Rafiki yangu mpendwa,
Kikwazo kikubwa kabisa kwa watu kufanikiwa ni kukosa msingi ambao wanauishi kwenye maisha yao.
Wengi wanaposikia tu neno mafanikio, wanakimbilia kufanya chochote wanachoona kinaweza kuwapa mafanikio.
Matokeo yake watu wamejikuta wanahangaika na mambo mengi yasiyokuwa na tija kwao, kitu kinachokuwa kikwazo kwa mafanikio yao.
Ili uweze kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unapaswa kuwa na msingi unaoutumia kuyaendesha maisha yako.
Msingi ambao ndiyo utautumia kufanya maanuzi yote muhimu kwenye maisha yako ya mafanikio.
Misingi ipo mingi, kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA tunaongozwa na msingi mkuu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA.

Kama umesahau, KISIMA CHA MAARIFA ni jamii ya tofauti na ya kipekee kabisa ya watu ambao wamejitoa kweli ili kupata mafanikio makubwa.
Ni jamii ambayo watu wameshika hatamu ya maisha yao na hawalalamiki, kulaumu au kusubiri wengine waje wawatoe pale walipo.
Hii ni jamii ambayo kila aliye makini na anayetaka kupata mafanikio makubwa basi anapaswa kuwa ndani yake.
Na wewe, kama bado hujawa kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA unajichelewesha, chukua hatua sasa ili uwe sehemu ya jamii hii na ujihakikishie kufanikiwa.
Tukirudi kwenye msingi wetu mkuu, umeona una maneno matatu, lakini ni yenye nguvu kubwa.
Sehemu ya kwanza ya msingi wa mafanikio ni NIDHAMU.
Nidhamu ni kupanga na kufanya kama ambavyo umepanga bila ya kuruhusu sababu yoyote kuingilia.
Nidhamu ina maeneo mengi.
Nidhamu binafsi ya kufanya kama ulivyopanga.
Nidhamu ya muda ya kulinda na kuthamini muda wako.
Nidhamu ya fedha ya kuwa na matumizi mazuri ya fedha zako, matumizi kutokuzidi mapato.
Nidhamu ya kazi kwa kuweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya.
Bila nidhamu, huwezi kufanikiwa na hata ikitokea umefanikiwa, utaanguka haraka sana.
Sehemu ya pili ya msingi wa mafanikio ni UADILIFU.
Uadilifu ni kuwa na maisha ya aina moja, faraghani na hadharani.
Kwenye jamii za kawaida, watu wengi huwa na maisha ya aina nyingi.
Wakiwa mbele za watu hutaka kuonekana wa aina fulani.
Wakiwa peke yao wanafanya mambo ambayo ni ya tofauti kabisa.
Watu hawa huwa na mambo wanayoyaficha mara zote, kitu kinachowagharimu sana.
Kwa kutumia njia zisizo sahihi huwa wanaweza kufanikiwa, ila mafanikio hayo hayadumu kwa muda mrefu.
Mafanikio ya kweli na yanayodumu yanahitaji mtu awe na uadilifu.
Atimize kile anachoahidi kwa namna alivyoahidi.
Mara zote afanye kile kilicho sahihi bila kujali nani anaangalia.
Na awe na maisha ya aina moja, asiwe na chochote ambacho anaficha kwa wengine.
Bila uadilifu, huwezi kujenga uaminifu kwa wengine, kitu ambacho ni muhimu sana kwa mafanikio.
Sehemu ya tatu ya msingi wa mafanikio ni KUJITUMA.
Hapa unahitaji kwenda hatua ya ziada kwa kila unachofanya.
Usifanye kile tu ambacho kimezoeleka au kinategemewa, badala yake nenda hatua ya ziada.
Fanya zaidi ya ilivyozoeleka na inavyotegemewa.
Toa thamani kubwa kuliko unavyolipwa.
Kwa njia hizo, unakuwa umeitega asili, unakuwa umeikopesha na kwa kuwa asili haipendi madeni, itahakikisha inakulipa.
Kwenye jamii ya kawaida watu wamekuwa wanasubiri walipwe zaidi kwanza ndiyo waanze kufanya kwa juhudi kubwa.
Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA tuko tofauti, tutaanza kufanya kwa juhudi kubwa kwanza na baadaye tunalipwa zaidi.
Kwa chochote unachofanya, nenda hatua ya ziada, fanya zaidi ya ilivyozoeleka au unavyotegemewa na utaona jinsi matokeo yatakavyokuwa mazuri.
Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kuishi msingi huo wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA kwa vitendo na uyaone matokeo yake kwenye maisha yako.
Zimebaki siku na nafasi chache za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Mwisho wa kupata nafasi ya kujiunga ni tarehe 31/10/2021 ili tuweze kuuanza pamoja mwaka wa mafanikio.
Karibu sana uchukue hatua ya kujiunga leo. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA wasiliana na 0717 396 253 kupata maelezo kamili.

Pia hakikisha unapata kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO ambacho ni nguzo muhimu sana kwa mafanikio yako.
Kitabu hiki kina maarifa muhimu sana unayohitaji ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako.
Wasiliana sasa na 0752 977 170 kupata nakala yako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.