Rafiki yangu mpendwa,
Mara kwa mara umekuwa unafanya maamuzi mabovu kwenye maisha yako.
Hilo linatokana na makosa ya kisaikolojia ambayo kila mmoja wetu huwa anayafanya.
Ni mara ngapi umetoka nyumbani ukiwa huna mpango wa kununua kitu chochote kile, lakini ukarudi nyumbani ukiwa umenunua vitu mbalimbali ambavyo huna hata matumizi navyo?
Unajikuta umekutana na tangazo la kitu kinauzwa kwa bei ya punguzo, ambapo mwisho wa punguzo hilo ni siku hiyo. Unasukumwa kununua ili usikose punguzo hilo. Unachokuwa huoni ni kwamba hujanunua kitu hicho kwa sababu unakihitaji, ila kwa sababu hutaki kupitwa na punguzo.
Huo ni mfano mmoja wa makosa ya kisaikolojia ambayo huwa yanapelekea wewe ufanye maamuzi mabovu.
Ukiangalia matangazo mengi ya kibiashara, utajionea wazi jinsi yalivyoandaliwa kuteka saikolojia yako ili ufanye maamuzi mabovu.
Chukua mfano wa matangazo yenye neno BURE au PUNGUZO. Ukiyaona maneno hayo kwenye tangazo, unasahau kwamba hukuwa na uhitaji na vitu hivyo, badala yake unakimbilia kununua ili usikose.

Angalia matangazo ya vilevi mbalimbali, utaona watu warembo na watanashati wakifurahia kupata kilevi hicho. Kamwe huwezi kuona tangazo la kilevi likionyesha mtu akiwa amelewa, yanakuwa yanaonyesha vitu vizuri pekee ili vikuvutie.
Pia matumizi ya watu maarufu kwenye matangazo mbalimbali kunakufanya utake sana kutumia vitu hivyo kwa sababu unataka kuwa kama mtu huyo maarufu.
Akili zetu huwa zinafanya maamuzi mengi kwenye maisha yetu. Zoezi la kufanya maamuzi siyo rahisi, linahitaji muda na nguvu pia.
Hivyo akili zimetengeneza njia ya mkato katika kufanya maamuzi yanayojirudia.
Akili inaangalia vitu vichache ambavyo vikishakuwepo basi inafanya maamuzi mara moja.
Hili ni kwa nia njema kabisa, kwamba badala ya akili kutumia rasilimali zake nyingi kufanya maamuzi kila mara, inatengeneza njia ya mkato.
Kwa bahati mbaya sana, wachache wanaojua njia hizo za mkato huwa wanazitumia kujinufaisha wao wenyewe zaidi.
Wale wanaojua jinsi saikolojia ya binadamu inavyofanya kazi, wanaweza kuitumia kuwashawishi watu kufanya maamuzi yenye manufaa kwao.

Kwenye kitabu kipya cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO kina sura inayokufundisha jinsi ya kufanya maamuzi bora ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Ni kwenye sura hii ndiyo unapata nafasi ya kujifunza makosa 28 ya kisaikolojia yanayopelekea wewe ufanye maamuzi mabovu.
Makosa hayo 28 ni mambo ambayo umezoea kufanya kila siku, ila yamekuwa yanachangia sana wewe kufanya maamuzi mabovu.
Kwa kuyajua makosa hayo 28 na kuyafanyia kazi, utaweza kufanya maamuzi bora kabisa kwa mafanikio yako.
Usikubali kuendelea kufanya maamuzi mabovu ambayo yanakugharimu sana. Yajue makosa ya kisaikolojia uliyonayo na jinsi yanavyoathiri maamuzi yako kisha uchukue hatua sahihi.
Jipatie leo kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO ili uweze kuyakabili makosa hayo ya kisaikolojia yasiwe tena kikwazo kwako.
Kupata kitabu wasiliana na 0752 977 170 na utatumiwa au kuletewa kitabu pale ulipo.
Kuijua saikolojia yako ni hitaji muhimu kwa mafanikio yako. Kama huyajui makosa unayofanya kwenye maamuzi, utaendelea kufanya maamuzi ambao yanakugharimu na kukuzuia usifanikiwe.
Pata na usome kitabu leo ili uweze kufanya maamuzi bora kwa mafanikio yako.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.