Rafiki yangu mpendwa,
Njia rahisi ya kujipima kama kweli uko kwenye njia itakayokufikisha kwenye mafanikio makubwa siku za mbeleni ni kujua umuhimu wako kwa wengine. Kujua wengine wanakuchukulia kwa umuhimu kiasi gani. Kujua unahitajika na wengine kiasi gani.
Na njia rahisi ya kupima umuhimu wako kwa wengine ni kujiuliza kama ukiacha kufanya kile unachofanya, je kuna mtu atakayejua umeacha? Je kuna atakayeathirika kwa wewe kuacha? Kwa lugha nyingine ni kama haupo, je kuna ambao watakuulizia?
Kama jibu ni ndiyo, kwamba kuna watakaokukosa, watakaoathirika na kutokuwepo kwako, basi unafanya kitu cha tofauti, kitu kikubwa na chenye mchango kwa wengine. Na hicho ni kiashiria kwamba utakwenda kufanikiwa sana.
Lakini kama jibu ni hapana, kama watu hawatakukosa, kama hakuna atakayeathirika na kutokuwepo kwako wala atakayekuulizia, basi jua wazi kwamba hakuna kikubwa unachofanya na huna mchango wa kipekee kwa wengine. Hicho ni kiashiria kwamba mafanikio makubwa yatakuwa magumu kwako kufikia.
Mtu mmoja amewahi kusema kama kuna watu wawili, ambao wako eneo moja na wanafanya kitu kimoja kwa kufanana, basi mmoja kati ya hao wawili siyo muhimu. Hii ni kweli, iwe ni kwenye kazi au biashara, kama huna cha kukutofautisha na wengine, huna namna unaweza kufanikiwa zaidi.
Kama unafanya biashara na siku ukifunga wateja hawakosi chochote badala yake wanaenda kwa wafanyabiashara wengine na maisha yao yanaendelea kama kawaida, huna umuhimu kwao na safari yako ya mafanikio ni ngumu.
Kama unafanya kazi na kipindi unachokuwa likizo watu hawakukosi au kukuulizia au baadhi ya vitu kutokwenda vizuri basi jua huna utofauti na umuhimu kwenye kazi hiyo.
Unawezaje kujijengea utofauti ambao utakufikisha kwenye mafanikio?
Swali ambalo wengi huwa wanajiuliza ni hilo, kwamba wanataka kujijengea utofauti ili waweze kufanikiwa, lakini hawajui jinsi ya kufanya hivyo.
Jibu la swali hili limejibiwa na Naval kwenye makala niliyokushirikisha ya jinsi ya kuwa tajiri bila kutegemea bahati.
Naval anasema;
“Jijengee ujuzi mahsusi, uwajibikaji na nyenzo.
Ujuzi mahsusi ni ule ambao hakuna anayeweza kukufundisha.
Kama jamii inaweza kukufundisha kitu, basi pia inaweza kumfundisha mtu mwingine na akachukua nafasi yako.
Ujuzi mahsusi hupatikana kwa kujua kusudi lako, kile unachopenda na unachokidadisi sana badala ya kuhangaika na fursa mpya kila wakati.
Kujenga ujuzi mahsusi kwako itakuwa kama mchezo, wakati kwa wengine itakuwa ni kazi ngumu.”
Maelezo ya Naval kwenye hilo yamejitosheleza sana, hapa nitakwenda kukupa ufafanuzi kwenye baadhi ya maeneo ili ujue hatua sahihi kwako kuchukua uweze kufanikiwa.
Kwanza kabisa kujitofautisha na wengine na ili uweze kuuliziwa unapokuwa haupo unapaswa kujijengea ujuzi mahsusi. Huu ni ujuzi ambao hakuna yeyote anayeweza kukufundisha, ni ujuzi unaoanzia ndani yako, na kwa sababu kila binadamu ni tofauti, ukiweza kujua kile kilicho tofauti kwako na kukitumia kwenye kazi au biashara yako, kitakutofautisha sana.
Pili usitegemee kuwa tofauti kupitia kile ulichojifunza shuleni. Chochote ambacho jamii inaweza kukufundisha, inaweza kuwafundisha wengine pia na hivyo watakuwa tayari kuchukua nafasi yako. Ukishajifunza shuleni au kwenye jamii jinsi ya kufanya kazi au biashara yako, weka utofauti na upekee wako kwenye kazi unayofanya na hilo litakufanya uzalishe matokeo ya tofauti na watu wakutegemee.
Tatu ujuzi mahsusi unatokana na kusudi ambalo liko ndani yako, ni matokeo ya vipaji ulivyonavyo. Hakuna anayeweza kukuambia unachoweza kufanya kwa sababu hajui unaweza kufanya nini. Bali wewe mwenyewe ndiye unayejua ndani yako ni nini unapenda kufanya, kitu gani huwezi kuvumilia kinapokuwa siyo sawa na nini unachopenda kudadisi na kuboresha zaidi. Kwa kujua kusudi lako na kulifanyia kazi, chochote utakachokifanya, kitakuwa tofauti kabisa na wengine wanavyofanya, na hapo watu watakutegemea kwa utofauti wanaoupata kwako.
Nne ujuzi mahsusi hautakuwa kazi kwako. Wakati wengine watakuwa wanaona mateso kufanya kitu fulani, wewe kwako itakuwa kama mchezo tu. Inakuwa ni kitu unachopenda sana kukifanya, uko tayari hata kukifanya bure kwa sababu unaridhika sana pale unapokifanya na tena unapokifanya kwa ubora.
Kwa kujumuisha, njia pekee ya kuwa tofauti kwenye kile unachofanya, ili wengine wakutegemee na uweze kupata mafanikio makubwa ni kuweka utu wako kwenye kile unachofanya.
Chochote unachofanya, acha kufanya kwa mazoea, acha kufanya kama wengine wanavyofanya na anza kukifanya kama wewe, kwa namna ya kipekee, ambayo wengine hawawezi kufanya.
Na hili halihitaji maigizo, wala kutumia nguvu sana. Ukijiona inabidi utumie nguvu kubwa au ufanye kwa maigizo jua unachofanya siyo sahihi. Maji hayatumii nguvu yanapotiririka kutoka sehemu ya juu kwenda sehemu ya chini, yanatiririka tu lakini ndani yake yanakuwa yamebeba nguvu kubwa. Hivyo pia ndivyo unavyopaswa kuwa, usitumie nguvu wala maigizo, bali kuwa wewe na fanya kwa upekee ulio ndani yako.
Karibu kwenye mazingira yatakayokuwezesha kuwa wa kipekee.
Rafiki yangu mpendwa, jamii ina vita na wewe. Jamii haitaki uwe tofauti, kwa sababu inajua ukiwa tofauti utakuwa ghali, utategemewa na wengi na hilo litawafanya wasioweza kuwa tofauti kama wewe kushindwa kufanikiwa kama wewe.
Kama unabisha hilo angalia pale ulipoenda kuanza kitu kipya mahali na wale uliowakuta walikupokeaje. Labda ulianza ajira mpya, ukaenda ukiwa na shauku kubwa ya kufanya vitu kwa tofauti. Lakini ulipokutana na wakongwe kwenye kazi hiyo wakakuambia tulia, mambo huwa hayaendi hivyo. Wanakuingiza kwenye mazoea yao na hapo unakuwa kama wao, unaacha kuwa hatari kwao. Wanajua wakikuacha uwe tofauti, wao watakosa maana, hivyo hawataruhusu hilo litokee.
Kadhalika kwenye biashara, nenda kaanzishe biashara mahali na panga kufanya kwa utofauti. Wale waliopo kwenye biashara hiyo watakuwa wa kwanza kukukatisha tamaa. Watakuambia unajisumbua, wateja wenyewe hawajali, unapoteza nguvu bure na maneno mengine kama hayo.
Japo nimekuambia kwenye kufanya kilicho tofauti kwako huhitaji nguvu wala maigizo, unahitaji nguvu za ziada kukabiliana na jamii inayokuzunguka, ambayo inakuzuia usiwe tofauti.
Peke yako huwezi kukabiliana na kundi kubwa linalokuzunguka, hivyo unahitaji kuwa kwenye mazingira yanayokupa nguvu ya kupuuza wale wote wanaokuzuia usiwe tofauti.
Mazingira hayo ni KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kuwa kwenye KISIMA, unapanga hatua zipi kubwa unazokwenda kupiga kwa miaka kumi ijayo na ni nini utafanya kufikia hatua hizo. Utaeleza ni maeneo yapi unataka kubobea zaidi kwenye maisha yako. Na pia kwenye kila mwaka wa mafanikio, utaeleza lipi lengo lako kuu unalifanyia kazi.
Hilo litakupa wewe nafasi ya kujitofautisha na wengine, utatambua vipaji na kusudi lako na kuweza kuvihusisha kwenye kazi au biashara unayofanya.
Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA unazungukwa na watu wengine ambao pia wameshachagua nini wanataka na wanajituma kuhakikisha wanapata kile wanachotaka. Watu hao wanakuwa wameshashinda upinzani wa jamii na kuchagua kuyaishi maisha yako. kwa kuzungukwa na watu wa aina hii, utapata nguvu ya kuishinda jamii inayokuzunguka. Maana jamii itakapokuambia hakuna anayefanya tofauti, wewe unajua wapo wanaofanya tofauti, kwa sababu wamekuzunguka kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajichelewesha sana kufikia mafanikio makubwa. Unajiweka kwenye hatari ya kuendelea kurudishwa nyuma na jamii inayokuzunguka, ambayo inakutaka uwe kawaida ili usiwe hatari kwa wengine.
Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili upate nafasi ya kuchagua kusudi kuu la maisha yako na ambalo utaliishi na kulifanyia kazi kila siku, huku ukipata nafasi ya kuzungukwa na wengine ambao pia wanayaishi makusudi yao kitu ambacho kitakuzuia usikatishwe tamaa na wale walioshindwa, ambao ni wengi kwenye jamii zetu.
Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.
KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.
KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.
Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;
- Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.
- Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)
- Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
- Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.
- Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.
- Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.
- Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.
- Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.
- Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.
- Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.
Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.
Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.
Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.
Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.
Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania