Hili ni swali la kwanza na muhimu kabisa kujiuliza kwenye jambo lolote lile. Ni rahisi sana kuamini yale ambayo watu wanatuambia hasa wanapoonekana kusema kutoka ndani ya mioyo yao na kwa ushawishi.

Tunachosahau ni kwamba kila mtu huwa anadanganya, wapo wanaofanya hivyo kwa kujua, ambao hawa hufanya hivyo kulinda maslahi yao au tu kupotosha wengine.

Na wapo wanaodanganya bila kujua, hawa kwa sehemu kubwa huwa wamesahau au wameamini kisichokuwa sahihi.

Kwa vyovyote vile, kuwa na njia ya kukusaidia kuujua ukweli badala tu ya kupokea na kuamini yale unayoambiwa na wengine.

Kumbuka kila mtu hudanganya, ni moja ya udhaifu ambao kila binadamu anao, usiufiche maana utakupoteza.

Mara kwa mara jihoji mwenyewe ni maeneo gani unajidanganya na kuwadanganya wengine.

Ukweli unakuweka huru, pambana kuufikia.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kazi muhimu kwako kufanya, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/01/2224

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma