Mambo mengi, muda mchache… hii ni kauli ambayo ni maarufu kwenye zama hizi, kutokana na ukomo wa muda tulionao, huku mambo ya kufanya yakiongezeka kila siku.

Lakini wenye akili na hekima kubwa waliotutangulia, waliuangalia muda kwa namna ya tofauti. Mmoja wa watu hao alikuwa mwanafalsafa wa Ustoa aliyeitwa Seneca.

Yeye alisema tatizo la muda siyo kwamba tuna uhaba nao, bali tunao mwingi kiasi kwamba tunaamua kuuchezea na kuupoteza.

Sasa ukinipa mimi kazi ya kuchagua kumsikiliza mtu wa sasa aliyevurugwa na mwanafalsafa wa kale aliyekaa na kuyatafakari mambo, nitamsikiliza mwanafalsafa wa kale.

Na kwa hili la muda, nimekuwa namsikiliza Seneca, na kufanya yale aliyoshauri kwenye muda na nimekuwa napata muda mwingi zaidi wa kufanya yale yenye manufaa.

Baada ya mimi kunufaika na kufanyia kazi maarifa hayo ya wanafalsafa, niliona siyo vibaya kukushirikisha na wewe pia, maana haitanipunguzia chochote kama na wewe utakuwa na muda mwingi kama nilionao mimi.

Hivyo nilikuandikia kitabu cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU. Wengi waliposikia jina hilo la kitabu walishangazwa, unawezaje kupata masaa mawili ya ziada kwenye siku wakati kila mtu ana masaa 24 pekee?

Na hapo ndipo nilipowakaribisha wajionee wenyewe muda mwingi ambao wamekuwa wanaupoteza kwenye mambo yasiyo na tija, ambao wakiuokoa, wanaweza kupata angalau masaa mawili ya ziada kila siku.

Jambo jingine linalowatatiza watu kwenye muda ni ukishapata masaa hayo mawili unayafanyia nini. Maana kuna watu wamepunguza majukumu yao, labda kwa kutafuta wasaidizi, lakini muda waliookoa wanaishia kuupoteza kwenye mambo yasiyo na tija.

Kwenye kitabu cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA, nimekupa mwongozo pia wa jinsi ya kutumia muda huo wa ziada unaouokoa kwenye siku yako.

Ninachotaka kukuambia leo rafiki yangu ni hiki, kama umewahi kulalamikia muda, kama umekuwa unapanga mambo ya kufanya lakini hupati muda wa kuyafanya, basi jua tatizo siyo muda, bali tatizo ni wewe.

Na hatua ya kwanza kwako kuchukua ni kusoma kitabu cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

Na kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, nikijua ukiwa na muda zaidi maisha yako yatakuwa bora na lengo la kazi yangu litakuwa limekamilika, leo nakupa zawadi ya kitabu hicho.

Kwa siku ya leo tu, yaani tarehe 18/09/2020 utaweza kukipata kitabu hiki cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA kwa tsh elfu moja tu, badala ya bei yake ya kawaida ambayo ni elfu 4.

Ninachotaka ni wewe rafiki yangu usome kitabu hiki, halafu uchukue hatua na maisha yako yawe bora. Ndiyo maana sisiti kukupa kitabu hiki kama zawadi kwa bei sawa na bure kabisa.

Kupata zawadi hii ya kitabu, ingia kwenye SOMA VITABU APP, njia mpya na bora kabisa ya kusoma vitabu kwa mfumo wa nakala tete, kisha nunua kitabu hicho kwa tsh 1,000/= na uanze kukomboa muda wako leo.

Kupakua app, fungua kiungo hiki; http://bit.ly/somavitabuapp kupata maelezo ya jinsi ya kuiweka na kuitumia app, fungua kiungo hiki; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/somavitabuapp/

Rafiki, zawadi hii nzuri kwako ni ya siku hii moja tu, sitaki uikose, changamkia nguvu hii ya buku ili uweze kudhibiti muda wako na ufanye makubwa zaidi ya unavyofanya sasa.

Kumbuka, muda unao wa kutosha, ila kwa namna unavyoutumia ndiyo imekuwa kikwazo kwako. Soma leo kitabu cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA na utaweza kuwa na muda zaidi.

Chukua hatua sasa kabla zawadi haijaisha, fungua hapa; http://bit.ly/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania