“Try to live your life and be happy with your destiny, acquiring inner peace by love and good deeds.” —MARCUS AURELIUS

Njia pekee bora ya kuyaishi maisha yako ni kufurahia hatima ya maisha yako na kupata utulivu na amani ya ndani.
Na ili kupata hayo, unapaswa kuwa na upendo na matendo mema.
Huwa tunapoteza muda na nguvu nyingi kutafuta furaha nje yetu,
Tunaangalia nini wengine wanacho au wanafanya na kuonekana kuwa na furaha ili na sisi tufanye.
Cha kushangaza tunafanya, lakini hatuipati furaha, wala amani.
Hii ni kwa sababu tunakuwa tumekosa misingi sahihi ya furaha,
Ambayo ni upendo na matendo mema.

Anza na upendo, kwa kujipenda wewe mwenyewe, kuwapenda wengine na kupenda kile unachofanya.
Usijihangaishe na chochote usichokuwa na upendo nacho,
Haya maisha ni mafupi kwa kila mmoja wetu, yatumie vizuri kwa yale unayopenda. Usiipe chuki nafasi kwenye maisha yako.

Kisha kuwa na matendo mema,
Chochote unachokifanya, kifanye kwa uzuri na wema.
Fanya hivyo kwa sababu ndiyo sahihi na siyo kwa sababu unataka uonekane.
Kufanya kwa wema kunapaswa kuanzia ndani, na siyo nje.
Unapofanya kwa wema, unaridhika na kitendo hicho, hata kama hakuna anayeona au kukusifia.
Kuridhika kwako kunakupa furaha na amani ya ndani kuliko sifa unayoweza kupewa na yeyote.
Maisha ni mafupi, tusiyapoteze kuwa kufanya mambo mabaya au yasiyo na mchango wowote kwa wengine.

Ni UPENDO NA WEMA, vitakavyokupa FURAHA NA AMANI.
Vyote hivi vipo ndani ya uwezo wako, hapo ulipo sasa, chukua hatua leo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania