Rafiki yangu mpendwa,
Zimebaki siku tisa pekee za kupata nafasi ya kujiunga na jamii ya KISIMA CHA MAARIFA kabla ya kuanza kwa mwaka wetu wa mafanikio 2021/2022.

Kwenye mwaka huo wa mafanikio ambao utaanza Novemba 2021 nitakwenda kufanya kazi kwa ukaribu kabisa na kila mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA ili kila mmoja aweze kupiga hatua kubwa.

Ili kupata nafasi hiyo ya kufanya kazi pamoja, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA sasa kabla mwaka wa mafanikio haujaanza.

Kama bado hujapata picha ya kwa nini unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA sasa, leo nakushirikisha vitu vitatu muhimu tunavyofanyia kazi.

Kitu cha kwanza ni IMANI.
Imani yetu kuu kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni UPENDO.
Tunaongozwa kwa upendo na tunaamini kwenye upendo.
Upendo huo umegawanyika kwenye maeneo matatu.
Eneo la kwanza ni upendo binafsi, ambapo tunajipenda wenyewe na kujikubali vile tulivyo.
Eneo la pili ni upendo kwa wengine, ambapo tunawapenda wengine na kuwakubali vile walivyo.
Eneo la tatu ni upendo kwenye kile tunachofanya, ambapo tunapenda sana kazi au biashara tunazofanya na kuzifanya kwa viwango vya juu.
Bila upendo wa kweli, ni vigumu sana kuweza kupata mafanikio makubwa.

Kitu cha pili ni MAONO.
Kwenye KISIMA tuna maono makubwa ambayo tunayafanyia kazi.
Maono hayo ni “Tunajenga  jamii ya  tofauti ambapo tumechagua  kuchukua jukumu  la maisha yetu,  kuishi maisha yenye kusudi,  kuwa na  ndoto kubwa  na kuzipigania ili kuwa  na mafanikio  na furaha .”
Kwa maono hayo, KISIMA CHA MAARIFA inakwenda kuwa jamii ya tofauti kabisa na ile ambayo tunatokea.
Inakuwa ni jamii ya watu wenye mafanikio makubwa na furaha.
Usikubali kukosa kuwa sehemu ya jamii hii.

Kitu cha tatu ni MKAKATI.
Tunao mkakati tunaofanyia kazi ili kufika kwenye maono makubwa tuliyonayo kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Mkakati wetu ni; “Tunajifunza na kuishi  misingi  sahihi ya mafanikio, tunashirikiana na wengine  wenye  mtazamo  wa mafanikio  na tunatoa thamani kubwa  kwa wengine.
Kwa kujifunza na kuishi misingi ya mafanikio, huku tukishirikiana na walio sahihi na kutoa thamani kubwa, hakuna namna tutayakosa mafanikio.

Kikubwa zaidi ni mtazamo mkuu ambao tumejijengea kwenye KISIMA CHA MAARIFA ambao ni KILA KITU  KINAWEZEKANA.
Tunaamini bila ya shaka yoyote kwamba kila kitu kinawezekana.

Je usingependa kuwa sehemu ya jamii hii ya tofauti na ya kipekee kabisa?
Chukua hatua sasa ya kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA kwa kuwasiliana na 0717 396 253.
Mwisho wa kupata nafasi ya kujiunga ni tarehe 31/10/2021, baada ya hapo hutaweza kupata nafasi hii tena.
Hivyo chukua hatua sasa hivi ili usiikose nafasi hii.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.