Rafiki yangu mpendwa,
Umezoea mwaka mpya huwa unaanza tarehe moja mwezi wa kwanza wa kila mwaka.
Na huo ndiyo wakati ambao wimbo maarufu wa ‘mwaka mpya mambo mapya’ husikika kwenye kinywa cha kila mtu.

Ni wakati ambao watu huwa na hamasa ya hali ya juu ya kuweka malengo kwa kufuata mkumbo.
Kwa sababu kila mtu anazungumzia malengo, basi kila mtu anaweka malengo.

Siku za mwanzo wa mwaka huwa ni siku ambazo zimechangamka kwenye maeneo mengi.
Ukienda maeneo ya michezo na mazoezi yanakuwa yamejaa.
Ukienda maduka ya vitabu unakuta wanunuaji wengi.
Wengi wanakuwa wameanza kwa kasi utekelezaji wa malengo waliyojiwekea.

Ukirudi kwa watu hao hao mwezi mmoja baadaye, hutaamini kile utakachokiona, kwani ile hamasa kubwa ambayo watu walikuwa nayo awali inakuwa imetulia kabisa.
Ile kauli ya mwaka mpya mambo mapya inakuwa imezimika.
Watu wanakuwa wamerudi kwenye mazoea yao ya awali.

Wanasubiri tena mwaka mwingine mpya warudie zoezi hilo.
Hivyo ndivyo wengi wamekuwa wanaishi maisha yao na hilo linakuwa kikwazo kwa mafanikio yao.

Je wewe unataka kuendelea na hali hiyo ya kugangaika na mabadiliko ya mmhemko ya mwaka mpya kisha muda mfupi baadaye kurudi kwenye mazoea yako?
Kama jibu ni ndiyo basi endelea, lakini jua hutaweza kufanikiwa.

Kama jibu ni hapana, kama umechoshwa na hayo mahangaiko na unataka njia ya uhakika ya kupata mafanikio makubwa basi nina habari njema kwako.

Nakukaribisha kwenye mwaka mpya wa mafanikio 2021/2022 ambao utaanza tarehe 01/11/2021 na kumalizika mwezi oktoba 2022.

Mwaka huu mpya wa mafanikio ni tofauti na mwaka wa kalenda na una nguvu ya kukupa mafanikio makubwa kwa sababu kubwa tatu;

Moja ni unakupa nguvu kubwa ya ushindani.
Tunapoelekea mwisho wa mwaka, wengi wanakuwa wamechoka na kuona mwaka unaisha hivyo hawaweki tena juhudi kubwa.
Badala yake wanasubiria mwaka mpya uanze ndiyo waweke juhudi kubwa.
Kwa wewe kuuanza mwaka wa mafanikio wakati wengine wameshachoka, unakuwa mbele zaidi kiushindani.
Wakati wengine wanapumzika, wewe unaweka juhudi kubwa na hivyo kuwa na uwanja mpana wa kufanya makubwa.

Mbili unaondoka kwenye mhemko wa kuweka malengo kwa kufuata mkumbo. Unapoweka malengo mwanzo wa mwaka, kwa sehemu kubwa yanakuwa hayajatoka ndani yako, bali yanakuwa yamechochewa na wengine. Hayo yanakuwa siyo malengo sahihi kwako. Kwa kuuanza mwaka wa mafanikio tofauti na wengine, unaondoka kwenye kuweka malengo kwa mazoea.

Tatu inakuondoa kwenye kundi na mazoea na kuweka kwenye njia sahihi kwako.
Ukifanya kile ambacho umezoea kufanya, utapata matokeo ambayo umezoea kupata.
Ukifanya yale ambayo wengine wanafanya, utapata matokeo ambayo wengine wanafanya.
Hakuna kitakachobadilika kwenye maisha yako kama wewe mwenyewe hautabadilika.
Hivyo kuanza mwaka wa mafanikio kwa utofauti ni sehemu ya kuanza kubadilika na kuyabadili maisha yako.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili tuweze kuuanza mwaka mpya wa mafanikio kwa utofauti mkubwa, kitu kitakachokupa mafanikio makubwa.

Uzuri wa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA na kuuanza mwaka mpya wa tofauti ni unapata usimamizi wa karibu kwa mwaka mzima kwenye kufanyia kazi malengo yako.
Hivyo hutayaacha malengo hayo hata iweje, maana haupo peke yako katika kuyafanyia kazi.

Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA unajichelewesha kuianza safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Karibu ujiunge leo na KISIMA ili uwe sehemu sahihi kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe kwenda namba 0717 396 253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA na utapewa maelekezo.

Muhimu; muda wa kupata nafasi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ni mfupi, mwisho ni tarehe 31/10/2021 ili tuweze kuuanza mwaka mpya wa mafanikio pamoja.
Chukua hatua sasa ili usikose nafasi ya kuuanza mwaka mpya wa mafanikio pamoja na tuweze kufanya makubwa.
Tuma ujumbe sasa kwenda namba 0717 396 253.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.