Rafiki yangu mpendwa,
Najua unayataka mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Lakini je uko tayari kulipa gharama unayopaswa kulipa ili ufanikiwe?
Wengi ambao hawafanikiwi ni kwa sababu wanafikiri mafanikio ni kitu kinachokuja kwa sababu tu wanayataka au wanastahili.
Aliyewahi kuwa tajiri mkubwa J. P. Getty amewahi kusema siri kubwa ya mafanikio inaweza kufupishwa kwenye hatua hizi tatu;
1. Jua kwa hakika nini unachokitaka.
2. Jua gharama unayopaswa kulipa ili kupata unachotaka.
3. Kuwa tayari kulipa gharama hiyo ili upate unachotaka.
Rafiki, kanuni hii fupi imebeba ujumbe mkubwa mno kuhusu mafanikio. Ukichagua kuiishi kanuni hii tu na ukaachana na mengine yote, lazima utafanikiwa.
Kulipa gharama ni hitaji muhimu sana ili uweze kufanikiwa.
Na kadiri mafanikio unayotaka kupata yanavyokuwa makubwa, ndivyo gharama ya kulipa nayo inakuwa kubwa pia.
Je ni gharama zipi unazopaswa kulipa ili upate mafanikio unayotaka wewe?
Hapa ndipo wengi wanakwama, maana wanataka sana kufanikiwa, ila hawajui gharama gani walipe.

Sehemu muhimu ya kulipa gharama za mafanikio ni kuzijua na kuziishi sheria za mafanikio.
Hizo ni sheria ambazo mtu yeyote akizifuata, bila ya kujali anafanya nini, lazima atafanikiwa.
Kuna sheria muhimu 100 za maisha ya mafanikio ambazo kila anayetaka kufanikiwa anapaswa kuzijua na kuziishi kwenye kila siku ya maisha yake.
Yeyote asiyejua na kuishi sheria hizi, ni vigumu sana kufanikiwa. Atahangaika na mengi hapa duniani, lakini hakuna makubwa atakayopata.
Je wewe rafiki yangu upo tayari kuzijua na kuziishi sheria 100 za mafanikio?
Kama jibu ni ndiyo basi nina habari njema kwako.
Kitabu kipya cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO kipo tayari na kimesheheni sheria hizo 100 unazopaswa kuzijua na kuziishi.

Sheria hizo hazihitaji uwe na elimu kubwa, uwe na uwezo mkubwa au mtandao. Ni sheria ambazo kila mtu aliyejitoa kweli kufanikiwa anaweza kuziishi na akabadili sana maisha yake.
Najua umejitoa kufanikiwa ndiyo maana umesoma mpaka hapa, sasa fanya kitu kimoja, wasiliana sasa na 0752 977 170 ili kupata nakala yako ya kitabu na kujifunza sheria hizo 100 ili uanze kuziishi mara moja.
Usikubali kuendelea kuhangaika na mengi hapa duniani wakati kuna machache ya msingi ambayo ukiyazingatia yataleta matokeo makubwa.
Pata sasa kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO ili ujue hayo machache na muhimu ya kuzingatia kwenye maisha yako na upate mafanikio makubwa.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.