
Akili yako ni kompyuta yenye uwezo wa hali ya juu mno. Huwa inachakata chochote kinachoingia na kuzalisha matokeo.
Kama uchafu unaingia kwenye akili, akili inauchakata na kutoa uchafu zaidi.
Vile ulivyo sasa kwenye maisha yako ni matokeo ya kile ulichoruhusu kiingie kwenye akili yako.
Kama unataka kuyabadili maisha yako, anza kwa kubadili unayoruhusu yaingie kwenye akili yako.
Ruhusu maarifa na taarifa safi ndiyo ziingie, huku ukizuia maarifa na taarifa chafu na hasi.
Linda sana akili yako, hiyo ndiyo rasilimali kubwa na muhimu zaidi kwako.
Ukurasa wa kusoma ni utapiamlo wa akili; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/12/2355
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Asante kocha kwa Maarifa aya
LikeLike
Karibu.
LikeLike