Rafiki yangu mpendwa,
Tarehe 16 na 17 Oktoba 2021 tunakwenda kuwa na SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA.

Hili ni tukio la kukutana ana kwa ana kwa wale wote wenye kiu ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao.
Tukio hili huwa linatokea mara moja tu kwa mwaka na siyo tukio la kukosa kwa yeyote aliye makini na mafanikio yake.

Rafiki, nakusihi sana ushiriki kwenye semina hii kwa sababu inakwenda kuwa na manufaa makubwa mno kwako.
Inakwenda kukupa miongozo sahihi ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima ili uweze kupiga hatua kubwa zaidi.

Ili kuhakikisha hujipi sababu yoyote ile ya kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, ninakwenda kukushirikisha SABABU 30 KWA NINI HUPASWI KUKOSA SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Kila siku kwa siku 30 za mwezi huu wa Septemba 2021 nitakupa sababu moja ya msingi kabisa, kisha wewe ufanye maamuzi ambayo ni sahihi kwako na ambayo hutoyajutia.

Sababu ya kwanza ya kwa nini hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni UNAKWENDA KUPATA ANGALAU TSH MILIONI 2 YA ZIADA.

Rafiki, bidhaa na huduma zote ambazo huwa nazitoa huwa natumia msingi wa MARA KUMI (10X).
Kwamba gharama yoyote ambayo mtu analipia kwa bidhaa au huduma ninayouza, yeye anakwenda kupata mara kumi ya kile alicholipia.

Nimekuwa nasimamia msingi huu kwa kila ninachofanya na ndiyo maana nimekuwa najisukuma sana kuhakikisha kila ninachomuuzia mtu kinakuwa na manufaa kwake.

Kwa sababu huduma hii nimepanga kuifanya kwa maisha yangu yote mpaka siku nakufa, najua njia pekee ya kuweza kuendelea ni kwa watu kunufaika.
Kama watu hawanufaiki hawawezi kuwa tayari kuendelea kulipia huduma hizi.

Pia moja ya falsafa ninazotumia kwenye huduma hii ni ile ya UNAWEZA KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA KWENYE MAISHA YAKO KAMA UTAWASAIDIA WENGI ZAIDI KUPATA KILE WANACHOTAKA.

Kwa kuwa ninachotaka ni fedha, tena kwa kiwango cha mabilioni, ninahakikisha nawasaidia wengi zaidi kupata fedha kwa viwango vya mabilioni.

Ndiyo maana nakusihi sana wewe rafiki yangu usikose SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, kwani kwa kiwango cha chini kabisa, utapata kipato cha ziada kisichopungua tsh milioni 2.

Kumbuka hicho ni kiwango cha chini, tena kwa yule ambaye huenda anajiambia hajui wapi ataanzia ili kuongeza kipato chake. Lakini nafasi ya kupata zaidi ya hapo, hata mara 10 au 100 inawezekana kabisa.
Na hiyo ni ndani ya mwaka mmoja.

Kwa nini milioni 2?
Kama nilivyokueleza hapo juu, msingi ninaotumia ni 10X, yaani kupata mara 10 ya kile unacholipia.
Ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 kwa siku mbili ni tsh laki mbili.

Hivyo kwa kulipia laki mbili na kushiriki semina, nakuhakikishia unakwenda kuongeza angalau tsh milioni mbili kwa mwaka mmoja tunaokwenda kufanya kazi pamoja baada ya semina.

Nani ambaye hapendi uwekezaji bora namna hiyo? Kwamba unapata mara kumi ya kile ulichowekeza.
Na hii sikuambii kukufurahisha, bali nakuambia kwa uhakika.
Ninakuhakikishia kabisa kwa sababu wengine wameweza, na wewe pia utaweza.

Karibu sana ushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ili ujihakikishie kuongeza kipato chako kwa angalau tsh milioni 2.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz