Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya sifa muhimu unayopaswa kujijengea na kuilinda kama unataka mafanikio makubwa ni uaminifu.
Iko hivi, chochote unachotaka kwenye maisha yako kinatoka kwa wengine.
Na hao wengine wapo tayari kukupa unachotaka kama wanakuamini.
Kama huaminiki, watu hawapo tayari kushirikiana na wewe na hilo litakuwa kikwazo kwa mafanikio yako.
Uzuri ni kwamba uaminifu siyo kitu ambacho inabidi uwaombe watu wakupe, au ambacho unahitaji fedha kukinunua.
Wala siyo kitu cha kurithi useme kwamba umekikosa kwa sababu hujarithishwa.
Uaminifu ni kitu ambacho mtu unajenga au kubomoa wewe mwenyewe, kutokana na tabia unazokuwa nazo.
Kuna tabia zinazojenga uaminifu na kuna tabia ambazo zinaubomoa.
Wajibu wako ni kuwa na tabia zinazojenga uaminifu na kuepuka tabia ambazo zinavunja uaminifu.
Kuna tabia moja muhimu sana ambayo ukijijengea, utajenga uaminifu mkubwa sana kutoka kwa wengine.
Tabia hiyo ni rahisi kuifanya kuwa kanuni unayoiishi kila siku na ikaleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Kanuni hiyo ni; FANYA NENO LAKO KUWA SHERIA.
Rafiki, kanuni ni hiyo, rahisi na inayoeleweka kabisa, isiyohitaji uwe na elimu kubwa ndiyo uweze kuitekeleza.
Ni rahisi kabisa, kila neno linalotoka kwenye kinywa chako, linakuwa sheria kwako.

Hivi unajua watu huwa wanakuhukumu kwa maneno yako mwenyewe?
Na kwa sababu ni rahisi kuongea kuliko kutekeleza, umekuwa unaongea mengi, unatekeleza machache na hivyo watu wanakuchukulia muongeaji tu!
Sasa ni wakati wa kujenga sifa mpya, kuondoa sifa ya ubabaishaji ambayo huenda ukishajijengea huko nyuma kwa kuropoka mambo ili tu kuwafurahisha watu, lakini kwenye utekelezaji ukashindwa.
Sasa ni wakati wa kujijengea sifa ya uaminifu kwa kuishi kanuni ya neno lako kuwa sheria.
Ahidi yale tu ambayo una uhakika yako ndani ya uwezo wako kutekeleza.
Na ukishaahidi, pambana kutekeleza kama ulivyoahidi.
Hata kama utakutana na magumu au changamoto, usikimbilie kutumia kama sababu, badala yake simamia neno lako kuwa sheria.
Kuna wakati unafanya kila unaloweza kufanya, lakini inakuwa vigumu kutekeleza kile ulichoahidi.
Je kwenye nyakati kama hizi unaishije kanuni hii ya neno lako kuwa sheria?
Ipo njia nzuri mno ya kuendelea kuishi kanuni hii ya neno lako kuwa sheria hata kama imeshindikana kabisa kutekeleza kile ulichoahidi.
Njia hiyo imeelezwa kwa kina kabisa kwenye kitabu kipya cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.
Sura ya saba ya kitabu hiki imeeleza kwa kina jinsi ya kuishi kanuni hii ya kufanya neno lako kuwa sheria.
Inakupa njia za kuitekeleza mara zote kwa kuhakikisha unaahidi mambo ya uhakika.
Lakini zaidi, kinakupa njia ya kuendelea kusimamia neno lako hata pale kila kitu kinaposhindikana kabisa.
Kama kweli unayataka mafanikio kwenye maisha yako, kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO hupaswi kukosa kukisoma.
Jipatie nakala yako ya kitabu leo kwa kuwasiliana na 0752 977 170 na utatumiwa au kuletewa kitabu ulipo.

Fanya kila neno lako kuwa sheria na utaweza kujijengea uaminifu mkubwa kwa wengine utakaokuwezesha kufanikiwa sana.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.