Rafiki yangu mpendwa,
Unaweza kushangaa mbona nazungumzia mwaka 2022, wakati ndiyo kwanza tuko nusu ya mwaka 2021!

Rafiki, wanajeshi huwa wanaamini duniani kuna makundi mawili ya watu, wanajeshi na raia. Kama siyo mwanajeshi basi wewe ni raia tu.
Na wanajeshi wana taratibu zao ambazo raia hawawezi kuzielewa.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio. Kuna makundi mawili ya watu, wale wanaofanikiwa sana na watu wa kawaida.
Wanaofanikiwa sana wana namna wanaishi maisha yao ambayo watu wa kawaida hawawezi kuielewa.

Na hiyo ndiyo maana unaona naongelea mwaka 2022, kwa sababu kwenye KISIMA CHA MAARIFA, jamii ya kipekee ambayo inayasaka mafanikio makubwa mno na kukataa ukawaida, hatuhesabu mwaka kwa kalenda ya kawaida.

Ule utaratibu wa kuanza mwaka tarehe moja januari na kushangilia ni mwaka mpya ni utaratibu wa watu wa kawaida na umekuwa kikwazo kwao kupiga hatua kwenye maisha yako.

Hebu fikiria ni mara ngapi watu wamekuwa wanaweka malengo yale yale kila mwaka ila hawayafikii? Pamoja na vikwazo vingine, lakini cha kwanza kabisa ni kukosea ‘timing’.
Januari mosi siyo muda mzuri wa kuweka na kuanza kufanyia kazi malengo, kuna kelele na usumbufu mwingi mno.

Ndiyo maana kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunauanza mwaka wetu wa mafanikio wiki ya kwanza ya mwezi nobemba kila mwaka. Hapo ndipo mwaka wetu mpya wa mafanikio unaanza na tunapambana kufanya makubwa.

Uzuri wa kuanza mwaka katika kipindi hicho ni wengi wanakuwa wameshachoka na kukata tamaa, wanasubiri tena January mosi ifike waanze tena heka heka za malengo.
Wakati wengine wamechoka na kukata tamaa, sisi ndiyo tunakuwa tunauanza mwaka, tukiwa na hamasa kubwa kweli kweli na hilo linatuweka kwenye nafasi nzuri ya ushindi.

Rafiki, mwaka huo wa mafanikio pia huwa tunauanza kwa kukutana pamoja kwenye semina ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA. Hapa tunakutana wanamafanikio wote kutoka kila eneo, tunakaa pamoja, tunapata mafunzo na hamasa na tunaondoka tukiwa na moto wa kutusukuma kwa mwaka mzima.

Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa kwamba SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo ndiyo inakwenda kuuanza mwaka wa mafanikio itafanyika tarehe 16 na 17 mwezi Oktoba 2021 jijini Dodoma Tanzania.

Huo ndiyo wakati wa kukutana pamoja watu wote wenye kiu ya mafanikio, kuweka mikakati ya kupambania kwa mwaka mzima na kuondoka tukiwa na moto wa kufanya makubwa.

Lakini huenda umewahi kushiriki semina na mikutano mbalimbali, ukatoka ukiwa na hamasa kubwa lakini siku chache baadaye hamasa hiyo ikapotea kabisa na kurudi kwenye maisha yako ya kawaida.

Nikuambie tu kwamba hilo halitatokea unapokuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Moto unaouwasha hautazima kwa mwaka mzima. Hamasa unayoipata utaendelea kuichochea kwa mwaka mzima.

Hiyo ni kwa sababu kwa mwaka mzima nitakufuatilia kwa karibu kuhakikisha yale uliyopanga unayatekeleza kama ulivyopanga.

Hivyo nikukaribishe sana ushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, kwani utapata nafasi ya kufanya kazi kwa karibu na Kocha kwa mwaka mzima unaofuata baada ya semina.
Nakuahidi sitakuacha njiani, labda wewe mwenyewe uamue kukataa kabisa, lakini kama bado utakuwa na nia ndani yako na hujakata tamaa, tutakwenda pamoja na mwaka wako utakuwa wa tofauti kabisa.

Wahi sasa nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, nafasi ni chache kwa sababu naweza kufanya kazi moja kwa moja na watu wachache tu.
Kama bado hujathibitisha kushiriki semina hii, tuma ujumbe sasa wenye maneno NITASHIRIKI SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 kwenda namba 0717 396 253 na utajiwekea nafasi yako pamoja na kupata utaratibu zaidi.

Rafiki, hii ndiyo nafasi ya kipekee ya kuleta mabadiliko yanayodumu kwenye maisha yako. Katibu tuwe pamoja tarehe 16 na 17 oktoba  tuweke mipango ya mwaka mzima wa mafanikio na nikufuatilie kwa mwaka mzima.

Kumbuka duniani kuna makundi makubwa mawili ya watu, wanaofanikiwa sana na wanaobaki kawaida. Maisha ni yako na uchaguzi ni wako. Kama umechagua kubaki kawaida basi endelea ulivyo sasa.
Ila kama umechagua kufikia mafanikio makubwa, hakikisha upo kwenye KISIMA CHA MAARIFA na usikose SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Nakusubiri kwa haku na shauku kubwa, ili tuweze kuupangilia na kuushinda mwaka 2022 kabla hata haujaanza.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
www.amkamtanzania.com