Rafiki yangu mpendwa,
Kwa muda sasa nimekuwa nakupa taarifa kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo itafanyika jijini Dodoma tarehe 16 na 17 Oktoba 2021.

Nimekupa maelezo kamili ya semina hii, manufaa yake na sababu nyingi kwa nini hupaswi kuikosa.
Nimefanya hayo yote kwa sababu najua thamani kubwa ya semina hiyo kwako.
Najua huwezi kushiriki semina hiyo na ukabaki vile ulivyo sasa.
Ndiyo maana kutoka ndani ya moyo wangu kabisa, sitaki yeyote aliyejitoa kweli kufanikiwa akose semina hii.

Rafiki, napenda kuchukua nafasi hii kukukumbusha kwamba zimebaki siku 7 pekee za kupata nafasi ya kushiriki semina hii.
Mwisho kabisa wa kuthibitisha na kulipa ada ya kushiriki ni tarehe 01/10/2021.

Kama bado hujachukua hatua, lakini ndani yako kuna sauti inayokuambia shiriki hii semina, isikilize sauti hiyo, inajua namna unavyoihitaji semina hii.

Na kama bado una maswali au maeneo ambayo ungependa kupata ufafanuzi zaidi kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, nakupa nafasi ya kufanya hivyo leo.

Karibu uulize swali lolote lile au kuomba ufafanuzi wa jambo lolote kuhusu semina hii.
Uliza swali hilo moja kwa moja kwa kujibu ujumbe huu au kutuma kwenda namba 0717 396 253.

Maswali yote yatakayoulizwa nitashirikisha majibu ya pamoja na kwa wote kwenye makala ya kesho.
Hivyo karibu sana upate ufafanuzi wa chochote kinachokuwa kikwazo kwako kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Kumbuka, mwisho kabisa wa kupata nafasi ya kushiriki semina hii ni tarehe 01/10/2021, hivyo kama hujajihakikishia nafasi yako, fanya hivyo sasa kwa namba 0717 396 253.

Kama ndiyo unapata taarifa hizi kwa mara ya kwanza, soma taarifa kamili kuhusu semina hapo chini.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz