“Kuna njia mbili tu za kuyaishi maisha yako…”, alinukuliwa Albert Einstein, “… moja ni kama vile hakuna miujiza na nyingine ni kama vile kila kitu ni miujiza.”

Nimekuwa nayaishi maisha yangu kwa namna ya pili kabla hata sijasikia kutoka kwa Einstein, lakini baada ya kusikia kutoka kwake, niliamua kuzidisha hiyo miujiza na hivyo kuchukulia kila ninachoishi, kufanya au kukutana nacho kuwa muujiza.

Na hilo likapelekea mimi kuweza kufanya mambo mengi ambayo awali niliona siwezi kufanya.

Ninachotaka kukuambia leo rafiki yangu ni hiki, hata wewe unaweza kufanya miujiza mikubwa kwenye maisha yako, kama utachagua kuchukulia kila kinachoendelea kwenye maisha yako kama miujiza.

Na uzuri ni kwamba nimekuandalia kitabu kitakachokupa mwongozo wa NGUVU KUBWA YA MIUJIZA iliyo ndani yako na jinsi unavyoweza kuitumia kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Ukweli ni kwamba, kila mtu ana uwezo mkubwa kuliko ule anaoutumia sasa. Na hiyo iko hivyo kwa sababu wengi hawajui kama tayari wana uwezo mkubwa. Kwa kukipata na kukisoma kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, utaweza kujijua vizuri wewe mwenyewe na kisha kufanya makubwa.

Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA pamoja na kingine cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA vitazinduliwa rasmi siku ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020.

Semina hiyo ya kukutana ana kwa ana itafanyika jumapili ya tarehe 15/11/2020 jijini Dar Es Salaam. Semina hii inatupa nafasi ya kukutana pamoja watu wote wenye kiu ya mafanikio makubwa na wanaochukua hatua ili kufanikiwa zaidi.

Kupitia semina hii unapata nafasi ya kujifunza na kuhamasika, kitu kinachokupa msukumo wa kufanya zaidi ya unavyofanya sasa.

Ukizingatia yote ambayo tumekutana nayo mwaka 2020, ni muhimu sana kukutana pamoja na kuweka mikakati ya kwenda kufanyia kazi mwaka mzima.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, upate uzinduzi wa vitabu vipya viwili nilivyoandika mwaka huu 2020 pamoja na kupata mafunzo mengine na hamasa kutoka kwa wengine wengi.

KWA NINI HUPASWI KUKOSA SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020.

Rafiki yangu mpendwa, kama utachagua kukosa semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020, utakuwa umechagua kukosa mengi. Yafuatayo ni baadhi ya mengi utakayojifunza kwenye semina ya mwaka huu 2020;

1. JINSI YA KUONDOKA KWENYE HALI YA UCHOVU NA KUKOSA HAMASA (BURNOUT)

Kwa yale yaliyotokea mwaka huu 2020, kila mtu amechoka kupitiliza, hamasa kwa wengi imeshuka mno. Ule msukumo wa kufanya makubwa umepungua na kupotea kabisa kwa wengi.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 tunakwenda kujifunza jinsi ya kuondoka kwenye hali ya uchovu na kukosa hamasa, inayojulikana kwa Kiingereza kama burnout. Utajifunza mbinu ambazo zitakuwezesha kuendelea kujisukuma bila ya kujali nini kinaendelea kwenye maisha yako au duniani.

2. MPANGO WA MUONGO WA 2020 – 2030

Watu wamekuwa wanadanganywa kuna njia ya mkato ya kufanikiwa, wanajaribu kila njia na kujikuta wamerudi pale pale. Wengine wamekuwa wanakimbizana na kila fursa inayojitokeza mbele yao, lakini mwisho wa siku wanajikuta hawajapiga hatua yoyote.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 utajifunza jinsi ya kuweka mpango utakaoufanyia kazi kwa muongo (miaka kumi) mzima wa 2020 – 2030. Utatoka kwenye semina ukiwa umeshaamua unakwenda kupambana na nini na kuachana na usumbufu mwingine wowote.

3. LENGO KUU LA MWAKA WA MAFANIKIO 2020/2021

Wakati watu wa kawaida wakianza mwaka mpya tarehe moja ya mwezi wa kwanza kwenye mwaka husika, sisi wanamafanikio huwa tunauanza mwaka mapema kabisa, wiki nane kabla ya watu wa kawaida.

Mwaka wetu wa mafanikio huwa unaanza wiki ya kwanza ya mwezi Novemba na kumalizika wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba mwaka unaofuata. Kwa kuanza mwaka wa mafanikio mapema, tunakuwa mbele zaidi na hatuanguki kwenye mkumbo wa wale wanaoweka malengo kwenye mwaka mpya kwa sababu kila mtu anaweka malengo.

Semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 itakuwa ni ufunguzi wa mwaka wetu wa mafanikio 2020/2021 hivyo pia utapata nafasi ya kuweka na kushirikisha malengo yako ya kimafanikio kwa mwaka huo wa mafanikio. Usikose semina hii ili uweze kuuanza mwaka 2021 mapema kabisa, mpaka wengine wanapokuja kuamka, wewe umeshafanya makubwa.

4. MWONGOZO WA MWAKA WA MAFANIKIO 2020/2021

Kila mwaka wa mafanikio huwa tuna kitu kinatuongoza kwa mwaka mzima. Kitu hicho ndiyo kinapima kila kipaumbele na mengine yote yasiyoingia kwenye mwongozo huo yanakaa pembeni.

Mwaka huu wa mafanikio 2019/2020 tunaoumaliza mwongozo ulikuwa KIPATO ZAIDI 2020, ambapo mpango ni kuongeza kipato kwa asilimia 20. Kwa mwaka mzima tumefanyia kazi mwongozo huo na watu wameweza kufanya makubwa, licha ya changamoto zilizoukumba mwaka huu.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 utakwenda kujifunza na kuondoka na mwongozo wa kufanyia kazi mwaka 2020/2021 ambao utakuwezesha kufanya makubwa kwenye mwaka huo.

5. SHUHUDA ZA WANAMAFANIKIO

Sehemu nzuri kabisa ya mkutano wa KISIMA CHA MAARIFA ni shuhuda zinazotolewa na wanamafanikio mbalimbali. Unajionea wazi jinsi ambavyo watu wanapiga hatua na kufanya makubwa, bila ya kukubali sababu zozote kuwarudisha nyuma.

Unapotoka kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA unakuwa na nguvu, msukumo na hamasa kubwa ya kwenda kufanya makubwa pia.

Kwenye semina ya mwaka huu 2020 kuna shuhuda kubwa na nzuri kutoka kwa wanamafanikio ambao wameweza kupambana licha ya ugumu tuliopitia na hizo zitakuondolea kila sababu unayojipa kama kikwazo cha mafanikio yako.

6. KUWEKA MIKAKATI NA NJIA ZA KUJIFUATILIA 2020/2021

Kuweka malengo ni rahisi, kupanga mipango ni rahisi pia, lakini inapokuja kwenye utekelezaji, hapo ndipo wengi wanapokwama.

Wengi wamekuwa wanalalamika kwamba wakihudhuria mikutano au semina mbalimbali wanatoka wakiwa na hamasa, lakini siku chache baadaye hamasa ile inakuwa imepoa na wanarudi kwenye mazoea yao.

Semina za KISIMA CHA MAARIFA ni tofauti kabisa, kwani hizi zina njia ya kukupa hamasa kwa mwaka mzima tangu uliposhiriki semina. Kwenye semina hizi huwa natoa nafasi chache na adimu za programu ya ukocha ambapo nakufuatilia kwa karibu kutekeleza yale uliyojipangia. Na unapokuwa kwenye programu hizo, sikuachii kirahisi.

Karibu ushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 na upate nafasi ya kuwa na hamasa ya kufanya makubwa kwa mwaka mzima, kwa kuwa chini ya ufuatiliaji wa karibu wa kocha.

7. UZINDUZI WA VITABU VIWILI; NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA NA ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Kila mwaka kwenye semina hizi huwa nazidua vitabu vipya vya mafanikio, mwaka jana ilikuwa kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 nitakwenda kuzindua vitabu viwili muhimu mno kwenye zama tunazoishi na yale yanayokuja mbele yetu. Vitabu hivyo ni UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA na ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA. Watu wamekuwa hawajui nguvu kubwa iliyo ndani yao ya kuwawezesha kufanya makubwa, kitabu hicho kitakuonesha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa. Pia kitabu cha elimu ya msingi ya biashara kinakupa mafunzo muhimu ya kuanzisha na kukuza biashara yako. Usikose semina hii, kwani ndiyo sehemu pekee utakapoweza kupata nakala zilizosainiwa za vitabu hivyo.

8. NA MENGINE MENGI.

Watu mnapokutana, kuna mengi sana ambayo huwa yanatokea, mengi huwezi kuyaelezea. Kila mwaka ninapoandaa semina hizi, hutokea watu wapya ambao hawajawahi kushiriki na wapo njia panda, iwapo washiriki au la. Mimi huwa nawaambia washiriki kama jaribio, na kama semina haitakuwa na manufaa kwao, basi wanaweza kudai gharama walizolipa.

Mtu mmoja niliyewahi kumwambia hivyo, siku ya semina, kabla hata haijaisha alinifuata na kuniambia kwa nini usiwe unaandaa semina hizi mara mbili kwa mwaka? Aliona thamani kubwa ambayo hakutegemea, na ilimsaidia sana.

Usikose SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020 ambapo tunakwenda kujifunza mengi na kuondoka na nguvu na hamasa ya kufanya makubwa 2020/2021.

UTARATIBU WA SEMINA.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dar es salaam, kwenye moja ya hotel, taarifa zaidi utazipata baada ya kuamua kushiriki.

LINI; Jumapili ya tarehe 15 mwezi Novemba 2020, semina ni ya siku nzima, kuanzia saa moja kamili asubuhi mpaka saa moja kamili usiku.

ADA; Gharama za kushiriki semina hii ni tsh 200,000 (laki mbili) ambayo itagharamia kila kitu kwa siku ya semina pamoja na kuwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima ukipata mafunzo kila siku.

KUSHIRIKI; Ili kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 unapaswa kutoa taarifa mapema (leo hii) kwa kutuma ujumbe wenye majina yako kamili na namna ya simu na kueleza NITASHIRIKI SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020. Ujumbe unautuma kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253.

MALIPO; Malipo ya ada ya kushiriki semina yanafanywa kwa njia ya MPESA 0755 953 887 au tigo pesa/ airtel money kwenda namba 0717 396 253 majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo, tuma ujumbe ukieleza umelipia SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020. Unaweza kufanya malipo kidogo kidogo.

MWISHO WA MALIPO; Tarehe ya mwisho kufanya malipo ni 10/11/2020.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, karibu tupate nafasi ya kuuanza pamoja mwaka mpya wa mafanikio, tutoke tukiwa na nguvu na hamasa ya kwenda kufanya makubwa ili tufanikiwe zaidi.

Chukua hatua sasa ili ujihakikishie nafasi ya kushiriki semina hii, tuma ujumbe wa kushiriki kwa wasap namba 0717396253.

Naamini tutakuwa pamoja kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, karibu sana.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania