha utatumiwa kwenye email yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania