Rafiki yangu mpendwa,
Kauli maarufu kwenye zama tunazoishi sasa ni mambo mengi muda mchache.

Ukizingatia simu zetu janja tulizonazo, ambazo tunakwenda nazo kila mahali, zinatosha kutuweka ‘bize’ kwa siku nzima huku hakuna chochote chenye tija tunachokamilisha.

Mambo ni mengi kweli, na kila siku yanaongezeka. Lakini muda ni ule ule wa masaa 24 tu kwa siku.
Je unachaguaje ufanye nini na uache nini?

Hapo ndipo ambapo wengi wamekuwa wanakwama na kupelekea kushindwa kupata mafanikio makubwa.

Leo unakwenda kujifunza mwongozo sahihi wa kufanya maamuzi yatakayokufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, jamii ya kipekee katika kuyaendea mafanikio, tunao mwongozo mkuu wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA.
Vitu hivyo vitatu ndiyo vinatuongoza tufanye nini na tusifanye nini ili tuweze kufanikiwa.

Tukianza na AFYA.
Huu ndiyo mtaji mkuu kabisa kwenye maisha, maana bila afya hakuna kitu kikubwa unachoweza kufanya.
Mafanikio ni shughuli pevu ambayo inamtaka mtu awe na afya imara kabisa.

Hivyo katika kufanya maamuzi yako, unapaswa kuweka kipaumbele kwenye afya. Unapaswa kufanya mambo yanayoboresha afya yako na kuepuka yale yanayoidhoofisha.

Kuna vitu vitatu muhimu kwenye afya ambavyo unapaswa kuvizingatia.
Cha kwanza ni ulaji sahihi, kula virutubisho sahihi na kuepuka sumu mbalimbali.
Cha pili ni kufanya mazoezi, mazoezi ni sehemu muhimu ya kuimarisha afya.
Cha tatu ni kupumzika, unapaswa kupata muda wa kupumzika ili upate nguvu za kuendelea na mapambano ya mafanikio. Zingatia sana afya maana bila hiyo hakuna kingine kinachowezekana.

Wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA wakifanya mazoezi ya pamoja ikiwa ni sehemu ya kujenga afya imara. Kama unapenda kuwa sehemu ya jamii hii ya kipekee wasiliana sasa na 0717 396 253

Tukienda kwenye UTAJIRI.
Haya ni matokeo ya maisha ya mafanikio, kwa kuishi kwa misingi sahihi, utajiri unakuwa ni matokeo.

Unapaswa kutumia utajiri kama kigezo katika kuweka vipaumbele vyako, ukizingatia kufanya yale yanayojenga na kulinda utajiri.

Jamii ya kawaida imekuwa inabeza utajiri na kuuchukulia kama kitu kibaya. Hivyo sivyo tunavyouchukulia utajiri kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA.
Kwetu utajiri ni kitu kizuri na kitu muhimu.
Kwa sababu tunajua utajiri ni matokeo ya thamani kubwa tuliyozalisha kwa wengine na siyo kwamba tumewapora wengine.

Tunaupenda utajiri na hivyo tunauvuta zaidi uje kwetu, kwa kuwa tayari kutoa thamani kubwa na kuwa tayari kupokea pia.

Pia tunafanya maamuzi sahihi ya kulinda utajiri ambao tumeshaupata badala ya kuuacha upotee hovyo tu.

Tukimalizia na HEKIMA,
Hii ndiyo ulinzi wa mafanikio tunayokuwa tumeyajenga.
Matatizo mengi kwenye maisha ni matokeo ya kufanya maamuzi bila ya kutumia hekima.
Mtu unasukumwa tu kufanya maamuzi na wengine au kwa hisia na baadaye yanakuwa tatizo kwako.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunaweka kipaumbele kikubwa kwenye hekima, kujijengea hekima ili kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua sahihi.

Hakuna uhaba wa maarifa kwenye zama tunazoishi sasa, maarifa yapo tele na yanapatikana kwa urahisi kabisa. Unaweza kujua chochote unachotaka kujua.
Kinachokosekana ni kufanyia kazi yale maarifa ambayo mtu unapata.
Na hapo ndipo hekima inapokuja, makosa mengi ambayo watu wanafanya siyo kwa sababu hawajui, ila kwa kuwa wamekosa hekima.

Kwa kujijengea hekima na kuitumia kufanya maamuzi utaweza kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, hivyo ndivyo vipengele vitatu muhimu kwenye mwongozo wa kufanya maamuzi sahihi kwa mafanikio yako. Vifanyie kazi kila siku na utaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Kama ungependa kupata usimamizi wa karibu katika kuishi mwongozo huo, na kama ungependa kuzungukwa na wengine wanaoishi mwongozo huo, basi karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni jamii ya tofauti na ya kipekee kabisa ya watu waliojitoa kufika kwenye mafanikio makubwa kwa kuishi kwa misingi sahihi.
Kwa kuwa ndani ya jamii hii unapata maarifa, hamasa na ushirikiano wa wengine ili uweze kufikia mafanikio unayoyataka.

Kupata nafasi ya kuwa kwenye jamii hii ya KISIMA CHA MAARIFA wasiliana sasa na 0717 396 253. Nafasi zilizopo ni chache na muda umebaki mfupi.
Mwisho wa kupata nafasi ya kujiunga ni tarehe 30/10/2021.
Chukua hatua sasa ili usikose nafasi hii.

Nikukumbushe pia kwamba kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO kimesheheni miongozo mbalimbali unayoihitaji ili uweze kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Moja ya vitu vikubwa utakavyojifunza kwenye kitabu hicho ni mchakato wa kufanya maamuzi sahihi.

Ufanyaji wa maamuzi ndiyo kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Ukianza kufanya maamuzi bora sasa, utaanza kupata matokeo ya tofauti kabisa.
Jipatie nakala yako leo ya kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO ili uweze kufanya maamuzi sahihi yatakayokupa mafanikio.
Kupata kitabu wasiliana na 0752 977 170.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.