Rafiki yangu mpendwa,
Huwa naamini kwamba kama mtu una kitu kizuri na chenye manufaa kwa wengine, ni wajibu wako kuhakikisha wale wanaoweza kunufaika na kitu hicho wanajua uwepo wa kitu hicho ba jinsi kilivyo na manufaa kwao.

Huo ni wajibu wako kabisa na hupaswi kuwa na uvivu kwenye hilo.
Maana kwa zama za sasa, watu wana mambo mengi, siyo rahisi wajue au wakumbuke kila kitu, hata kama ni muhimu kwao.

Ndiyo maana makampuni yote makubwa huwa yana matangazo endelevu. Chukua mfano wa mitandao ya simu, hata kama tayari unatumia mtandao husika, bado wataendelea kukutangazia. Kwa sababu wanajua wasipokutangazia, ni rahisi kusahau.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nakupa taarifa za SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021. Nimekupa kila sababu kwa nini hii siyo semina ya wewe kukosa na jinsi ilivyo na manufaa kwako.

Sasa ni wakati wako wa kufanya maamuzi, maana muda umefika ukingoni kabisa.
Tumebakiwa na siku 4 pekee za kupata nafasi ya kushiriki kwenye semina hiyo.

Huu siyo wakati wa kuendelea kujifikiria sana. Ni wakati wa kuisikiliza nafsi yako na kuchukua hatua.
Kama nafsi yako inakuambia hiki ni kitu muhimu kwako, basi fanya kila namna uweze kushiriki semina hii.
Maana nafsi yako inayajua mengi ambayo siyo rahisi akili yako kujua.

Rafiki, ijumaa ya tarehe 01/10/2021 ndiyo siku ya mwisho kabisa kwako kupata nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Usisubiri mpaka siku ya mwisho ndiyo uchukue hatua, bali chukua hatua sasa ili kujihakikishia nafasi yako.

Kama bado una wasiwasi kama semina itakuwa sahihi kwako, nakusihi uweke wasiwasi wako pembeni na ushiriki semina. Utakuja kujishukuru mno baadaye kwa hatua uliyochukua leo.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz