Rafiki yangu mpendwa,

Mazingira huwa yana nguvu kubwa sana ya kuathiri fikra ambazo tunakuwa nazo.

Kadiri unavyokaa kwenye mazingira ya aina moja kwa muda mrefu, ndivyo fikra zako zinabaki kuwa za aina moja.

Kuna wakati mpaka unaweza kudhani umeshafanya kila kitu na hivyo hakuna namna nyingine tena.

Lakini unapoyabadili mazingira yako kwa muda mfupi tu, fikra zako zinabadilika, unakuwa na mtazamo wa tofauti na hapo unaziona fursa nyingi ambazo zinakuzunguka pale ulipo.

Na hiyo ni sababu kubwa kwa nini kila mwaka tunakutana pamoja kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA.
Semina ambayo inawakusanya wanamafanikio kutoka sehemu mbalimbali na kuwa pamoja kujifunza na kuhamasika ili kwenda kufanya makubwa zaidi.

Kwa kushiriki semina, unajiweka kwenye mazingira ya tofauti na yale uliyozoea na hapo kuna namna fikra zako zitabadilika.

Wapo watu wamekuwa wanasema ya nini nishiriki semina wakati napata maarifa ya kutosha kutoka kwenye vitabu?

Ni kosa kubwa sana kulinganisha semina ya kukutana ana kwa ana na kusoma vitabu au semina ya kushiriki kwa mtandao.

Kusoma vitabu au kushiriki mafunzo mengine kwa njia ya mtandao, hakukutoi pale ulipo sasa.
Hivyo pamoja na kupata maarifa mengi na mazuri, bado kubaki kwenye mazingira uliyopo kunakuwa na kikwazo fulani.

Wakati unajifunza utakuwa unajiambia hiki kinafaa, kile hakifai. Hiki kinawezekana, kile hakiwezekani. Na hayo yote yanakuwa yamechochewa zaidi na mazingira uliyopo.

Unaposhiriki semina ya kukutana ana kwa ana, unabadili kabisa mazingira yako.
Unakuwa eneo la tofauti na ulilozoea huku ukizungukwa na watu wa tofauti na uliowazoea siku zote.

Hayo mawili yanakufungua kwa kiwango kikubwa sana.
Unaondoa kila aina ya ukomo wa kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani.

Unapojifunza huku ukipata shuhuda za wengine ambao wameweza kufanya mambo ya tofauti, unaona hata na wewe unaweza pia.
Hilo tu linatosha kukusukuma kwenda kufanya mambo ya tofauti na ulivyozoea kufanya.

Hivyo hata kama unajifunza kwa kusoma vitabu na makala,
Hata kama unasikiliza na kuangalia mafunzo mbalimbali,
Kuna nguvu kubwa ambayo huwezi kuipata kama hujashiriki semina ya moja kwa moja.

Huwa wanasema picha moja inabeba maneno elfu moja.
Naweza kukuambia kwa uhakika kabisha kushiriki semina moja ya ana kwa ana ni sawa na kusoma vitabu mia moja.

Kama semina ina washiriki 100 na ukapata nafasi ya kuongea kwa kifupi na hata washiriki 30 tu, unapata thamani kubwa kuliko ungesoma vitabu 100.

Na ndiyo maana tunafanya SEMINA ZA KISIMA CHA MAARIFA mara moja tu kila mwaka. Kwa sababu maarifa unayoondoka nayo utaweza kuyafanyia kazi mwaka mzima na bado usiyamalize.

Rafiki yangu mpendwa, ni wakati sasa wa kukutana pamoja kama wanamafanikio kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo itafanyika jijini Dodoma tarehe 16 na 17 oktoba.
Hii siyo semina ya wewe kukosa, maana ina nguvu kubwa ya mabadiliko kwako.

Njoo tukae pamoja kwa siku hizo mbili, ubadili mazingira na watu wanaokuzunguka na hilo litapelekea ubadili mtazamo wako, fikra zako, hisia zako na hatua unazokwenda kuchukua.

Usikubali kabisa kukosa semina hii kama unataka mwaka ujao wa mafanikio ukawe wa tofauti kubwa kwako.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, sehemu ambayo wale wote wenye kiu ya mafanikio makubwa na waliojitoa kweli kufanikiwa wanakutana na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

Kama bado hujajiwekea nafasi ya kushiriki semina hii muhimu sana kwa mafanikio yako, wasiliana sasa na 0717 396 253 upate nafasi yako mapema.

Kama bado hujakamilisha kulipa ada yako ya kushiriki semina, kamilisha sasa, kwani siku zimebaki chache za kufika ukomo wa kulipa ada.

Na kama ndiyo unasikia taarifa hizi za semina kwa mara ya kwanza hapa, soma hapo chini kupata maelezo zaidi.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz