Rafiki yangu mpendwa,
Kila siku huwa tunasikia hadithi za watu ambao wameweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao licha ya kuanzia chini kabisa.
Ni hadithi zinazotia moyo na kutupa hamasa ya kuchukua hatua zaidi ili kufanikiwa.
Lakini wengi ambao wamekuwa wanachukua hatua kupitia hadithi hizo, wamekuwa hawapati mafanikio makubwa kama yale ambayo wameyaona kwa wengine.
Hivyo wengi hufikiri hadithi hizo siyo sahihi au wao hawana bahati ambayo watu wengine wameipata.
Lakini hayo siyo sahihi, kama umesikia hadithi ya mtu mwingine aliyefanikiwa na ukafanyia kazi yale uliyojifunza lakini hujafanikiwa, tatizo siyo hadithi, wala tatizo siyo aliyekupa hadithi, bali tatizo ni wewe.

Bila ya kukiri tatizo ni wewe na kuchukua hatua sahihi, hutaweza kufanikiwa.
Leo utakwenda kujifunza ni jinsi gani wewe umekuwa tatizo kwako kufanikiwa kupitia hadithi za wengine waliofanikiwa.
1. Husikilizi hadithi kwa ukamilifu na kuihoji kwa kina.
Unachoondoka nacho kwenye hadithi ni kwamba mtu alianzia chini na sasa yuko juu kabisa. Unapata hamasa kwamba na wewe unaweza kuanzia chini na kufika juu kabisa.
Kwenye kila hadithi ya mafanikio, kuna vitu huwa havisemwi, na hata vikisemwa, havipewi uzito ambao vinastahili.
Hivyo ni wajibu wako kutafuta na kujua vitu hivyo, kuputia kusikiliza hadithi kwa ukamilifu na kuhoji mambo mbalimbali.
Hii inakufanya uwe na uelewa, ujue wapi unaanzia na nini cha kutegemea kwa hatua unazokwenda kuchukua.
2. Unaiga kila kitu kwenye hadithi.
Kwa sababu mtu mwingine amefanikiwa kwenye kitu fulani, haimaanishi na wewe utafanikiwa kwenye kitu hicho.
Sisi binadamu tunatofautiana, na hitaji la kwanza kwenye mafanikio ni mtu kupenda kile unachokifanya.
Wenzako anaweza kufanikiwa kwenye kilimo kwa sababu ndiyo kitu anachopenda, yuko tayari kufanya kwa muda mrefu hata kama hakimlipi mwanzoni. Lakini wewe unapoingia kwa kuangalia faida tu, hutachukua muda, maana hutaipata faida, huku pia ukiwa hupendi kilimo hicho.
Hivyo unaposikiliza hadithi za mafanikio, usitake kufanya kile ambacho aliyefanikiwa kafanya, badala yake jifunze misingi iliyomfanya afanikiwe, na kisha itumie misingi hiyo kwenye kile ambacho unafanya wewe, kile ambacho unapenda kweli kukifanya.
Chochote kile ambacho unapenda kufanya, kile ambacho uko tayari kufanya hata kama hakuna anayekulipa, hicho ndiyo kitakachokufikisha kwenye mafanikio makubwa. Jifunze misingi sahihi ya mafanikio kutoka kwa waliofanikiwa na itumie kwenye kile unachopenda kufanya na siyo kuiga wanachofanya wao.
3. Hujajiandaa kwa magumu na changamoto zinazokusubiri.
Kwenye hadithi za mafanikio, msisitizo huwa unawekwa maeneo mawili, chini kabisa ambapo mtu ameanzia na juu kabisa ambapo mtu amefika. Kitu ambacho huoneshwi ni magumu ambayo mtu huyo alipotia. Japo atakuambia nilipitia magumu na sikukata tamaa, kuna tofauti ya kuambiwa na kushuhudia au kupitia hali yenyewe.
Sisi binadamu huwa tunasahau haraka, na hata kwenye hadithi za mafanikio, huwa tunakumbuka na kueleza vile vitu ambavyo ni vizuri kwa watu kusikia. Lakini hutasikia kwenye hadithi za mafanikio mtu akieleza kwa kina magumu aliyopitia, siku ambazo hakupata usingizi usiku, mambo mengi aliyokata tamaa kabisa mpaka hatua za mwisho ndiyo akajaribu tena.
Chochote unachofanya ili kufanikiwa, jua kuna magumu na changamoto kubwa zinazokusubiri mbele yako. Na jua kabisa huwezi kukadiri ukubwa wake, ila jua katika watu 100 ambao watakutana na changamoto hizo, ni mmoja pekee anayeweza kuzivuka, na mmoja huyo anapaswa kuwa wewe.
Lazima uweke agano la kufa na kupona, kwamba utapata unachotaka au utakufa ukikitafuta, hakuna mbadala wa hilo. bila ya agano la aina hii, hutaweza kufika mbali, magumu na changamoto zinazokusubiri vitakuondoa haraka sana.
4. Unategemea mambo yatokee haraka.
Kitu kingine ambacho hakioneshwi sana kwenye hadithi za mafanikio ni muda. Kuna muda uliojichimbia kabla hata mtu hajaanza safari ya mafanikio, ambao umekuja kuchangia kwenye mafanikio yake lakini umekuwa hauhesabiwi.
Yeyote aliyefanikiwa, kuna uwekezaji mkubwa wa muda ambao ameufanya tangu zamani, ambao umechangia kwenye mafanikio yake. Labda mtu amekulia kwenye familia ambayo imekuwa inafanya biashara na watoto wote wanafanya kazi kwenye biashara hizo. Hivyo tangu mdogo anajihusisha na biashara na kuna misingi fulani anajifunza. Anapokuja kuanzisha biashara baadaye, anafanikiwa haraka.
Sasa wewe ambaye hujawahi hata kuuza kibanda, unataka uanzishe biashara na ufanikiwe haraka kama mwenzako aliyeanza kuijua biashara tangu mdogo. Unajidanganya. Na hili ndiyo linapoteza wengi mno. Tena tukiangalia kwenye mfano huu wa biashara, kila mtu ambaye hayupo kwenye biashara ukimuuliza kwa nini atakujibu moja kati ya haya mawili; sina mtaji au sijapata wazo zuri. Hakuna hata mmoja atakayekujibu hana uzoefu, na kinachoua biashara siyo mtaji wala wazo, bali uzoefu.
Unahitaji kujijengea uzoefu wa kutosha kabla hujafanikiwa kwenye jambo lolote unalofanya. Hivyo usijidanganye kwa mafanikio ya haraka, jipe muda wakujenga uzoefu utakaokusaidia kufanikiwa.
5. Unapenda sana maonesho.
Umepata wazo la biashara hata bado hujaianzisha unakimbilia kuposti mitandaoni kwamba tayari wewe ni mfanyabiashara, watu wasubiri mambo yako makubwa. Umepanda mazao hata hayajazaa umeshapiga picha na kuweka mitandaoni, watu wasubiri mambo makubwa.
Tunaishi kwenye zama ambazo watu wanaweka nguvu nyingi kwenye maonesho badala ya kuweka nguvu kwenye kufanya kazi halisi na itakayoleta matokeo sahihi.
Hakuna aliyefikia mafanikio makubwa kwenye maisha kwa kuanza maonesho mapema. Wengi walijichimbia na kusahaulika kabisa, kisha kuja kuibuka wakiwa wamefanikiwa.
Kama biashara au kazi yako haihusishi mitandao kupata wateja, kaa mbali na mitandao na weka kazi kwenye kuikuza biashara au kazi yako.
Njia sahihi ya kunufaika na hadithi za mafanikio.
Rafiki yangu mpendwa, ili unufaike na hadithi mbali mbali za mafanikio unazozipata kutoka kwa wengine, unahitaji kuwa kwenye mazingira sahihi.
Mazingira ambayo unazungukwa na wale waliofanikiwa au wanaokazana kufanikiwa.
Mazingira ambayo yanakupa subira kwenye kile unachofanya.
Mazingira ambayo yanakuzuia usikate tamaa, hata pale mambo yanapokuwa magumu kweli kweli.
Mazingira yanayokupa wewe uhuru wa kufanya kile unachotaka kufanya kwenye maisha yako.
Jamii zetu zimekosa sana mazingira haya na ndiyo maana wengi wanazidi kushindwa licha ya hadithi za mafanikio kuwa nyingi na kila mtu kuweza kuzijua.
Kujua pekee hakutoshi, unahitaji mazingira sahihi katika kuchukua hatua kwenye yale uliyojifunza ili uweze kunufaika.
Mazingira hayo sahihi unayapata kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kuwa kwenye KISIMA, unapata mafunzo, msingi, mwongozo na hamasa sahihi ya kuchukua hatua kwenye maisha yako ili upate mafanikio makubwa kwa chochote unachochagua kufanya. Ndani ya KISIMA, unachagua kuyaishi maisha yako na siyo kuiga maisha ya wengine.
Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo, ili na wewe uweze kutengeneza hadithi ya mafanikio yako, hadithi ambayo itakuwa msaada kwa wengine ambao wanaanzia kwenye mazingira magumu na yenye changamoto kama unayoanzia wewe.
Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.
KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.
KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.
Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;
1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.
2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)
3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.
5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.
6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.
7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.
8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.
9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.
10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.
Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.
Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.
Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.
Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.
Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania