Rafiki yangu mpendwa,
Najua kuna mengi makubwa ambayo unayataka kwenye maisha yako.

Inaweza kuwa ni kuongeza kipato chako na kufikia uhuru wa kifedha.

Inaweza kuwa ni kuanzisha na kukuza biashara yako ili iwe na mafanikio makubwa.

Inaweza kuwa ni maeneo mengine ya maisha yako unayotaka kuyaboresha, iwe ni kazi, afya na mahusiano.

Ninachotaka kukuambia ni hiki, chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, kinawezekana kabisa.

Kitendo tu cha wewe kuweza kukifikiria na kukitaka, ni kiashiria kwamba kinawezekana na wewe unakiweza kabisa.

Kama kitu kingekuwa hakiwezekani, usingeweza hata kukifikiria.
Napoleon Hill amewahi kusema; chochote kile ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufikiri na kuamini, inaweza kukifikia.

Unajionea hapo rafiki, kama umeweza kukifikiria kitu, hatua ya pili muhimu ni kukiamini na hapo lazima utakipata.

Swali ni je unakipataje? Maana kufikiria na kuamini ni hatua tu za awali.
Napoleon Hill, kwenye kitabu chake cha Think And Grow Rich ametushirikisha hatua sita na za uhakika za kutaka chochote kile unachotaka.

Na hii ndiyo sababu ya 8 kwa nini hupaswi kukosa kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kwenye semina hiyo, utapata nafasi ya kutengeneza hatua hizo sita na kuzifanyia kazi kila siku, kitu ambacho kitakuwezesha kupata matokeo bora kabisa.

Kuna vitu viwili vinavyohusiana kwa karibu ambavyo utakwenda kufanyia kazi mwaka mzima baada ya semina. Vitu hivyo ni FEDHA na BIASHARA.
Haya ndiyo maeneo mawili ambayo kila mmoja wetu ana uhitaji wa kupiga hatua, lakini pia ndiyo maeneo yenye nguvu ya kutupa mafanikio makubwa.

Kwa kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 unakwenda kujijengea hatua sita za kufuata ili kuweza kukuza biashara yako na kuongeza kipato chako.

Kwa kifupi nikushirikishe hatua hizo sita kutoka kwa Napoleon Hill, lakini kwa undani wake na hatua za kuchukua utajifunza kwenye semina.

Hatua ya kwanza; jua kwa hakika nini unataka.

Lazima ujue kwa hakika nini unataka na utaje kwa namba kabisa.
Hii ni hatua muhimu kwani sababu namba moja kwa nini watu hawapati wanachotaka ni hawajui nini hasa wanachotaka.

Kwa upande wetu hapa utakwenda kutaja kiwango cha fedha unachotaka kupata kwa mwaka mmoja baada ya kushiriki semina.
Unataja namba kabisa ambayo utaifanyia kazi.

Hatua ya pili; unachokwenda kutoa.

Hakuna kitu cha bure, kila kitu kizuri kina gharama.
Hivyo ili kupata unachotaka, kuna gharama unapaswa kulipa, kuna vitu unapaswa kutoa.
Kwenye hatua hii ya pili unakwenda kueleza wazi nini unakwenda kutoa ili kupata unachotaka.

Kwa upande wetu, tunakwenda kutoa thamani kupitia biashara. Tunachagua matatizo au changamoto walizonazo watu, tunazitatua na wanakuwa tayari kutulipa fedha.
Kwenye hatua hii utaeleza thamani gani unakwenda kutoa ili kupata fedha unazotaka.

Hatua ya tatu; tarehe ya ukomo.

Lazima uweke tarehe ya ukomo ya kupata kile unachotaka.
Bila ukomo, sisi binadamu huwa tuna tabia ya kuahirisha mambo kwa kuona muda bado upo.
Unapojiwekea tarehe ya ukomo, unajisukuma kwa kujua muda siyo rafiki.

Kwa upande wetu tarehe ya ukomo ni mwaka mmoja tangu kushiriki semina.
Hivyo utakuwa na tarehe ya uhakika ambayo ndiyo unapanga kuwa umepata kile unachotaka.

Hatua ya nne; weka mpango na tekeleza.

Unahitaji mpango kamili ambao utafanyia kazi ili kuweza kupata unachotaka.
Bila ya kuwa na mpango unaoufanyia kazi, utakuwa tu unajifurahisha.
Ni kupitia kuchukua hatua ndiyo unaweza kupata chochote unachotaka.

Kwa upande wetu tunakwenda kuwa na mpango wa kibiashara utakaoufanyia kazi kwa mwaka mzima  ili kupata kiasi cha fedha ulichochagua.
Mpango huo utalenga maeneo matano;
1. Kuongeza mtaji.
2. Kuongeza wateja.
3. Kuongeza mauzo.
4. Kutoa thamani zaidi.
5. Kupunguza gharama.
Kwa kufanyia kazi hayo, matokeo makubwa yanakuwa ni ONGEZEKO LA FAIDA.

Hatua ya tano; andika maelezo ya hatua hizi.

Unapaswa kuandika maelezo ya hatua hizi, nini hasa unataka, muda wa kukipata, utatoa nini na mpango wako ni upi.
Kwa kuandika hatua hizi unakuwa umezielewa kwa kina na kujua nini cha kufanyia kazi.

Kwa upande wetu tutaandika kiwango cha fedha tunachotaka kupata, muda wa kukipata, thamani tunayopanga kutoa na mpango tunaofanyia kazi.
Maelezo hayo ndiyo yanabeba mkakati wa mwaka wetu mzima wa mafanikio.

Hatua ya sita; yasome maelezo yako kila siku.

Baada ya kuandika maelezo yako kwenye hatua ya sita hapo juu, unapaswa kuyasoma angalau mara mbili kila siku.
Pale unapoamka asubuhi na kabla hujalala.
Unapoyasoma kabla ya kulala unaipa akili yako ya ndani (subconscious mind) kitu cha kufikiria unapokuwa umelala.
Unapoyasoma pale unapoamka unayafanya kuwa kipaumbele chako kwa siku nzima.

Kwa upande wetu, tutakuwa tunayaandika maelezo haya upya kila siku tunapoamka.
Hiyo itakwenda kuwa njia bora ya kuhakikisha tunayafanyia kazi kwa mwaka mzima bila kuacha hata siku moja.

Rafiki yangu mpendwa, hapa nimekueleza kwa kifupi sana.
Kujifunza hatua hizi kwa undani wake na kuweka kwenye vitendo, yaani kutengeneza mpango utakaofanyia kazi kwa mwaka mzima, karibu ushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kwenye semina hiyo utajifunza hayo hatua kwa hatua na Kocha atakusaidia kutengeneza mpango sahihi kwako na kukusimamia kwenye utekelezaji wake kwa mwaka mzima.

Rafiki, hii siyo semina ya kukosa kama kweli uko makini na mafanikio makubwa unayoyataka.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, sehemu ambayo wale wote wenye kiu ya mafanikio makubwa na waliojitoa kweli kufanikiwa wanakutana na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

Kama bado hujajiwekea nafasi ya kushiriki semina hii muhimu sana kwa mafanikio yako, wasiliana sasa na 0717 396 253 upate nafasi yako mapema.

Kama bado hujakamilisha kulipa ada yako ya kushiriki semina, kamilisha sasa, kwani siku zimebaki chache za kufika ukomo wa kulipa ada.

Na kama ndiyo unasikia taarifa hizi za semina kwa mara ya kwanza hapa, soma hapo chini kupata maelezo zaidi.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz