“Only misconceptions need to be supported by elaborate arguments. Truth can always stand alone.” – Leo Tolstoy

Ukweli hauhitaji kelele nyingi, una nguvu ya kusimama wenyewe.
Lakini uongo unahitaji kelele nyingi za kulazimisha ukubalike.
Uongo unahitaji maelezo mengi ili kuwashawishi watu waukubali.
Na uongo huwa unalazimisha watu waamini, tena bila ya kuhoji.

Ukweli huwa haujitetei na wala haumlazimishi mtu yeyote kukubaliana nao
Ukweli huwa unasimama kama ukweli, na hata kama watu wataukataa, hauachi kuwa ukweli.

Mwisho wa siku ukweli hudhihirika, bila ya kupiga kelele au kulazimisha kukubalika.
Mara zote simama kwenye ukweli, ndiyo njia bora na sahihi ya kuyaishi maisha yako.
Mara zote sema ukweli na hutahitaji kutumia nguvu nyingi kuwalazimisha watu wakubaliane na wewe.

Ukiona mtu anatumia muda na maelezo mengi kuelezea kitu,
Ukiona analazimisha watu wakubali na kuamini bila hata ya kuhoji,
Jua hapo kuna uongo.
Kwa kujua hili, unaweza kupembua ukweli na uongo kwa urahisi sana.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu sumu inayoua taratibu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/14/2175

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.