Rafiki yangu mpendwa,
Changamoto kubwa ya mafunzo na ushauri mbali unaotolewa kwenye eneo la mafanikio na kuwalenga watu kwa pamoja.

Kwa sababu kuna watu wamefanikiwa kwa njia fulani, basi wengine huona na wao wanaweza kufanikiwa kwa njia hizo hizo.

Hilo ni kosa ambalo limewaangusha wengo, limewafanya wahangaike na mengi ma bado wasipate mafanikio wanayoyataka.

Kila siri na tabia za mafanikio walizojifunza kwa wengine wamefanyia kazi, lakini bado hawafanikiwi.

Tatizo siyo siri na kanuni za mafanikio kutokufanya kazi, tatizo ni watu kuzichukua kama msaafu na kuzifuata bila kuziboresha ziendane na wao.

Sisi binadamu tunatofautiana, hakuna watu wawili wanaofanana kwa kila kitu, hata mapacha wa kufanana.

Hivyo kinachofanya kazi kwa mtu mmoja, kinaweza kisifanye kazi kwako pia.
Anachofanya mtu mwingine akafanikiwa na wewe ukakifanya hivyo hivyo hutafanikiwa.

Pamoja na kuzijua siri na kanuni za mafanikio, bado unahitaji kukaa chini na kutengeneza mpango wako binafsi wa mafanilio, mpango unaoendana na wewe.

Na hii ndiyo faida kubwa unayokwenda kuipata kwa kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Katika semina hiyo, utapata nafasi ya kufanya kazi na Kocha kwa karibu kuweka mpango wako wa mafanikio na kusimamiwa kwa karibu.

Semina na mafunzo mengi ya mafanikio huwa yanatolewa kwa watu wengi kwa wakati mmoja. Ndiyo maana pia gharama zake zinaweza kuwa ndogo.

Lakini SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA ni tofauti, hailengi wengi, bali inalenga wachache sahihi.
Hivyo nafasi za kushiriki ni chache na ndiyo maana gharama zake ni kubwa pia.

Kipi unataka kwenye maisha yako, kupata mafunzo ya mafanikio ya jumla na kuishia hapo au kupata mafunzo ya mafanikio yanayoendana na wewe na kuweza kuyafanyia kazi na ukapiga hatua?

Kama unachotaka ni mafunzo unayopata yawe na tija kwako, yalete mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako, basi unapaswa kuhakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Kwenye semina hiyo, utapata nafasi ya kukaa ana kwa ana na Kocha, kuweka na kupitia mpango na baada ya hapo kunakuwa na ufuatiliaji wa karibu kwa kipindi cha mwaka mzima mpaka tena kufika semina nyingine.

Kama nilivyokushirikisha hapo juu, nafasi za kushiriki semina hii ni chache na pia muda wa kupata nafasi hiyo umebaki mdogo sana.

Chukua hatua sasa kujihakikishia nafasi yako ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ili utengeneze mpango binafsi wa mafanikio na utakaofanyia kazi ili upate mafanikio ya kweli kwenye maisha yako.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz